GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 11
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila
Kinshasa:
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amewafukuza kazi watumishi zaidi wa umma nchini humokatika juhudi zake za kupambana na rushwa, usimamizi mbaya wa matumizi ya fedha katika idara mbalimba nchini humo ikiweno forodha na idara ya utozaji kodi.
Rais Kabila amewafukuza kazi wafanyakazi 119 huku wengine zaidi ya 2,500 kulazimishwa kustaafu.
Mwaka uliopita Rais Kabila aliwafukuza kazi ama kuwastaafisha watumishi wa umma wapatao 1,300 na majaji wapatao 100.
Rais huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amekuwa akipambana kuinua uchumi wa nchi hiyo na kupunguza madeni ya nje.
Rais Kabila anahitaji mapato zaidi kutoka katika miradi ya madini ambayo ndiyo uti wa mgongo wa taifa