Kikwete akiimba kimoyomoyo

Martinez

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
525
160
images

Wizi na uwongo, ni ujanja nilorithi kutoka kwa mama yangu mimi, vyote mkagundua, mkaona silingani kabisa kuwaongoza.
Na kama haitoshi, mkakata kabisa na shina la mabango yangu mimi, eti kisa wizi, mkaona bora mniache mimi muende upinzani.
Naskia hivi sasa wote mpo chadema, mnatupa kadi za ccm na mnakuwa wa chama fulani, iliniuma sana, sana.
Naskia hivi sasa wote mpo chadema, mnatupa kadi za ccm na mnakuwa wa chama fulani, iliniuma sana, iliniuma sana, sana.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.

Mngejua jinsi gani, machozi niliyolia kwa uchungu wa kura zenu nyinyi, mwenzenu jinsi gani, vile nimeumia moyoni. Hata jukwaa sitamani, utamu wa usanii mwenzenu imekula kwangu mimi, mwenzenu sina hamu, hata raha ya ikulu mi sioni.
Naskia hivi sasa wote hamnitaki, vile mkikaa hata mkiongea, mmeungana sana, sanaa. Mi mwenzenu Slaa huyu mi sina hamu, tena nna mpango wa kuongea na shimbo, nataka aende mbali, nijiepushe na kero zake mi mwenzenu siwezi.

Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
Tatizo huyo Dr Slaa, Mara Epa mara madini, tatizo huyo Dr Slaa, mkaona uongozi siuwezi.
 
Nimeiipeenda saaaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnnnnnnnnnnnaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Pia yuko anapata shida watoto wake watakwenda wapi, make alidhani mambo yakienda sawa 2015 Ridhani anagombea Urais make January makamba atakuwa Katibu mkuu wa chama.
 
ki ukweli umeisuka kaka,nimeipenda bure,kama kwenda studio kutoa single nitachangia
 
Hahahaha! Imetulia mimi nimeimba kwa sauti na kwa sauti....Tatizo kwangu Slaa (Mbagala?). Ataipenda JK wao!
 
Usiku unakuwa mrefu kwake,ingekuwa hamu yake uchaguzi usogezwe mbele na kampeni ziwe 24hrs na Back up ya TCRA,PCCB,JWTZ iendelee kwa kishindo
 
Nimeipenda hiyo tungo maka huu ataimba sana maana washirika wake wa chama cho wamemuhama ,hata kingunge ameacha kushioriki siasa zake
 
images

Wizi na uwongo, ni ujanja nilorithi kutoka kwa mama yangu mimi, vyote mkagundua, mkaona silingani kabisa kuwaongoza. ..................

Wimbo wako mkuu Martinez uko poa kulingana na ulivyokuwa unajisikia lakini umekuwa UNFAIR AND UNCOUTH kwa maneno niliyo bold na ku-colour. Sitegemei mtu mwenye akili timamu kuandika maneno ya kashfa na dharau kwa mama yake JK. Wewe unamfahamu mama yake JK, kwanini useme JK karithi wizi wa mama yake, huyo mama aliiba nini???. Mimi nafikiri hatuandika kama kujifurahisha kwa ushabiki lakini tunatakiwa kuonyesha busara na hekima kwa yale tunayoandika badala ya kuandika ujinga ulionao kichwani kwako ambao hakuna mwenye akili timamu anaweza kuupenda.
 
Back
Top Bottom