Kikwete asitisha uuzwaji wa shamba la mpira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete asitisha uuzwaji wa shamba la mpira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Mar 1, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=6][/h][​IMG] Rais Kikwete asitisha uuzaji shamba la mpira

  Steven William, Muheza

  RAIS Jakaya Kikwete imepiga marufuku kuuzwa kwa mwekezaji yeyote shamba la mpira la Kihuhwi Rubber Plantations, liliyopo maeneo ya Bombani wilayani Muheza, mkoani Tanga.Akizungumza kwenye ziara ya kutembelea mashamba ya mkonge ya Kumburu Estate Kwanyefu, Kibaranga na Bwembwera juzi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluk Ole Medeye, alisema kuna maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kuwa shamba hilo lisiuzwe kwa mtu yeyote, bali likodishwe kwa wawekezaji... Source: Mwananchi - Habari za Biashara
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete amewaagiza wawekezaji katika sekta za madini, gesi na mafuta, kuhakikisha misaada kwa jamii inayowazunguka inakuwa moja ya sera zao za kibiashara ili kutoa fursa ya wananchi kufaidika na rasilimali zao.

  Kikwete atetea waishio kuzunguka migodi
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni hatua nzuri ili wakimaliza mkataba wao wanaondoka na shamba linabaki kuliko kuuza kabisa ambapo hata ardhi inakuwa mali yao.
   
 4. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mbona yuko kimya kutaifisha migodi na machimbo ya gasi yasiyo na faida kwa WaTZ?
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  TAMUCHUNGU NA KENGEMUMAJI, kwa pamoja mna IQ ambazo zote ni BELOW 20 ambapo kitaalam mnatakiwa muitwe IDENTICAL ******. Na pia nashukuru JF imepata mapacha wa akili. Mungu awape maisha marefu OUR ******!
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tamuchungu,

  Hilo shamba la mpira lilikuwa mali ya General Tyre (EA) Ltd lilianzishwa mahsusi kwa minajili ya kupunguza gharama za uagizaji mpira nje ya nchi pia kuzuia matumizi ya fedha za kigeni U$ kwa malighafi zinazoweza kupatikana nchini.

  Shamba liliamishiwa NDC kimjini mjini baada akapewa msomali ambae badala ya kuuza mpira General Tyre akawa anapeleka YANA na kampuni ya Bata zote za Kenya.Muda umepita sasa baada ya General Tyre kuuwawa sijui mpira shamba la mpira nani analitafuna hii ndiyo Tanzania bwana.

  Namsifu sana Mwl J K Nyerere aliona mbali sera zake zililenga kutukomboa waliofuata kazi yao ilikuwa ni kuuza na kujisifu jinsi walivyouza mashirika yetu ya umma.

  Mungu ibariki Tanzania ipate kiongozi mwenye sifa kama za Mwl Nyerere.
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu kutokana na hii ccm au chama kingine?
   
 8. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kama kweli ana nia hiyo ni kwanini serikali isitoe kidogo pesa wanayokusanya kwa wenyeji hata kama ni 5% ya mapato?. Huwezi kuwalazimisha wawekezaji kusaidia wakati serikali ndiyo inachkua kodi zote na kupeleka Dar.


   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na mambo ya vyama angalia uwezo wa mtu,unafikiri CCM ya Nyerere ilikuwa nzuri kwasababu ya jina lake au sera zake hapana.CCM ya enzi za Nyerere ilikuwa nzuri kwakuwa ilikuwa na mtu mahiri,mwadilifu,asiye na tamaa za kujilimbikizia mali jina lake Nyerere.Mtu mkuu wangu ni muhimu halafu chama kinafuata baadae mtu mzuri ana uwezo wa kutengeneza chama kizuri tafakari.

   
Loading...