Kikwete apaa kutumbua US, Wastaafu wa EAC wasota milango ya Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete apaa kutumbua US, Wastaafu wa EAC wasota milango ya Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Aug 29, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwananchi

  Date::8/28/2008
  Wastaafu Afrika Mashariki waandamana tena hadi Ikulu
  Na Patricia Kimelemeta

  WAASTAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana wameandamana hadi Ikulu wakidai malipo ya mafao yao ambayo mpaka sasa wanaona ni kitendawili.

  Wazee hao walisema wataendelea kuandamana mpaka Rais Jakaya Kikwete atakaporudi kutoka katika ziara ya siku nne nchini Marekani ili aweze kuwasikiliza na kulipatia ufumbuzi tatizo lake.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa wastaafu hao, Nathaniel Mlaki, alisema wameamua kufanya maandamano hayo kunatokana na serikali kushindwa kuwalipa haki zao badalayake wamekuwa wakiwazungusha bila sababu yoyote ya msingi wakati fedha zao zilishatolewa na serikali ya Uingereza.

  Alisema muda mrefu umepita tangu waanze kufuatilia malipo hayo, bila kupatiwaufumbuzi huku viongozi wanaohusikana malipo hayo wakiwakwepa huku wakidai kuwa wanachambua madai hayo.

  ''Tumemfuata Rais Kikwete atupe najibu sahihi juu ya malipo yetu kama watatulipa au la na kama watatulipa ni lini, tunmeona kwamba wanatuzungusha tu tangu tulipoambiwa fedha zetu zimefika. Hiyo inaonyesha wazi kuwa wanataka kutudhulumu, tumechoka kuzungushwa,'' alisema Mlaki.

  Aliongeza kwamba kila wanapopanga kuonana na Rais Kikwete, maafisa wa Ikulu wanashindwa kutoa ushirikiano ka kuwapangia muda ambao Rais anakuwa hayupo ikimaanisha kuwa wanawadanganya na kuwazungusha kwa makusudi.

  Alisema mpaka sasa baadhi yao wameshafariki kwa ajili ya kukosa fedha za malipo ya huduma za matibabu, na wengine wanashindwa kufuatilia fedha hizo kutokana uzee, lakini hakuna hata mtu wala kiongozi anayejitokeza kuwasaidia kupata haki yao.

  Alisema wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, Rais Kikwete alihaidi kulishughulikia suala hilo, lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ikimaanisha kwamba aliwadanganya.

  Alisema kutokana na hali hiyo wameamua waende Ikulu ili waweze kupata msaada hata kama waatishwa au kupigwa na kupelekwa polisi wataendeleza madai hayo mpaka hapo watakapoliwa.

  Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na shida zinazowakabili na ugumu wa maisha, hali ambayo inawafanya baadhi yao kulala katika stesheni ya reli, kushinda na njaa na kuokota chupa za plastiki kwa ajili ya kuuza ili wapate fedha za kuendeshea maisha.

  Agosti 21, mwaka huu, wajumbe wa waastaafu hao walikutana na maofisa wa Ikulu kujadili suala lao, lakini lilikuwa halijapatiwa ufumbuzi.

  Ilipofika 22 Agosti mwaka huu, waastaafu hao na maofisa wa Ikulu waandike barua ya kuonana na Rais na kuhaidiwa waende Agosti 28 ya kupatiwa majibu juu ya maombi yao.

  Wakati wanasubili majibu hayo, wastaafu hao wameamua kupiga kambi ikulu zaidi ya siku nne hadi Rais Kikwete atakaporudi katika ziara yake ya siku nne nchini Marekani ili waweze kushughulikiwa suala lao.


  Ndugu zangu,

  Miaka zaidi ya thelathini imepita na bado masikini wazee wa watu wanazungushwa. Awamu mbili zimepita na bado serikali ya CCM haioni wala umuhimu wa kuwajibika kwa hawa ndugu zetu. Mwaka wa tatu wa awamu hii unakatika na mkuu wa kaya bado anakata mbuga kuwakwepa wananchi wake. Wengi wa hawa wastaafu wameshafariki bila kuzifaidi pesa zao walizozitolea jasho.

