Kikwete ahaha urais 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ahaha urais 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Mar 3, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HARAKATI za kuwania urais zinahusishwa kuandaliwa kwa mtandao mpya wa Rais Jakaya Kikwete ambao unadaiwa unawarejesha baadhi ya wajumbe wake wa zamani, unampigia debe Spika Samuel Sitta na umetanuliwa hadi kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa vyama vya Upinzani, Raia Mwema imeelezwa.

  Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, juhudi hizo zinalenga kumfanya Rais Kikwete kupigiwa kura ya ‘ndiyo au hapana' kama ilivyokuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ili kufanikisha mpango huo, baadhi ya vyama vya Upinzani havitarajii kusimamisha wagombea urais na badala yake watajielekeza kwenye kuwania nafasi za ubunge.

  Mbali na mtandao huo mpya kutema wanamtandao wa zamani waliochafuka kwa kashfa za ufisadi, unatajwa pia kuhusisha baadhi ya wanaharakati na kundi teule la vijana katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi wakiwa karibu na familia ya Kikwete.

  Hata hivyo, wakati hayo yakitokea ndani ya CCM zimekuwapo taarifa kwamba baadhi ya vigogo wa chama hicho wanawashawishi wenzao kuchukua fomu za kuwania urais ili kumpinga Rais Kikwete, huku kukiwa na juhudi na mikakati ya kuwazima watu hao.

  Pamoja na juhudi hizo kupata vizingiti ndani na nje ya CCM, baadhi ya jumuiya za CCM ambazo viongozi wake wakuu wametangaza kumuunga mkono Kikwete.

  Inaelezwa kuwa wanaoshawishiwa bado hawajaonyesha nia dhahiri kukubali ama hata kukataa waziwazi ushawishi huo wakihofia kile kinachotajwa kuwa ni utamaduni wa CCM kumwacha Rais aliye madarakani kuongoza kwa mihula miwili.

  [​IMG]

  Rais Kikwete

  Sababu nyingine inaelezwa kuwa ni wanaoshawishiwa kumpinga Kikwete ndani ya CCM kujawa na hofu endapo wakishindwa hali itakayowagharimu katika nafasi nyingine za uongozi.

  Moja ya sababu zinazotumika kushawishi baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kumpinga Kikwete ni kile kinachotajwa kuwa ugumu wake katika kuamua masuala muhimu kwa Taifa, ikiwamo kusimamia misingi ya chama hicho katika kupambana na mitandao ya kifisadi ambayo si tu imejiimarisha CCM bali hata katika Serikali yake, kuanzia ngazi ya Baraza la Mawaziri.

  Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya CCM, katika vyama vya Upinzani wenyeviti wa baadhi ya vyama hivyo ambao wamekuwa wakigombea urais sasa wametangaza kuachana na azma hiyo. Miongoni mwao ni Freeman Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

  Mbowe anajiandaa kuwania ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ambalo alipata kuliwakilisha bungeni. Jimbo hilo sasa linashikiliwa na Mbunge wa CCM, Fuya Kimbita.

  Awali duru za kisiasa zilibainisha kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa ndiye atakayeteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho lakini sasa mpango huo haupo na Dk. Slaa anatarajiwa kuwania tena ubunge katika Jimbo la Karatu, ambako anatajwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa. Yeye mwenyewe amepata kukana waziwazi kuwa ana mpango wa kuwania urais.

  Sintofahamu pia imejitokeza katika Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho kimekuwa na kawaida ya kumsimamisha Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amewania nafasi hiyo mara tatu bila mafanikio makubwa.

  Sasa chama hicho kimekaa kimya kuhusu uamuzi wake wa kuweka au kutoweka mgombea ikidaiwa kuwa ki mbioni kuimarisha uswahiba na CCM.

  Uswahiba wa CUF na CCM umeanzia Zanzibar ambako ndiko iliko ngome kuu ya chama hicho kwa kiongozi mwenye nguvu na mzoefu, Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kukutana na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kabla ya kutaka Rais huyo aongezewe muda wa urais, msimamo ambao bado unaichanganya CUF na CCM sawia.

  Mbali ya uamuzi huo wa Seif, hatua ya Rais Kikwete kumteua msaidizi muhimu wa Seif, Ismael Jussa Ladhu, kuwa Mbunge, umeelezwa kuwa moja ya mikakati ya CCM kuimarisha mahusiano yake na CUF kwa kigezo cha kile kinachoitwa "maridhiano ya Kitaifa."

