Kikwete and team, tuachieni nchi na chama salama

Teamubwabwa

Senior Member
Jul 7, 2015
172
59
Kauli za membe sio njema kwa mustakabali Wa taifa letu. Namuomba mhe JK na wenzako aakina membe mutuache ssalama. Membe lazima aonywe na ccm sio mfano mzuri kwa uongozi mahala popote pale hata kama ni haki Yake kikatiba.

Magufuli ana miezi 2 na nusu tangu aanze kazi. Sasa kukosolewa huku kwa muda mfupi hivi nini hasa lengo lake?

Ni nani anayekuunga mkono mpaka ujihisi uko sahihi kukosoa rais anayekuzidi cheo kiserikali na hata kichama?

Chondechonde tuachieni nchi na chama chetu ccm salama salmini.
 
Huyu membe anatumwa...na anayemtuma anamdanganya...amwache rais afanye kazi bila pressure
 
Michezo ya ccm ni mingi mpaka ni vigumu kujua upi ni halisi upi ni fekelo
Na ndiyo strategy yao wanayo ipenda sana ,wanaweza kuweka ukweli hapa na uongo pale halafu wanawaacha muangaike wenyewe wao wanajua wanachokifanya ,pamoja na mambo mengi ya kipuuzi hawa jamaa wako smart sana
 
Na sasa wanachofanya ni juhudi kubwa za kututoa kwenye hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, kuna mengi yatafuata hata vitisho vya ugaidi nk
 
Na sasa wanachofanya ni juhudi kubwa za kututoa kwenye hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, kuna mengi yatafuata hata vitisho vya ugaidi nk
Ndio kazi ya kitengo chao pendwa ambacho badala ya kusimamia serikali kimegeuka kitengo cha chama na kimsingi ndio kinaipa ccm nguvu ,vinginevyo sijui ingekuaje
 
Naona mzimu wa JK unazidi kuwafuata watu! Yaani mtoa maoni ni Membe lakini anahusishwa JK! Kwani alichoongea Membe ambacho ni cha ajabu sana ni kipi ionekane kwamba mwenyewe hana ubavu wa kukisema hadi atumwe na JK? Mbona hata huyo JK alikuwa anachwana hadharani na wala haikuonekana wanaomchana wanatumwa na third part? Hivi hii tabia ya kuwaona wanasiasa ni miungu watu wasiopaswa kukosolewa inawasaidia nini akina nyinyi ambao majority mpo thousands of miles away from the main circle? Halafu ni nyinyi nyinyi mlikuwa mnawaita wafuasi wa CHADEMA kwamba nyumbu kwa ku-support kila kitu hata ujinga; sasa nyinyi mna tofauti gani na hao manyumbu? Yaani huyo Magufuli amekuwa Mungu kwamba hapaswi kukosolewa? Yaani mnaamimi kabisa kwamba tangu aingie madarakani maamuzi YOTE aliyofanya ni sahihi kwa 100%? Amekuwa malaika?

Yaani hii nchi ningekuwa na mamlaka, ningepiga marufuku siasa kwa vijana manake badala ya kuwafanya wakomae kisiasa, wengi wao inawafanya wawe misukule ya wanasiasa. Na mabadiliko ya kweli nchi hii yatakuja baada ya watu hususani vijana kuacha kuwa misukule ya wanasiasa na vyama vya siasa! Lakin kama upuuzi wenyewe ndo huu wa kuunga mkono kila kitu kilicho in favor of vyama vyetu na wale wanaotufanya tufikirie kama misukule na kupinga kila kitu kilicho against vyama vyetu na vilivyo against wale wanaotufanya tufikirie kama misukule; trust me, kwa staili hii mabadiliko ya kweli hayawezi kutokea hata kama Magogoni anakaa nani! Hayatatokea mabadiliko ya kweli kwa sababu karibu viongozi wote, wawe wa CCM na serikali yake au wawe wa upinzani; majority wana matatizo yale yale; na nyuma yao tayari kuna kundi la watu lililokaa tayari kutetea kila watakachofanya hata kama ni ujinga na kupinga kila kitakachosemwa dhidi yao hata kama kina mantiki! Mbaya zaidi, majority ya wanaopiga kelele wenyewe wala sio wanufaika wa mfumo...
 
Kauli za membe sio njema kwa mustakabali Wa taifa letu. Namuomba mhe JK na wenzako aakina membe mutuache ssalama. Membe lazima aonywe na ccm sio mfano mzuri kwa uongozi mahala popote pale hata kama ni haki Yake kikatiba.

Magufuli ana miezi 2 na nusu tangu aanze kazi. Sasa kukosolewa huku kwa muda mfupi hivi nini hasa lengo lake?

Ni nani anayekuunga mkono mpaka ujihisi uko sahihi kukosoa rais anayekuzidi cheo kiserikali na hata kichama?

Chondechonde tuachieni nchi na chama chetu ccm salama salmini.
Ungesema kauli za membe ni toishio kwa maendeleo ya ccm hapo ningekuunga mkono.....lakin kauli zake zina nia njema kabisa kws maendeleo ya tanzaniad yetu so mwache aongee ukweli,kwa maendeleo ya nchi acheni kuweweseka!!!!
 
Back
Top Bottom