Kikwete akiimba kimoyomoyo

Martinez

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Posts
525
Reaction score
161

Wizi na uwongo, ni ujanja nilorithi kutoka kwa mama yangu mimi, vyote mkagundua, mkaona silingani kabisa kuwaongoza.
Na kama haitoshi, mkakata kabisa na shina la mabango yangu mimi, eti kisa wizi, mkaona bora mniache mimi muende upinzani.
Naskia hivi sasa wote mpo chadema, mnatupa kadi za ccm na mnakuwa wa chama fulani, iliniuma sana, sana.
Naskia hivi sasa wote mpo chadema, mnatupa kadi za ccm na mnakuwa wa chama fulani, iliniuma sana, iliniuma sana, sana.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.

Mngejua jinsi gani, machozi niliyolia kwa uchungu wa kura zenu nyinyi, mwenzenu jinsi gani, vile nimeumia moyoni. Hata jukwaa sitamani, utamu wa usanii mwenzenu imekula kwangu mimi, mwenzenu sina hamu, hata raha ya ikulu mi sioni.
Naskia hivi sasa wote hamnitaki, vile mkikaa hata mkiongea, mmeungana sana, sanaa. Mi mwenzenu Slaa huyu mi sina hamu, tena nna mpango wa kuongea na shimbo, nataka aende mbali, nijiepushe na kero zake mi mwenzenu siwezi.

Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
 
Nimeiipeenda saaaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnnnnnnnnnnnaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
kaka hapo umemaliza kabisaaaaa...:A S thumbs_up:
 
Pia yuko anapata shida watoto wake watakwenda wapi, make alidhani mambo yakienda sawa 2015 Ridhani anagombea Urais make January makamba atakuwa Katibu mkuu wa chama.
 
ki ukweli umeisuka kaka,nimeipenda bure,kama kwenda studio kutoa single nitachangia
 
Hahahaha! Imetulia mimi nimeimba kwa sauti na kwa sauti....Tatizo kwangu Slaa (Mbagala?). Ataipenda JK wao!
 
amekaa kama anafanya mtihani wa hesabu lakini amesahau kabisa fomula
 
Nimecheka sana! kumbe u mtunzi mzuri.
 
Usiku unakuwa mrefu kwake,ingekuwa hamu yake uchaguzi usogezwe mbele na kampeni ziwe 24hrs na Back up ya TCRA,PCCB,JWTZ iendelee kwa kishindo
 
Nimeipenda hiyo tungo maka huu ataimba sana maana washirika wake wa chama cho wamemuhama ,hata kingunge ameacha kushioriki siasa zake
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…