  Chama cha NCCR-Mageuzi ambacho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 kilimteua Dk. Sengodo Mvungi, kuwania urais bado kimebaki kimya huku Mwenyekiti wake, James Mbatia, akitangaza nia yake ya kuwania ubunge katika Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam, ambalo kwa sasa linaongozwa na Rita Mlaki wa CCM.

  NCCR-Mageuzi pia imekuwa ikitoa matamko kadhaa yanayoashiria kuonyesha kuwa chama hicho sasa hakina ‘ugomvi' sana na CCM baada ya Kikwete kuingia madarakani.

  Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) amekwisha kuweka wazi kwamba kiu yake ya urais imetoweka na kwa ajili hiyo hatowania urais, badala yake atakwenda kuwania ubunge katika Jimbo la kwao la Vunjo, Kilimanjaro linaloshikiliwa na Aloyce Kimaro. Mrema ni kati ya viongozi wa Upinzani waliokwisha kutangaza waziwazi kumuunga mkono Rais Kikwete.

  Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ambaye aliwania urais mwaka 1995 na mwaka 2000, aliona busara ya kwenda jimboni mwaka 2005, akafanikiwa kuwa mbunge, sasa anajiandaa kutetea nafasi yake hatua hiyo ikiacha chama chake bila mgombea wa urais.

  Katika harakati za kuzuia upinzani dhidi ya Rais Kikwete, mtabiri maarufu nchini Sheikh Yahya Hussein wa Dar es Salaam naye alijitumbukiza ulingoni kwa kutabiri vifo kwa ambao wangejitokeza.

  Ni ajabu kwamba kuna pilikapilika za kutaka Rais Kikwete awe mgombea pekee ikizingatiwa kwamba ana historia ya kuingia ulingoni tangu mwaka 1995 alipojitosa kuwania nafasi ya kupitishwa ndani ya CCM kabla ya kupitishwa Benjamin Mkapa.

  Katika hatua nyingine juhudi binafsi za Kikwete kwa kugharamiwa na baadhi ya rafiki zake zimekuwa zikielekezwa kuhakikisha makundi yanayotishia uhai wa CCM yanamalizwa huku akitumia nafasi hiyo kuwatumia vijana na watu wake wa ndani kufanya kampeni nchi nzima.
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwenye hii habari kuna ya kujiuliza, Kama ametenda kazi yake kwa mujibu wa katiba kwanini anahaha? kama amefanya mahamuzi kwa maslahi ya wapiga kura hofu ya nini? kama amesimamia vyema kushusha mfumuko wa bei shida ni nini? kama ameweza kuwezesha huduma bora mashuleni na hospitalini anawasiwasi gani tena?
  Ukitazama hayo yote utaona ayajatekelezwa for past five year, tangu mzee wetu Mkapa(japo alikuwa na mapungufu yake) aondoke. Sasa hana jipya kwa umma hivyo lazima ahahae.
   
 3. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  He promised a lot. He failed. Kazi anayo
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Kama taarifa hii ni kweli tatizo liko wapi JK au vyama vya upinzani??

  Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, juhudi hizo zinalenga kumfanya Rais Kikwete kupigiwa kura ya ‘ndiyo au hapana' kama ilivyokuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ili kufanikisha mpango huo, baadhi ya vyama vya Upinzani havitarajii kusimamisha wagombea urais na badala yake watajielekeza kwenye kuwania nafasi za ubunge

  kwa hiyo vyama havisimamishi wagombea kwa sababu ya JK kafanya mpango huo? mmethibitisha, najua opposition wako weak kama mlenda, ila siamini kbaisa kama wamemezeshwa sumu na JK wasigombee urais. hata kama leo hii Slaa atasimamishwa, kushindwa lazima ashindwe tu.

  Hii habari imaendikwa na mjasiriamali anayetaka kuuza gazeti kutokana na hali halisi ilivyo. impact ya aliyoyasema ni kuwa chama kipya kuingia madarakani ni lazima iwe miaka kama 100 ijayo!!
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Lini baadhi ya wapinzani ilitafsriwa kama wapinzani wote? Waberoya bana, hata spining huwezi?! chuki dhidi ya wapinzani (hasa chadema) naona inazidi kipimo cha maji ya kunywa.
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tuna kazi kubwa sana kuing'oa CCM, hivi tunaweza kutegemea kuwa mgombea uRais akae tu bila kuwa na mikakati ya kushinda. Na katika kuunda tume akiwepo Sita, Chenge ama yoyote ndani ya CCM, hakuna kustaajabu, manake mduara wa CCM ni uleule, wanajifanya wapiganaji nje, lakini wakishikwa tu mikia ndani wanakuwa wapole kama Simba.

