Kikwete anapousifu ukoloni

Kikwete anapousifu ukoloni

mpinga shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,234
Reaction score
959
Ujumbe huu unasambazwa na MWALIMU mmoja aliyepata Shock baada kumsikiliza Kikwete

NITAFICHA WAPI USO WANGU KWA ALIYOSEMA RAIS?


Rais profesa Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari ikulu leo alimuambia rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu.

Rais ameniumbua.Sijui nitaficha wapi uso wangu. Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu historia huku nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema.Niliwaambia wakoloni walikuwa wakitunyonya, wa kitukandamiza na kutudhalilisha. Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.

Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga wakoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa ndio mashujaa wetu.Niliwasema vibaya wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama “HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA” na kunukuu sehemu ya “The Dar es salaam School of thought” kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni hawakutufaa.

Leo rais kaniumbua.Kama wanafunzi wangu wamemsikiliza rais nitakoma.Lazima watamuamini kwa sababu rais wetu ni profesa. Forwarded as received..
 
Duh! Hata mimi nimejisikia aibu ghafla!! Kumbe wakoloni walikuwa watu poa sana? Nadhani Mwalimu nyerere anajisikia aibu kuliko mimi na wewe huko aliko! Au labda alisema tu hivyo ili hao former colonist wasimfukuze huko kwao!

Si unajua anavyopenda kubembea kwenye bembea zao?au ni zile suti? All in all president ana sababu milioni za kuwasifu wakoloni, mimi, wewe na Nyerere hatuna macho ya kuona mazuri ya wakoloni hawa, kikwete ni profesa, unakumbuka hilo?
 
Sijaona hotuba yake kama kweli alisema ivo nadhani alikua hasomi alicho andikiwa.
 
Nyie mnafikiri huo Uprofessor aliupata bure? unaweza kuitwa professor kwa sababu tofauti, unaweza kupewa jina na kuitwa professor wa ujinga.
 
Tunaomba source ya hii habari.. Tusiaminishwe kuwa huyo mwalimu ndio source yenyewe.
 
Ukiwa ombaomba unaweza hata kumsifia mtu kuwa anamtia vizuri mkeo.
 
umwinyi, utwana na ubwana ni homa ya watu wa pwani, ( sasa namkubali Mugabe)
 
Tuseme tu ukweli, Ukitoa reli ya Mchina ya TAZARA, Tangu mjerumani aondoke kuna reli gani ambayo tumeijenga cc Watanganyika tangu tupate uhuru?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom