Kikwete anasoma barua za wananchi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anasoma barua za wananchi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Nov 22, 2011.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Katika Pitapita zangu nikainyaka hii kutoka kwa wananchi, Je Mkuu kweli husoma Barua za Wananchi?
  Niliwahi Kuuliza Maswali katika website ya Serikali nikapewa namba ya kusubiti majibu,ni miaka 2 sasa

  source: Barua Kwa Raisi Kikwete Toka Kwa WANANCHI TARAFA YA NYANJA MAJITA MUSOMA VIJIJINI « Jaluo
  Barua Kwa Raisi Toka Kwa WANANCHI TARAFA YA NYANJA MAJITA MUSOMA VIJIJINI

  Kilio Chetu Kwako Mh Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
  Sisi wananchi wa Musoma Vijijini Tarafa ya Njanja Majita tunapenda kuleta kilio chetu kwako Mh. Rais tuliyekupigia kura wakati uchaguzi
  uliopita na ambaye tutakupigia kura uchaguzi ujao 2010 ili uweze kumaliza kipindi chako cha miaka Kumi katika madaraka.Tunakuomba usome waraka huu vizuri kasha utujibu sisi wananchi hata kupitia vyombo vya habari,hatutaki Mbunge wetu aje aseme kwa niaba yako kwani si mpenda maendeleo hasa huku Majita.


  Tarafa ya Nyanja ina Kata 12 ,na kila kata kuna shule zaidi ya moja,Tarafa hii inasifika sana kwa uvuvi wa samaki na dagaa hasa kule
  Busekera,na baadhi ya vitiongoji vilivyopo kando kando ya ziwa . Wananchi tunachangia kulipa kodi ya serikali kama itavyotakiwa
  japokuwa hatujawahi kuambiwa ni kiasi gani cha kodi tumechangia katika mwaka wa fedha.
  Tarafa yetu hii imekuwa na matatizo mengi sana na sugu ambayo yametufanya tuachwe nyuma kimaendeleo ukilinganisha na upande wa pili wa musoma vijijini nazungumzia Butiama na vitongoji vyake . Nadhani hata wewe Mheshimiwa Rais ulipokuja kwenye Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Taifa miezi michahche iliyopita ulipata fursa ya kuonyeshwa maendeleo ya huo upande hasa kujengwa kwa shule za kisasa ambazo baadhi zao kuna Computer na madawati lakini kwa bahati mbaya Mbunge wetu hakuchukua jukumu la kukuleta wewe au mawaziri wengine katika tarafa yetu ili waone nini amefanya,huku majita hakuna kabisa alichofanya zaidi ya kutoa misaada ya mabati na genereta ambayo nayo ipo hapo takribani miaka mitano na itaoza.
  Matizo tuliyo nayo sisi wananchi ni mengi ambayo Mbunge wetu
  hameshindwa kuyatatua kabisa na kuegemea upande mmoja wa kwao. Naomba nianzie upande wa shule za Msingi kwa ujumla shule si nzuri na hazipo kwenye hali ya kuridhisha kabisa ,wanafunzi wanakaa nchi kutokana na ukoisefu wa madawati ,vyoo hakuna ,na isitoshe hata kama vyoo vipo basi vimejaa tayari Kwahiyo ,watoto wetu wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizo kutokana na kutokuwepo na vyoo safi .Mbali na hilo shule hazina madawati ya kutosha ambapo wanafunzi wanakaa kwenye mawe kama enzi ya Mkoloni.Walimu pia hakuna kabisa,mtoto anamaliza shule hafahamu hata kuandika au kuongea kiingereza sababu kubwa wanadai uhaba wa walimu ,vifaa vya kufundishia hakuna kabisa japokuwa tunalipa kodi zetu kwa Serikali ili tuweze kunufaika kodi yetu.Kwa kweli Mh Rais kama kuondoa ujinga katika tarafa yetu hii itakuwa ni historia.Tunasikia kwenye radio kuwa kumetokea ubadilifu wa pesa za ualimu,Serikali inawasomi kwani wasitatufe njia ya kufatilia ni walimu wangapi wamelipoti kazini na pia kuwe na unique namba za ku track record za walimu.