  Na hii dhana kuwa upinzani utapata nguvu kwa kumeguka CCM inachelewesha mapigano. Wengi wa wapinzani walikuwa CCM, kwa hiyari yao ama kulazimishwa enzi zile za hupati chochote mpaka upate mafunzo ya CCM.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Yaani umeona ninaichukia chadema mpaka ufikie kiasi cha kuona ninaichukia?

  nani anasimamishwa kwenye ugombea wa urais wa Tanzania from chadema???

  Na msiposimamisha mwandishi atakuwa amesema ukweli kuwa ni mkono wa JK!

  Jaribu kusoma tena post yangu halafu uone kama nimesema Chadema kwa namna yoyote ile! au unaweza kunionyesha sentensi unayoona kuwa nimeisema Chadema!

  Hii post yako nimecheka sana, mimi nampinga mwandishi kusema kuwa wapinzani wasiposimamisha mgombea ni kuwa wamevutika kwa JK!

  Wewe unasema nimeandika kuhusu chadema! mwafrika vipi kaka, ukiiona post ya waberoya unajua tu anaichukia chadema!

  chadema siwezi kuwachukia kwa lolote lile, maana watanisaidia nini niwachukie au nisiwachukie? mkuu, I am not you! mimi natoa post kutokana na ninayoyawaza au kuyaamini. huwa siyumbi na ninachokisema, wala sina side!

  kwa hiyo baada ya kufuatilia post zangu umegundua ninapenda chama gani?? lol!

  sasa hapa umenichekesha sijui chadema imeingiaje hapa! ebu nionyeshe nilipoitaja chadema!! duh!!
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi utafanyika na wanachadema wataamua nani wa kusimama... ipe muda

  Nimeisoma vizuri sana na nimeona ukibaishia upinzani wote (kwa kuwaita mlenda) wakiwemo chadema. Niliwahi kukupa ushauri siku moja hapa ila ukakimbia bila kujibu, kama upinzani ni mchovu kiasi unachosema hapa kila siku, kwa nini wewe waberoya usianzishe chama cha upinzani ambacho kitakuwa imara na mfano kwa wengine wooote?

  Sababu za kuwachukia chadema unazijua vyema ila hiyo ni topic ya siku nyingine

  Hilo nalo ni swali? wewe ni maji ya kijani - chama cha mafisadi
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,412
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  sijaona sababu kubwa ya huyu mdengereko kurudi madarakani aliahidi ajira millioni moja kwa vijana sidhani kama hata nusu kafikia labda kama atajumlisha na wale matapeli wanaoiba benki na kuteka magari kule Kasindaga Biharamulo. Tatizo kubwa ni hawa wapinzani kutokuwa na msimamo wa thati wa kuwang'oa hawa jamaa nadhani ingekuwa vizuri kama wangemsimamisha mmoja. K'wetw atashinda lakini si kwa asilimia 80 kama 2005. Itashuka kuonesha alivyochokwa!
   
 10. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama issue ni udengereko hapa ! au wewe wasemaje mkuu
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,412
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Ni namna tu ya kumtambulisha wala sikuwa na maana kwamba ameponzwa na UNDENGEREKO mkuu. Asante Mwafrica!
   
 12. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna uwezekano mkubwa kwa JK kuwa mgombea pekee kama wapinzani (na ndani ya CCM) wataendelea kuweka mbele woga na maslahi binafsi zaidi ya ukombozi wa nchi.

  Wapinzani wanaona uwezekano wa kushinda ni mdogo kwa hiyo dawa ni kukacha kuweka wagombea imara, na Ndani ya CCM wanaogopa vibano kama wakishindwa na JK.

  Ningependa tu kuwakumbusha wote kuwa, hakuna kitu kinachobadilika bila kusukumwa. Ingawa kwenye kujaribu kuna kushindwa, ni muhimu zaidi kuelewa kuwa bila kujaribu hakuna uwezekano wa mabadiliko yoyote kutokea.

