Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

HAKIKA CHADEMA NI CHAMA MAKINI TUNAKUHASHMU DOCTA WA UKWELI, TUNAKUOMBEA MUNGU AKUEPUSHE NA BALAA KAMA LILIMKUTA MWAKEMBE KWAN TUNAYOYASIKIA KUMUHUSU HYU DR. Mwenzako baada ya umaarufu mkubwa YANASIKITISHA Keep it up Kamanda
 

Kimbunga,
Mkuu umeshaambiwa kuwa na subra wakati muafaka ukifika umma utajulishwa. Sasa unataka uambiwe lini wakati mazungumzo bado yanaendelea? Hebu tuwe waungwana japo kidogo haya mambo yanafanyika kwa umakini na kwa maslahi yetu wote.
 
Sawa mkuu hapo tunaelewana. Tunataka elimu kama hii. Nadhani muda huu wamekuw makini hawakusaini communique manake wakati ule waliushangaza umma kwa kusaini communique na kesho yake wakaikana! Naona sasa kwamba mara ya kwanza walikosea na umuhimu wa Dr. Slaa kuwepo ulijidhihirisha. Kwa maana hiyo mkuu yale makubaliano yanakuwa null and void ab initio?
 


kama CCM ni gari lilishindwa safari mbona chadema mnadandia mkitaka kuwa miongoni mwa abiria wake.
 
Nafikiri hujafikiri vya kutosha kwa taarifa yako wananchi wamechoka na JK na uwezo wa kuandamana ni mkubwa bila kusukumwa na chama chochote ugumu wa maisha ndio unawasukuma kufanya hivyo isipokuwa CDM ndio wanawachelewesha kwa kuwapoza kama hivyo kukaachini kwanza kuongea na Rais amasivyo wangesha andamana muda mrefu tangu kipindi cha mgawo wa umeme mfano mdogo Mbeya walisha kaa barabarani tayari CDM ndio waliokwenda kuwaomba wasitishe hata hivyo maandamano yameirekebisha na kuitia adabu serikali ya CCM.
 
W.Slaa,
Kwanza pole sana kwa majukumu ya kichama pamoja na msiba...vile vile nakupa pongezi wewe pamoja na uongozi wote wa Chadema kwa kukutana na Rais ili kulitakia mema taifa letu.

Nadhani hakuna mtu aliosema kuwa mmewasaliti kutoka na nyie kwenda Ikulu..

Naomba nikuulize swali, kama unavyosema mwenyewe mnasukumwa na uzalendo na umma. wakati mnapanga kwenda Ikulu kuonana Rais, mlitoa taarifa kwa umma au mliamua nyie wenyewe tu kama chama?
 


smart moves by JK............for the first time he has attained a statesmanship image of a shaker of TZ politics .......always in-charge and willing to listen; so far, he scores an A in my score card.......................the question is what will he do with a myriad of advice percolating into his ear.............................
 
Kimbunga,
Mkuu umeshaambiwa kuwa na subra wakati muafaka ukifika umma utajulishwa. Sasa unataka uambiwe lini wakati mazungumzo bado yanaendelea? Hebu tuwe waungwana japo kidogo haya mambo yanafanyika kwa umakini na kwa maslahi yetu wote.
Ahsante Mwita Maranya. Kwa hiyo kutakuwa na mikutano mingine kadhaa? Yote heri tu ili mradi yote yafanyike kwa maslahi ya watanzania wote bila kuangalia vyama na maslahi binafsi. Lakini pia muwe makini kwa kuwa CHADEMA kama Chama kinaongea na Serikali ya CCM! Sioni viongozi wa CCM kwenye hiyo mikutano (nina maana ya secretariat), hayo watakayokubaliana na serikali itabidi yaende chamani. CCM ikiyakataa itakuwaje? Tutaanza back to square one?
 

"null and void ab initio" hapa sidhani kama kamanda mwita amekuelewa!
 

jk tunamjua sisi bwana,kuna watu wanamuonaga jamaa kiazi,huwa wanakosea sana.Tusubiri tuone nini itatokea.
 
BAADA YA NDOA YA MKEKA INAYOSEMWA (CUF) KIKWETE ANATAFUTA NYUMBA NDOGO (CHADEMA:lol

Yaani nilikuwa nina mastress ya kufa mtu leo, ila hii post yako mkuu have made my day lol!
ivi mnatoa wapi haya maneno??
 
Mkuu kumbe nawe unafikiri? "nafikiri hujafikiri vizuri". Ngoma droo kumbe wote tunafikiri
 
ivi mbona mimi sizioni hizo picha, kama kuna mkuu anaweza kuzipost tena naombeni jamani.
 

Siasa si uadui, wameligundua lini hilo?
Ni juzi tu walikuwa wanataka kumtoa ikulu kwa 'nguvu ya umma' au siyo Chadema waliomkimbia bungeni?
Au ndiyo wanasiasa vigeugeu.
 

Kimbunga,
Ni muhimu ukatambua kwamba mimi ni mwanasiasa ninayefanya siasa nikiwa ndani ya siasa, ni mwanachama na kiongozi wa chama. Ninshiriki siasa kwa mikono yangu, najua ninachofanya na kinachotokea ktk siasa.
Mimi si mtazamaji wa siasa kama walivyo wengi wetu hapa JF ambao kazi yao ni kupiga makelele tu kama mashabiki wa mpira bongo wanachojua ni kuwaambia wachezaji piga mbeleeeeeee!!!
Ni kweli ktk siasa chochote chaweza kutokea kwakuwa hakuna adui ama rafiki wa kudumu ktk siasa! Na kadri muda unavyokwenda mwanasiasa makini unafanya tathmini na kujua mwelekeo sahihi wa wenzako na chama kwa ujumla.
 
unataka maji yaliyokamilika au nusunusu na kama ni hivyo itaondoa umaana wake sasa wewe vutasubila kama dr alivyokwambia iliupata majibu yaliyokamilika hata kama unataka kuyafanyia kazi ufanye kazi iliyokamilika mkuu.
 

Dr Slaa
Angalau sasa naweza kupumua kwa majibu yako ya matumaini.Kilio chetu ni kuwa na katiba bora itakayotupeleka miaka 100 mbele.Katiba bora itakayoipeleka chadema ikulu 2015.Tuna Imani na wewe Dr.Tunaamini hutatusaliti na wala huwezi kukubali umakam wa Rais ukatusahau watu wako.
Pigana Dr tupo nyuma yako.Wana CCM sasa wanapata hofu wanapokuona ukifanya maandalizi ya nguvu kuingia ikulu ya magogoni 2015.Ndio maana wale vibaraka wao walioko hapa jamvini wanahaha sasa kutisha na kukejeli wapiganaji.
Nasema tenao songa mbele Dr tunakuamini.
Dr nikudokeze kidogo nipo huku Arumeru tangu jana jioni na kijana wako Joshua Nassari anaungwa mkono na idadi kubwa ya wana Arumeru.
 
mkuu kumbe nawe unafikiri? "nafikiri hujafikiri vizuri". Ngoma droo kumbe wote tunafikiri
mkuu nimetumia neno hilo nafikiri kwasababu sipo ndani ya ubongo wako, ninaona matokeo ya ubongo wako kwenye maandishi yako nasitaki kuamini kwamba wewe hujui halihalisi huku mtaani ya ugumu wa maisha usiokuwa na sababu ya msingi ambao nyie magamba mmeusababisha kwa kutofikiri kwenu vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…