  Sekondari zipo 15 katika tarafa ya njanja ,tatizo ni uhaba wa ualimu hakuna ,vifaa hakuna vya kufundishia wanafunzi,mahabara kw ajili ya kufanya practical hakuna kabisa,watoto tunawalipia karo kila mwaka lakini inapofikia wakati wa kumaliza shule na matokeo yakitotoka ni
  zero ndiyo nyingi na wachache tu hawafiki hata 20 ndiyo wanachaguliwa kuendelea na kidato cha tano.Ili tatizo limekuwa sugu nenda rudi lakini hakuna uvumbuzi wowote ule,tumejaribu kumwambia Mbunge wetu amekuwa ni Mbunge wa kuturidhisha na vijibati vichache huku akiegemea kwake tu.Zaidi la hilo walimu hawaingii darasani kabisa na wanalipwa mishahara mwisho wa mwezi,kumbuka pesa ya mshahara niya walipa kodi.Inaumiza kama mlipa kodi hapewi huduma ya kuridhisha.Kadhalika amekuwa akijenga shule huko kwao tu na kupeleka wafadhili kuona maendeleo je huku majita hapaoni?na kama wafadhili wanatoa misaada je wanatoa kwao?Rais tusaidie ili na sisi Majita tuendelee.

  Hospitali ambayo ndiyo huduma muhimu hapa katika tarafa yetu ya Nyanja,cha kushangaza tuna dhahanati moja tu ya Mrangi ambayo
  imekuwepo hapa tangu enzi ya Mkoloni hadi leo na haijawahi kufanyiwa marekebisho ya haina yoyote yale wa upanuzi,Kweli Mh Rais fikiria
  tu,tangu enzi ya Mkoloni idadi ya watu itabakia kuwa ile ile?Hapana idadi ya watu imeongezeka sana kwa hiyo dhahanati hii ni ndogo sana na haiwezi kukidhi huduma kwa jamii kwa hiyo tunaishia kupoteza watu,Mbali na hilo wakina mama wajawazito wanakufa sana hasa wakati wa kujifungua,sababu kubwa ni ukosekanaji wa wakunga na vifaa au wakunga hawapati mafunzo ya kutosha na siyo tu wakina mama pia watoto wetu wanafariki kila kukicha kutoka na kutokuwa na Zahanati nzuri na kubwa yenye huduma bora zikiwemo na madawa, Zahanati yetu hii wakati wote haina madawa kabisa.Mbali na watoto kuna magonjwa mengine yanatumaliza bila sisi wenyewe kufahamu mfano,Kisukari,Ugonjwa wa Moyo,Shinikizo la damu, Malaria , Transmission disease. Kisa hakuna waganga,ma nurse, mahabara, madawa, pia choo hazilidhishi kabisa.Kwa kifupi hudumu hakuna kabisa wakina mama,watoto,wazee wanakufa kila kukicha,kwa wale walio na ndugu wenye uwezo ndiyo watasafirishwa kwenda Musoma Hospital kutibiwa japokuw ana yenyewe mpaka ufahamiane na mtu.

  Huduma ya Maji hakuna kabisa ,bado wananchi wanasafiri mile 10 kwenda kuteka maji ili aje atoe huduma nyumbani,Kweli serikali inashindwa kupata wafadhili wa kusambaza maji majita wakati ziwa lipo?Kama Musoma mjini wamepata wafadhili kutoka Ufaransa na wemetoa kiasi cha bilioni 14 ,je sisi tunashindwa nini?Mbunge anafanya kazi gani?Yeye ni kwao tu ,tumechoka Rais na Mh Mkono. Sisi wazee tunakuomba baba utuletee mfadhili wa kusambaza maji safi.Mpaka tunazeeka hatujawahi kuona bomba japokuwa enzi za mkoloni kulikuwapo na bomba.
  Barabara bado ni mbovu sana hasa ukizingatia tunatoa huduma ya uvuvi wa samaki huku ,wakati mvua zikinyesha inakuwa shida kubwa sana. Kwa ujumla barabara ni mbovu sana,kwa hiyo tunahitaji lami kama itawezekana Hatufahamu serikali inatoa kiasi gani cha pesa hasa katika tarafa yetu hii,sisi hatujui kabisa,tunasemewa na viongozi tu ambao hata kufika huku hakuna,report unayopewa niya uongo kwa wakandarasi hawajawahi kufika huku kujionea taabu tunazopata..
  Umeme hakuna japokuwa ,tunasikia kwenye vyombo vya habari ya kuwa serikali ya Marekani ilitoa pesa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini lakini na kama ni kweli sisi wananchi hatupati taarifa kabisa hata Mh Mkono hasemi chochote.Hayo ni baadhi ya huduma kwa jamii ambayo kwayo sisi wananchi wa Majita hatupati na hatufahamu tunapata fedha kiasi gani katika bajeti.

  Mh. Rais unaweza kutuuliza swali sisi wananchi kwanini hatujapeleka haya malalamiko kwa Mbunge wetu ili yeye aweze kuyafikisha kwenye
  vyombo husika vya Bunge?,Jibu ni kwamba Mbunge wetu ni shida sana kumpata ,pia anatudharau sisi wananchi kwa sabau hatujui kitu na
  hatujasoma ni kweli hatujaenda shule lakini ni vyema atusikilize sisi lakini cha ajabu ,anadiriki kusema kwetu kwenye ubunge hawezi kutoka
  kabisa hata msiponipigia kura ,anadai ataununua ubunge kwa gharama ya aina yoyote ile ili kwamba aendelee kubakia madarakani.