  JK needs to be challenged no matter how strong he is or the repercussions for doing so. Remember, even Hillary Clinton was once thought to be unbeatable, but was she?
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa mkuu ila tu nilikuwa najaribu kupata the best kwenye post yako na sio hilo la ukabila peke
   
 14. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wapinzani hao ni pamoja na Mbowe?
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  Nafikili Mtikila hawezi ku-acha kugombea, atagombea.
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280

  Duu
  huo ushauri ktk nyeusi hapo naukumbuka, lakini kumbukumbu zangu zinaonyesha zilitolewa na ID tofauti na mwafrika.teh teh teh teh
  Nirekebishe kama nimekosea.
   
 17. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .....Kama unadhani uko imara, kwanini uogope kupingwa?.....Kuna tatizo hapa, nadhani hata hao wanaompigia debe kwa maslahi yao binafsi wanajua hilo....
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kwani mimi nimezuia watu wengine kumshauri waberoya? Wewe ndiye labda unaweza kuweka uthibitisho kuwa mimi sikumshauri waberoya hapa (kama unao). Swala kwamba mkamap au luteni au mwanakijiji wametoa the same ushauri kwa waberoya haiondoi nafasi yangu kutoa the same.

  au wewe wasemaje?
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  CCM wanavyosemwa wangekuwa ndiyo wewe mkuu sijui ungejitundika! mbona kuna wanachadema wanadharau post zangu na kuona ni mtu tu anayetoa maoni yake?

  angalia sasa unapojiweka kwenye childish corner, kuwa ukimkosoa mtu basi inabidi uwe nafasi yake!

  So leo Mwafrika ukisema JK hawezi kuongoza basi jibu lake ukachukue nafasi ya urais? yaani ukikosoa tu inabidi uwe substitute ya uliyemkosoa! this is too cheap!

  Huwa nasema na nitarudia, vyama vya siasa vimelala, haihitaji degree kujua au kuamini hivyo, wala haihitaji kutuma post kubisha hilo, vinajieleza na kujionyesha! katika hao chadema wamo , so kama unaona post zangu zinakusumbua, pole sana, zitakusumbua sana mwaka huu na miaka yote ijayo. I will speak loud and clear!, kama wewe utapoteza muda wako kusubiri post ya waberoya inayoponda vyama , we subiri utazijibu sana, ila tafadhali uwe unazijibu kwa hoja!

  Inaonyesha una mengi unayoyajua kuhusu mimi, uwanja wa wazi huu wewe sema tu, kama unaona kuandika chochote inakupa raha!

  Nafurahi unanipa title ya kuwa mimi ni CCM, wa CCM nao wananichukia kama wewe!

  Mwafrika mkuu, tuliza boli, just think for a minute, ninaharibu nini chadema mimi kama waberoya? na je chadema wanagain chochote kutokana na hizi critics? kama hizi crititics hazileti faida kwa chadema, then what will be difference btn chadema and CCM?

  umekuwa kama Marmo si marmo, chiligati si chligati, makamba si makamba wa Chadema!!

  ukiona post zangu just consider I am a fool!! hakuna watu unaowaona na kuwadharau katika misha yako???, kwa nini mimi nisiwe mmoja wapo?, naomba uniweke kwenye hilo kundi, ukiona post zangu '' just say jinga hili'' maana utapata ugonjwa wa moyo, wengine tuna shock absrober ndiyo maana unaweza kucriticise vitu vilivyo wazi na tuko tayari kukosolewa vile vile!

  yaani toka mwaka 1995 kila mwaka uliofuatia vyama vinapata kura pungufu , wewe unaona hamna tatizo hapo! umerela!!x, because you like chadema so much. Halafu ukiona wana CCM wanampokea EL, RA na Chenge kwa mazuria unaona hawana akili, kumbe mko sawa kwa viwango na majina ya vyama tofauti.

  Dear Mwafrika, Chadema ikizibeba hizi critics na kuzifanyia kazi wanapata kura na tutashangilia wote, kuna faida gani ya kupeana matumaini pasipo na matumaini??

  Au umefikia level ya kuona leo hii mgombea wa chadema atakuwa threat kwa CCM huku kiongozi wenu shida salumu anasema JK forever!!
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh
  tatizo umetoa ushauri neno kwa neno, teh teh na wakati huo huo unataja id za kumshauri Waberoya zinazosharabiana sana kimtizamo na kimawazo.teh teh teh

  ni muono tu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...