Safi sana rais mstaafu nchi hii ni yako,umetumia vipawa vyote alivyokupa mwenyezi mungu kuongoza nchi kubwa Tanzania kwa miaka kumi,kisha ukamkabidhi mwingine mbele ya uso wa Walimwengu,wengine kwao imeshindikana,pumzika mheshimiwa hakuna binaadamu aliyezaliwa na mwanamke akawa mkamilifu,hongera na mapumziko mema.
Mbona ghafla, kutoka shopping za Mississippi,Michigan,London,Dubai na Shanghai mpaka mlimani city? Duh, hapo ni wiki mbili tu, naona mwezi mtukufu tutakutana pale Tandale kusaka futali!
Zote hizo ni mbwembwe tu na kutaka kuwahadaa wananchi kuwa wako pamoja nao;ila ukweli unabaki palepale kuwa wenzetu ni matawi ya Ilinois,Michigan,Mississipi,London,Dubai na kwingineko wanakostahili,so siyo kitu cha kushangaza kuwaona wakitokea Mlimani city maana viongozi wetu wameshazoea kutufanyia changa la macho,haukumbuki lile jamaa lilikuwa linaingia kula kwenye mighahawa ya kilala hoi na hata kulima wakati wa jua kali ili lipigwe picha na kutuhadaa kuwa chama cha kijani kinakula na kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi,yaani hii Tanzania ni balaa.