  Hii inamaanisha kuwa rushwa itatolewa kwa wananchi hasa kwa wale watakao rubunika ili kwamba wampigie kura mwakani aendelee kubakia
  Mbunge.Mbunge wetu anadiriki kudharau hata baadhi ya viongozi wa kata na Wilaya kwa sababu ya pesa aliyo nayo na kuleta mabati tu,na kutoa vijisenti kwa mfano alileta generator kwenye sekondari miaka mitano iliyopita baada ya muda akaleta simtank la lita 1000 kutokea hapo hakuna kitu chochote kile ,sisi kama wananchi hatuna uwezo. Japokuwa vyote vipo hapo havifanyi kazi anasubiri uchaguzi ufike amwage pesa,khanga na vitenge ili achaguliwe tena.RUSWA AU TAKRIMA

  Mh Rais sisi wananchi hatuelewi tunachangia kiasi gani kwenye kodi , na pia hatujui inatumika vipi,mbali na hilo serikali inatoa pesa kwakila wilaya lakini sisi tukimwuliza Mbunge wetu hatuambii kitu chochote kile,zaidi ya kutuambia nyie nyamazeni tutawaletea maendeleo wakati
  yeye anaishi Dar es Salaam kwenye jumba zuri,tunafahamu ya kuwa anazo pesa nyingi sana ambazo hata kama akitokea mtu mwingine wa kugombea atamshinda tu.

  Mh. Rais tumechoka kutawaliwa na watu wenye pesa kama hawa, hawatujali kabisa hasa pale wanapopata ubunge ,udiwani.Kazi yao ni kupeana posho lakini sisi wananchi tunaendelea kuteseka na hali ngumu ya maisha na kukoswa huduma kwa jamii.Tunashindwa kufahamu sisi tarafa ya Nyanja tunapewa kiasi gani cha pesa kutoka central government wakati wa budget,mbali . Mbali na hilo Mbunge ameshindwa kutuelezea matumizi ya pesa hizo ,Mkuu wetu wa wilaya hatujawahi kumwona zaidi ya kwenda ofisini kwake pale musoma Mjini.
  Mh Rais imefikia wakati tunataka serikali yetu iwe ya wazi kwa wananchi ili kwamba tufahamu ni nini kinachofanyika kwetu,wabunge na watenda kazi wanakula 10% kila kukicha,chukulia walimu hawaingii darasani lakini ikifika mwisho wa mwezi wanalipwa na kuna walimu wengi ambao ni hewa na wanaendelea kulipwa mishahara. Mh Rais kuna kipindi tuliomba jimbo ili likatwe mara mbili ili kwamba na sisi tuwe na mbunge wetu,lakini lilipofikishwa katika mkutano wa
  halmashauri kuu ya taifa ya CCM ,mbunge wetu alitupilia mbali hoja
  yetu.Sababu kubwa ni Tarafa ya Nyanja ina vyanzo vingi vya utajiri hasa samaki na dagaa ,pia kuna madini mbali na hilo kuna wapiga kura
  wengi .Kwa Mh Rais tunahitaji kwa lazima kwa kufuata taratibu za serikali ili na sisi tuwe na jimbo letu linalojitegemea. Mh.Rais
  tunahitaji jimbo ili likatwe mara mbili ikiwezekena iwe ni wilaya inayojitegemea.Au kuna sifa zinazohitajika kuwa wilaya?

  Mbunge wetu anapoenda kwenye vikao vya bunge hatusikii chochote zaidi ya kusema amejenga shule lakini ukitazama shule nyingi zimejengwa upande wa kwako ,hii inaonyesha ubaguzi ambao na sisi hatuutaki kabisa,na pia hatutaki tufikie kukatana mapanga kama ilivyokuwa Rorya.Tumemchoka Mkono
  Mh Rais kuna hii Basket Fund je na sisi tunafaidika vipi na huu mfuko hasa vijijini?Mbali na hilo hatuna huduma zingine kama bank,vituo vya
  polisi je lini huduma hizi zitawekwa?.Hata pia viongozi wa juu wa Serikali wakija wanafikia Butiama na Wilaya zingine au kusikia Rais ,
  Wawaziri ,Mkuu wa Mkoa amekuja kututembelea sisi wananchi zaidi ya kuishia Butiama,tatizo lipo wapi?Kwanini wajita wamesahaurika katika
  nyadhifa za juu za serikali hasa kwenye uwaziri na sekta zingine?Tangu wakati wa Mwl Nyerere mpaka leo hii bado tupo nyuma jetulikosea nini Serikali ya Jamhuri ya Muungano?.

  Mh Mbunge (Mkono) amekuwa akija kwetu hasa kwa sabubu ya uchaguzi ambao umekaribia,na kutoa vijipesa vidogo kwa wananchi na kuhaidi kutuletea au kuto mabati kwenye mashule ,Na pia kukutana na baadhi ya viongozi wa Tarafa na kuwapa pesa kidogo ili waanze kampeni taratibu kwa wananchi .Sisi tunasema hapana hizi pesa chafu hatuzitaki kabisa na hazituletei maendeleo katika tarafa ya Nyanja. Tunafahamu anazo pesa nyingi sana na anaweza kufanya chochote ili aendeleaa .
  Mh. Rais sisi wananchi na hasa kupitia wazee wetu ambao hawana uwezo wa kujieleza hasa kwa Kiswahili wameshindwa kuelewa uongozi wa huyu Mbunge tajiri Mkono,Kwani yeye ni Butiama tu na sehemu zake hasa upande wa kwao ndizo anazoendeleza na kutafuta wafadhili.
  Sisi hatutaki Mbunge tajiri tena mfanya biashara kwa sababu hawa ndiyo chanzo cha kuwepo na vurugu ,rushwa na pia hawatusaidii .Tunadhani kutoka na kauli yako ulisema wabunge wafanya biashara ndiyo mwisho wao wa kugombea ubunge kwani wanaharibu sifa ya nchi yetu Tanzaia ,wanatumia pesa zao chafu kutuharibia nchi na amani na utulivu tulio nao.Tunaomba kama ikiwezekana tume ya kudhibiti rushwa itumwe huku kwetu kutadhimini hali ya uchaguzi wa mwakani 2010.pesa chafu zinameanza kutembezwa.Tunafahamu ya kuwa Mkono ni mjumbe wa NEC ila hasitumie ubavu wake ili kwamba kwenyekura za maoni apitishe. Wajita tumechoka kununuliwa kwa pesa Mh.Rais tunahitaji maendeleo yanayoonekana na pia serikali iwe wazi inapotoa fedha hasa kwenye tarafa yetu.
  Kilio chetu tumekuwa nacho zaidi ya miaka 10 na hakuna ufumbuzi wa matatizo yetu inawezekana unaletewa reporti yenye kupotosha , kwahiyo sisi wananchi kupitia wazee wetu tumeona leo tuchukue jukumu la kukuletea wewe mh rais ili jambo kabla ya mwaka kuisha kwa kupitia vyombo vya habari,
  Tumemchoka Mbunge wetu kabisa japokwa anadai ya kuwa hakuna wa kumwondoa mpaka hapo atakapoachia madaraka,pesa anadai anayo na viongozi hakuna wa kumtoa hata wewe Rais .Tukimpigia simu kutoa shida anatujibu vibaya kiongozi gani asiye tujali sisi tuliomweka
  madarakani?.
  Mh.Rais uchaguzi umekaribia sana tunafahamu sana utashinda tena kupitia tiketi ya CCM na tutakupatia kura zote ila mbunge wetu hapana
  tunaomba mtupatie jina ili kwamba sisi wananchi tumchague ., tumechoka kununuliwa kwa pesa chafu ambazo hatujui zimetoka wapi , sasa Mh Rais tumeamka na macho yameona mbali .Tunasema , RUSHWA HAINA MAHALI PAKE TENA, Sisi Tarafa ya Nyanja tunaomba wananchi wenzetu walio na matatizo kama yetu hasa wa Vijijini tusinunuliwe kwa rushwa ya baiskeli kwani inatulemaza kabisa.


  Rais tunakuomba haya matatizo utupatie ufumbuzi wa kina hasa katika
  Tarafa yetu ya Nyanja na pia tunakuomba kabla ya kuanza kampeni uje Tarafa ya Nyanja na kama siyo wewe basi waziri Mkuu.

  Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2010
  WANANCHI TARAFA YA NYANJA MAJITA MUSOMA VIJIJINI


  Je RAIS ALIWAJIBU HAWA WANANCHI?
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi ungekuwa kiongozi wa nchi ungekuwa unasoma kila lawama na malalamiko? Hivi hujui kwamba kuna uongozi wa wailaya na mkoa ambao hiyo ndo kazi yake? Jifunze tena kidogo.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Kikwete hana muda mchafu. Akianza kusomasoma barua zinaweza kumuharibia vacation yake ya Bujumbura mwisho wa mwezi
   
 4. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  nimegundua humu JF kuna watu hata hawaelewi hii nchi inakwendaje,wengine wnakurupuka tu na kuleta topic humu ndani!
   
Loading...