Kikwete anaanza kujisahau kwa kushangiliwa ama alikosea tu?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Kikwete akosolewa



na Happiness Katabazi


BAADHI ya wasomi, wanasheria na viongozi wa vyama vya siasa, wamemkosoa Rais Jakaya Kikwete kwa kuifanya Ikulu ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Hoja zao zimetokana na taarifa za Rais Kikwete kutumia ofisi ya Ikulu kwa ajili ya mkutano wa Kamati Kuu ya CCM, juzi.


Walisema kwa utaratibu, kikao hicho kilipaswa kufanyika katika ofisi za CCM, ama ofisi ndogo ya Makao Makuu, Lumumba, Dar es Salaam, au Dodoma yalipo makao makuu ya CCM, au pengine panapomilikiwa na kuendeshwa na CCM.


Baadhi yao walisema haya ni matumizi mabaya ya madaraka, hasa dhana ya kofia mbili zinazomfanya rais wa nchi kuwa Mwenyekiti wa CCM.


Mmoja wa watu waliokerwa na hilo ni mwanasheria mahiri, Tundu Lissu. Akizungumza na gazeti hili wiki hii, alisema kitendo hicho kimedhihirisha wazi kuwa Rais Kikwete ameshindwa kutenganisha kofia hizo mbili.


Lissu alisema ni makosa makubwa kufanyia vikao Ikulu, kwa kuwa ofisi hiyo ni mali ya umma, si ya CCM. Alisema kitendo hicho hakikubaliki katika nchi inayoongozwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa.


“Leo hii, Kamati Kuu ya CCM inathubutu kufanyia kikao Ikulu huku wakijua wazi wakati huu nchi ina mfumo wa vyama vingi, haya ni makosa na imeonyesha dhahiri rais wetu anashindwa kutofautisha kazi za chama zinapaswa zifanyike wapi na za serikali zifanyike wapi… namkumbusha kuwa sasa hivi tupo kwenye mfumo wa vyama vingi,” alisema Lissu.


Naye Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, alisema kitendo hicho kimedhihirisha wazi CCM inavyotumia vibaya mali ya umma.


“Ni upuuzi CCM kufanyia kikao chake Ikulu, kwa kuwa serikali hiyo hiyo ndiyo imeridhia kuanzishwa kwa vyama vingi… sasa leo hii wanajifungia kwenye Ikulu ambayo ofisi hiyo ni mali ya umma na kufanya kikao chao… nasema hivi Rais Kikwete tambua unawatumikia Watanzania na wanachama wa CCM, hivyo ni lazima utambue unatumikia mabwana wawili na wote unatakiwa uwatumikie kwa mujibu wa kiapo ulichokula cha kuwatumikia, la sivyo itafika wakati watakuhoji,” alisema Mrema.


Mrema alisema Kamati Kuu ya CCM ilishawahi kufanyika Ikulu wakati wa utawala wa mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa kipindi hicho nchi ilikuwa ni utawala wa chama kimoja.


Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, naye alimlaumu Rais Kikwete kwa kufanya hivyo, akisema ni vibaya.


“Kila siku NCCR inapinga mfumo wa chama dola, hivyo endapo mfumo huo ukibadilishwa haya yote hayatatendeka kamwe, na ninataka wananchi watambue jeuri ya CCM kufanyia kikao hicho Ikulu, inatokana na mfumo wa chama dola ambao tunaupinga… hivyo, wote tuupigie kelele mfumo huo ili ubadilishwe. La sivyo, mali za umma zitaendelea kutumiwa na CCM,” alisema Mbatia.


Mwingine aliyemlaumu Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, aliyesema rais ameshindwa kutofautisha kazi za siasa na za serikali.


Alisema hizi ni dalili kwamba rais anataka kufuta mfumo wa vyama vingi. Alisema Kikwete ameviteka vyombo vya habari nchini ili vimsifie na kumwandika vizuri kwa kumpa sifa za kutengeneza, ili aonekane bora kuliko waliomtangulia.


“Kitendo hiki ni cha aibu, na kimeonyesha wazi hajui kutumia kofia mbili alizonazo.


“Nia yake ni kutaka kuleta migongano na wafuasi wa vyama vya siasa kwa kuwa leo hii Kamati Kuu ya CCM imefanyia kikao chake Ikulu. Je, na sisi vyama vya upinzani tukitaka kufanya vikao vyetu vya kamati kuu tukafanyie Ikulu?” alihoji Mtikila.
 
Hao jamaa wa Usalama na Mzee tafiti hii mada vipi ? JK kulikoni hadi anafanyia U CCM kenye jengo letu na watanzanai tusio na vyama tunaamini katika Bendera na Katiba ya Nchi pekee ??
 
hapa kwa kweli raisi amekosea. hiyo kamati kuu lazima walikunywa chai na vitumbua vya ikulu ambayo ni gharama kwa walipa kodi wa tanzania nzima.

kwanini kikao hicho kisifanyike CCM Lumumba? Sijui ni kazi ya nani kumshauri Raisi katika masuala kama haya. kuna mtu hakufanya kazi yake.

ukiacha ushauri nasaha, mambo madogo kama haya yanamshinda Raisi wetu kufikiria. sasa sijui masuala mazito yenye kuchanganya akili itakuwaje. haba na haba hujaza kibaba, yetu macho.
 
Tafiti vipi huyu mzee mshikaji wake RO ? Maana kaanza na kamati kesho atafanya nini pale Ikuku ndiyo kulewa madaraka na sifa ambazo anazitengeneza ? Huyu JK keshapata ukweli mbona asioma msamaha kwetu Watanzania tusio kuwa wana CCM ?
 
Back
Top Bottom