  Kwamba hawa MAFISADI watarudishwa tena madarakani mwaka 2010 na watanzania hao hao wanaoibiwa kila kukicha, ni jambo linalohitaji akili zisizo za kawaida kulielewa. Kwamba tuna bunge linalowakilisha na kutetea wananchi na kusimamia serikali wakati yote haya yakitendeka, ni ukweli ambao unahitaji ujasiri uso wa kawaida kuukubali. Kwamba kuna mahakama inayotafsiri sheria na kutoa haki kwa mwananchi akidhulumiwa, ni uchungu unaohitaji miujiza kuuvumilia.

  Lakini hii yote ni kwa sababu Tanzania ni nchi ambayo imekumbatia sera ya wizi na rushwa. Viongozi huchaguliwa kulingana na uwezo wao wa KIFISADI iwe serikalini, bungeni hata kwenye mahakama. Sera kubwa ya viongozi wa nama hii ni kuweka kando utawala wa kisheria na kuwezesha maovu kushamiri miongoni mwao kwa kulindana. Wasilojua ni kuwa historia ina tabia nzuri sana ya kuwapa mgongo siku ya kiama. Hiyo siku inakaribia hapa Tanzania na anayeweza kusikia na asikie.
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kejeli sana ukizingatia wastaafu hawa walibembelezwa sana kumpigia kura Muungwana kwa ahadi ya kushughulikia matatizo yao. Leo umepata ulichotaka unaacha mlangoni kwako huyooooo Marekani. Wazee hawa mwaka 2010 wataombwa tena kumpigia kura huyo huyo kwa ahadi nyingine mpya.

  Tafakari...............................................!!!
  Amua..................................................!!!
   
 3. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  I hate mifisadi whatever name you call it. Lakini naona kama ni vicious circle kati ya ufisadi na serikali kutowatendea haki wastaafu. Hivi hawa wastaafu wa East Africa kama wangekuwa mafisadi wakati huo leo hii wangepiga kambi hapo IKULU? Ni njaa inasumbua!! ndiyo maana waajiriwa wote wanajitengenezea pension n kabla ya kustaafu na matokeo yake wanatumbukia katika ufisadsi.

  DAWA ni kuchagua watu makini watakaokomesha hali ya kunyanyasa wastafu na kuweka sera sahihi na nzuri ya kuwaenzi wastaafu na sio ex presidaa na mpm whiel they wre fisadi as well SHAME
   
 4. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kutoka katika gazeti la TANZANIA DAIMA jana....................Dk. Slaa awalilia wastaafu EAC
  MBUNGE wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ametishia kuondoa shilingi katika bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kama hatapatiwa majibu ya kuridhisha kuhusu malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
  Dk. Slaa alisema alishauliza suala hilo mara saba sasa, lakini hapati majibu ya kuridhisha na kusisitiza kuwa safari hii asipopata majibu sahihi, ataondoa shilingi ili kukwamisha bajeti ya wizara hiyo. Dk. Slaa alisema taarifa alizonazo zinaonyesha kuwa Serikali ya Uingereza, ilishatoa fedha za malipo kwa wastaafu wa EAC kwa nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.

  "Ni jambo la kushangaza kwa nchi za Kenya na Uganda kwamba zilishawalipa wastaafu wake miaka mingi, tena kwa viwango vya dola kama walivyokubaliana, lakini hapa Tanzania bado tunasuasua kwanini?" alihoji Dk. Slaa.
  Pia alitaka kujua katika kipindi cha tangu kuvunjika kwa jumuiya hiyo, fedha za malipo hayo zilikuwa sehemu gani na zilikuwa zinatumika kwa kazi gani.
  Aidha, Dk. Slaa alisema kama kuna uwezekano, jambo hilo liundiwe Kamati ya Bunge kwani ni la muda mrefu na kila kukicha, malalamiko ya wastaafu yanazidi kuongezeka.
  Alisema mpaka sasa kiasi kilicholipwa kwa ajili ya wastaafu hao ni sh bilioni 117 wakati Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alishatoa ahadi ya kutenga sh bilioni 450 kwa ajili ya malipo ya wastaafu hao.
  Akijibu hoja ya Dk. Slaa, Naibu Waziri wa Fedha, Omar Yusuph Mzee, alisema Serikali haitawadhulumu wastaafu hao kwani kila anayestahili atalipwa. Naye Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema suala la ulipaji wa wastaafu hao, lilikuwa na mkataba na baadhi ya viongozi wa wastaafu hao walishafanya mazungumzo na serikali na kama kuna matatizo, yataangaliwa. Alisema katika mkutano wa Bunge Novemba, watakuja na majibu kamili kuhusu suala hilo au watatumia njia nyingine za kulitolea taarifa
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Huo mkutano wa Bunge Novemba utajadili mambo mangapi. Huu nao ni mchanga wa macho maanake usanii sasa umevuka mpaka - miaka 30 na ushee na bado ule ule ubabaishaji wa serikali unaendelea kwa ari, kasi na nguvu mpya. Itakuwa safi sana wabunge wakiendelea kulivalia njuga hii habari kuwasaidia hao wazee.
   
 6. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kutoka katika gazeti la TANZANIA DAIMA jana....................Dk. Slaa awalilia wastaafu EAC
  MBUNGE wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ametishia kuondoa shilingi katika bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kama hatapatiwa majibu ya kuridhisha kuhusu malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
  Dk. Slaa alisema alishauliza suala hilo mara saba sasa, lakini hapati majibu ya kuridhisha na kusisitiza kuwa safari hii asipopata majibu sahihi, ataondoa shilingi ili kukwamisha bajeti ya wizara hiyo. Dk. Slaa alisema taarifa alizonazo zinaonyesha kuwa Serikali ya Uingereza, ilishatoa fedha za malipo kwa wastaafu wa EAC kwa nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.

  “Ni jambo la kushangaza kwa nchi za Kenya na Uganda kwamba zilishawalipa wastaafu wake miaka mingi, tena kwa viwango vya dola kama walivyokubaliana, lakini hapa Tanzania bado tunasuasua kwanini?” alihoji Dk. Slaa.
  Pia alitaka kujua katika kipindi cha tangu kuvunjika kwa jumuiya hiyo, fedha za malipo hayo zilikuwa sehemu gani na zilikuwa zinatumika kwa kazi gani.
  Aidha, Dk. Slaa alisema kama kuna uwezekano, jambo hilo liundiwe Kamati ya Bunge kwani ni la muda mrefu na kila kukicha, malalamiko ya wastaafu yanazidi kuongezeka.
  Alisema mpaka sasa kiasi kilicholipwa kwa ajili ya wastaafu hao ni sh bilioni 117 wakati Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alishatoa ahadi ya kutenga sh bilioni 450 kwa ajili ya malipo ya wastaafu hao.
  Akijibu hoja ya Dk. Slaa, Naibu Waziri wa Fedha, Omar Yusuph Mzee, alisema Serikali haitawadhulumu wastaafu hao kwani kila anayestahili atalipwa. Naye Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema suala la ulipaji wa wastaafu hao, lilikuwa na mkataba na baadhi ya viongozi wa wastaafu hao walishafanya mazungumzo na serikali na kama kuna matatizo, yataangaliwa. Alisema katika mkutano wa Bunge Novemba, watakuja na majibu kamili kuhusu suala hilo au watatumia njia nyingine za kulitolea taarifa
   
 7. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawa wazee si ndio waliandamana juzi kati wakisherekea hotuba ya Kikwete?
  mimi naona sawa tu, maana hao ndio wale wale wakiitwa kwenye Diamond wanakimbilia mara moja, na kikwete anafanya hivyo akijua kuwa hamna la kumfanya kwa sababu ya dhiki zenu mtampigia magoti tu.

  swala hapa ni kujiunga na mitandao ya alQaeda na kuanza mambo ya kiukweli ukweli kwa viongozi wote mafisadi na mafisadi wote wa nchi yetu
   
 8. L

  Lione Senior Member

  #8
  Aug 29, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo la nchi hii,uzee ni sehemu ya balaa,ndo maana ufisadi hauishi kwani hakuna atakae kuzeeka vibaya,totoz,utazihonga nini?
   
Loading...