Kikwete anamfahamu Al Adawi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anamfahamu Al Adawi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Feb 21, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mdadisi yeyote ziara ya anayejihita mmiliki wa Dowans Brig.Gen.Al Adawi inazua maswali mengi kuliko majibu; kwanza kwanini hakutaka kupigwa picha?

  Pili katika hali ya kawaida R.A kama mwakilishi wake ndiye mwenyeji wake, hivyo alitakiwa awepo katika mkutano wake na wahandishi wa habari kwaajili ya kumtambulisha, inaonekana hilo halikufanyika.

  Tatu ameingia tu na mtambo mmoja wa Dowans ukawashwa. Haiwezekanikuwashwa huko kwa mtambo huo ukatokana na mashauriano ya siku moja.

  Inavyoelekea mipango yote tayari ilikwisha andaliwa, haya yanayotendeka sasa ni kiini macho, ndiyo maana kuna tetesi ya kwamba hata huyo anayejihita Brig. Gen. Al-Adawi uenda hasiwe mwenyewe bali kivuli chake.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ile pichaniloiona hapa jf nimehisi ni tofauti na nikoiona kupitia google images!
   
 3. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Kwani u never knew kuwa kila kitu kihusucho DOWANS ni fake?? so possible maana he'z one of thoz so called Wamiliki

  :rain::rain::rain:
   
 4. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Changa la macho mtakuja fumbua macho jamaa kesha chukua chake kasepa.

  Inasemekana amefuata cheki yake ya mabilioni ya dola za kimarekani.

  maana inabidi aisaini kbla ya kuitumbukiza benki, tehteh

  Swali> Mr. prezidenti is it true?
  Jibu> teh teh teh don't listen to radio mbao teh teh
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Sio mhusika kabisa huo ni mchoro JK, EL, RA, Ngereja na ridhiwani walikuwa wanaratafuta njia namna ya kuuwasha Ridhiwani amemfuata Dubai na kumleta, hao wahariri ni mataahira na wao watakaaje kwenye press conference na mmliki ambaye anakataa kupigwa picha siwangeondoka.

  Hii serikali ya kikwete imeshatupima nakutuona watanzania hatujitambui hatuna mbele wala nyuma wanaweza wakasema na kufanya lolote na umma usifanye kitu ndio maana Raisi wa nchi anaweza akashirikiana na mamafia kuangamiza nchi
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu mbimbinho mbona muda mwingi upo kwenye kioo ..au na wewe unachakachua ngozi yako (mkorogo) lol
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sarakasi
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280

  Mchoro wote umeshachorwa....kingine cha kushangaza ni kwamba tuliambiwa Dowans ina wamiliki sita. Wazungu wawili toka Canada, Muhindi wa kutoka India, Mkenya, Mkorea na huyo Al Adawi, lakini amejitambulisha kama yeye ni mmiliki pekee wa Dowans. Haijulikani hao wengine kama si wamiliki tena wa hiyo kampuni au ni kipi kilichojiri mpaka huyo Al Adawi asiwataje wamiliki wenzie.
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,852
  Likes Received: 11,973
  Trophy Points: 280
  Hayo ndiyo matapeli ya kimataifa nyie mwacheni tu siku wikileaks ikitoa mambo yake kanzu itampwaya ataikana Dowanzi.
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu BAK, yaani hapa ni mazingaombwe tu yanaendelea... hivi ina maana wale wengine wa5 ndo washamuuzia kila kitu huyu generali fake!!!! :A S 13::A S 13:
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii line inayomhusu Ridhwani kumfuata huyu bwana huko ughaibuni, is worthy pursuing; maana katika siku hizi za karibuni, hapa janvini, kulikuwepo na michapo iliyo elezea ya kuwa Ridhwani, wakati akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kwenda Dubei, alisindikizwa na msafara kama kiongozi mkuu kitaifai.
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  MAFISADI MKOME HII SINEMA YA HIVI SASA JUU YA DOWANS LAASIVYO
  TUKAPOROMOSHE 'MI-WIKILEAKS' ZAKE HAPA MPAKA MJISIKIE KUFAKUFA HIVI!!!

  Hawa wamiliki wa Dowans wa KUKODI wala hatudanganyiki!! Lowassa na Rostam Azizi, kaundeni mpango mwingine; huu hapa tayari umeanguka kwa pua.

  Na mkijaribu kubisha basi TUTAPOROMOSHA USHAHIDI KAMA MVUA HAPA kuliko hata ya Wikileaks mpaka mshangae wenyewe. Naona bora mkasimamishe hii sinema ya huyo Msaudia aliyeletwa nchini na Ridhiwani Kikwete tayari na makabrasha yote bandia, kabla hamjapata kuabika zaidi!!!!​
   
 13. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Me wala huya Al nani cjui hajanichosha kama hawa wahariri wetu..!! Mtu aitishe press conference afu agome kupigwa picha na wao bado wanaendelea kumsikiliza...!! Au alikua anagawa hela nini kiukweli me sipati picha hapa..!! Na kama ye ni mmiliki halali why agome kupigwa picha?? IM SURE HATA OSAMA AKIJA BONGO HAWEZI KATAA KUPIGWA PICHA WHY THIS FASHIST AGOME?? :blah:
   
 14. M

  Mhango Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkwere anajua kabisa Matanganyika ni maoga ya Mabomu ngoja wamlete General Kabisa ili mkae kimya maana mkisema jamaa wanaleta Makombora....hahaha Bongo tu waoga wanatutishia Mwanajeshi duh...Mkwere kweli hamnazo....
   
 15. M

  Mhango Member

  #15
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Haya Mambo ya Kina Balali kutowekwa habari zao watanzania lini tutakomalia?Eti jamaa hataki kupigwa picha wala TV hataki waonyeshe alivyo maana kila kitu kitakuwa openeed, ****** yao yataanikwa kina Kikwete na familia yake, Uongo mweupe, Sitaamini na sitaki kuamini kama Balali alikufaga, the same story like hii hapa...Nazidi kuichukia CCM
   
 16. M

  Mhango Member

  #16
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwanza hao waandishi nadhani walichukuliwa na CCM mtu wangu
   
 17. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni waandishi gani kwanza waliokuwepo kwenye hiyo press?ngojeni j5 tutapata mkasa kamili katika gazeti la umma la mwanahalisi au raia mwema.
  "kama richmond iliku fake,basi na dowans ni fake na wamiliki wake ni fake pia"
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Haijulikani ndugu yangu na ndiyo sababu akachagua kundi la waandishi wa habari wachache ili wamuulize maswali. Huyu mtu haishi Tanzania kawafahamu vipi waandishi wa habari wa kuwaita katika hiyo news conference yake ili wamuulize maswali? Ni mchoro mtupu huu lakini Watanzania tumeshaushtukia.....na ni lazima tuhakikishe hapati hata senti moja.
   
 19. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni vema tukajua ni vyombo vipi vya habari vilishiriki kwenye mkutano huo; hisije ikawa ni Habari Corporation na maswahiba wake aliowaandaa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita kwaajili ya kuchakachua habari za uchaguzi
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wakati Rithiwani anasindikizwa hapa majuzi na msafara wa kiserikali kwenda uwanja wa ndege alikuwa anaenda wapi? Labda tuanzie hapo..
   
Loading...