Kikwete akumbana na zomeazomea Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete akumbana na zomeazomea Mbeya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mrefu36, Aug 30, 2010.

 1. mrefu36

  mrefu36 Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mjini Mbozi tukio la mgombea ubunge kuzomewa lilimkumba Dk Lucas Siyame baada ya kuitwa jukwaani na Kikwete ili awasalimie wananchi baada ya kumaliza hotuba yake fupi kutokana na kuwa na mkutano mwingine kwenye mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi ambao, hata hivyo, uliahirishwa hadi leo asubuhi.
  "Sipo peke yangu, jamani nawaombea kura pia madiwani, na mbunge,’ alisema Kikwete lakini kauli hiyo ilipokewa na kelele za wananchi waliokuwa wakipiga kelele kusema “maji, maji, maji, hatutamtaki huyo.”
  Wananchi hao walipiga mayowe hayo huku wakionyesha ishara ya vidole viwili ambayo ni alama ya Chadema, hali iliyomaanisha kuwa wanamuunga mkono mgombea wa chama hicho cha upinzani.
  Upepo wa kisiasa kwenye mji huo haujaikalia vizuri CCM kutokana na hali ilivyojionyesha dhahiri kwenye mkutano huo. Wakati baadhi ya watu walionekana kumkubali Kikwete, wengine walikuwa wakipiga miluzi na baadhi kuonyesha ishara ya vidole viwili.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  HABARI NDIYO HIYO NA HUKO NDIYO MBEYA wamechoka kudanganyika..............HATUKATAI KUDANGANYWA LAKINI KAMA NI KUDANGANYWA KILA MWAKA HIYO HAIOWEZEKANI..........WANAMBEYA WANAONESHA KWA VITENDO NA HUKO KWINGINE JE...KAzi kwenu.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huh!
  Yawezekana wameerevuka hawa wananchi!
  Huenda hatimaye wameona njia!!

  HOngera wajomba na shangazi zangu!..huh!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,990
  Trophy Points: 280
  Kikwete kweli hajui kusoma ala nyakati.
  Huko Mbeya watu walilala barabarani asipite, wakampiga na mawe.
  Bado anajipendekeza ili iweje?
  Awaachie CHADEMA wachukue mkoa wao.
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hayo ni ya kawaida kwenye msongamano. But mi ninavyojua mbozi na vwawa ni jimbo la Godfrey Zambi sa sijui SIyame alikuwa anpigiwa debe kivipi ye ni wa mbozi magharibi unyamwangani.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mbeya wamechoka!!! CCM kwishney!!

  Hongereni wana mBeya kwa kustua, na kuchukua tahadhari!! Hawa CCM ni donda ndugu. Haliponi ng'oooo.....

  Chagua Slaa, chagueni mbunge wa CHADEMA.
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hili lilitokea katika mji mdogo wa Tunduma kwenye Jimbo la Mbozi Magharibi.
   
 8. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Inatakiwa nchi nzima kuwazomea hao mafisadi, kila wanapopita. Juzi Jangwani walijaribu kukatisha matazngazo wakakutana na Peoples Power
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naona watu wengi hawajaielewa habari vizuri. Nashauri mnunue gazeti la mwananchi limeiandika vizuri kuliko huu umbeya uliopo hapa, Au ndo kujipa matumaini?
  Kama mjuavyo waandishi wetu wa habari wanaandika ili kuuza gazeti, Kichwa cha habari hakisanifu habari kamili ilivyo ndani. Sitaki kusema mengi, badi ni mchana nenda tu kanunue gazate achana na hii habari iliyochakachuliwa.
   
 10. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kikwete amewagawa sana watu wa mkoa wa MBEYA tangu aingie madarakani, na kama Chadema wataitumia vizuri nafasi hii, basi wana uwezo wa kupata kura nyingi sana za urais mkoani Mbeya. kuhusu wabunge, Mbeya wana kawaida ya kuchagua mtu na si chama, kwa mfano si rahisi kumshinda Mwandosya na Mwakyembe kwenye majimbo yao.
  CHADEMA wekeni nguvu pale, Mbeya walishamchoka Kikwete siku nyingi.
   
Loading...