Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Mwananchi
Date::8/28/2008
Wastaafu Afrika Mashariki waandamana tena hadi Ikulu
Na Patricia Kimelemeta
WAASTAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana wameandamana hadi Ikulu wakidai malipo ya mafao yao ambayo mpaka sasa wanaona ni kitendawili.
Wazee hao walisema wataendelea kuandamana mpaka Rais Jakaya Kikwete atakaporudi kutoka katika ziara ya siku nne nchini Marekani ili aweze kuwasikiliza na kulipatia ufumbuzi tatizo lake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa wastaafu hao, Nathaniel Mlaki, alisema wameamua kufanya maandamano hayo kunatokana na serikali kushindwa kuwalipa haki zao badalayake wamekuwa wakiwazungusha bila sababu yoyote ya msingi wakati fedha zao zilishatolewa na serikali ya Uingereza.
Alisema muda mrefu umepita tangu waanze kufuatilia malipo hayo, bila kupatiwaufumbuzi huku viongozi wanaohusikana malipo hayo wakiwakwepa huku wakidai kuwa wanachambua madai hayo.
''Tumemfuata Rais Kikwete atupe najibu sahihi juu ya malipo yetu kama watatulipa au la na kama watatulipa ni lini, tunmeona kwamba wanatuzungusha tu tangu tulipoambiwa fedha zetu zimefika. Hiyo inaonyesha wazi kuwa wanataka kutudhulumu, tumechoka kuzungushwa,'' alisema Mlaki.
Aliongeza kwamba kila wanapopanga kuonana na Rais Kikwete, maafisa wa Ikulu wanashindwa kutoa ushirikiano ka kuwapangia muda ambao Rais anakuwa hayupo ikimaanisha kuwa wanawadanganya na kuwazungusha kwa makusudi.
Alisema mpaka sasa baadhi yao wameshafariki kwa ajili ya kukosa fedha za malipo ya huduma za matibabu, na wengine wanashindwa kufuatilia fedha hizo kutokana uzee, lakini hakuna hata mtu wala kiongozi anayejitokeza kuwasaidia kupata haki yao.
Alisema wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, Rais Kikwete alihaidi kulishughulikia suala hilo, lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ikimaanisha kwamba aliwadanganya.
Alisema kutokana na hali hiyo wameamua waende Ikulu ili waweze kupata msaada hata kama waatishwa au kupigwa na kupelekwa polisi wataendeleza madai hayo mpaka hapo watakapoliwa.
Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na shida zinazowakabili na ugumu wa maisha, hali ambayo inawafanya baadhi yao kulala katika stesheni ya reli, kushinda na njaa na kuokota chupa za plastiki kwa ajili ya kuuza ili wapate fedha za kuendeshea maisha.
Agosti 21, mwaka huu, wajumbe wa waastaafu hao walikutana na maofisa wa Ikulu kujadili suala lao, lakini lilikuwa halijapatiwa ufumbuzi.
Ilipofika 22 Agosti mwaka huu, waastaafu hao na maofisa wa Ikulu waandike barua ya kuonana na Rais na kuhaidiwa waende Agosti 28 ya kupatiwa majibu juu ya maombi yao.
Wakati wanasubili majibu hayo, wastaafu hao wameamua kupiga kambi ikulu zaidi ya siku nne hadi Rais Kikwete atakaporudi katika ziara yake ya siku nne nchini Marekani ili waweze kushughulikiwa suala lao.
Ndugu zangu,
Miaka zaidi ya thelathini imepita na bado masikini wazee wa watu wanazungushwa. Awamu mbili zimepita na bado serikali ya CCM haioni wala umuhimu wa kuwajibika kwa hawa ndugu zetu. Mwaka wa tatu wa awamu hii unakatika na mkuu wa kaya bado anakata mbuga kuwakwepa wananchi wake. Wengi wa hawa wastaafu wameshafariki bila kuzifaidi pesa zao walizozitolea jasho.
Kwamba hawa MAFISADI watarudishwa tena madarakani mwaka 2010 na watanzania hao hao wanaoibiwa kila kukicha, ni jambo linalohitaji akili zisizo za kawaida kulielewa. Kwamba tuna bunge linalowakilisha na kutetea wananchi na kusimamia serikali wakati yote haya yakitendeka, ni ukweli ambao unahitaji ujasiri uso wa kawaida kuukubali. Kwamba kuna mahakama inayotafsiri sheria na kutoa haki kwa mwananchi akidhulumiwa, ni uchungu unaohitaji miujiza kuuvumilia.
Lakini hii yote ni kwa sababu Tanzania ni nchi ambayo imekumbatia sera ya wizi na rushwa. Viongozi huchaguliwa kulingana na uwezo wao wa KIFISADI iwe serikalini, bungeni hata kwenye mahakama. Sera kubwa ya viongozi wa nama hii ni kuweka kando utawala wa kisheria na kuwezesha maovu kushamiri miongoni mwao kwa kulindana. Wasilojua ni kuwa historia ina tabia nzuri sana ya kuwapa mgongo siku ya kiama. Hiyo siku inakaribia hapa Tanzania na anayeweza kusikia na asikie.