Mkuu FDR Jr bahati nzuri nimeyaona majina ya majaji wateule kwenye gazeti la Habarileo.
RAIS Jakaya Kikwete ameteua majaji wapya 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia Juni 26 mwaka huu. Idadi hiyo inafanya majaji wa Mahakama Kuu kufikia 59, awali walikuwa 50, kabla ya kustaafu kwa Jaji Thomas Mihayo hivi karibuni. Mahakama ya Rufani ina majaji 16. Katika uteuzi huo mpya wa Rais Kikwete, majaji wanawake ni sita na wanaume ni wanne.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo jana Dar es Salaam, majaji hao ni Ferdinand Wambali aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eliamani Mbise aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu na Sekela Moshi, aliyekuwa Mkurugenzi Mahakama za Wilaya hadi Rufani.
Pia aliwataja majaji wengine walioteuliwa kuwa ni Fatuma Masengi aliyekuwa Mkurugenzi wa Mahakama za Mwanzo, Sivangilwa Mwangesi aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya Rufani; Pellagia Khaday aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Moses Mzuna aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Iringa.
Aidha, aliwataja majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu kuwa ni Hamisa Kalombola aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mbeya; Fredrica Mgaya, aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mwanza na Profesa Ibrahim Juma aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. Mei mwaka jana, Rais Kikwete pia aliteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu huku saba kati yao wakiwa wanawake