Wewe Mwiba inaelekea jana hakula Daku!! Muda wa kufuturu unakaribia.
Makelele yenu mengi kama mnashangilia mpira tena ule wa kupitia redioni uliokuwa ukitangazwa kwenye idhaa ya biashara ya redio Tanzania anao anao goooal,wengi mmezaliwa juzi juzi hamuifahamu hio redio ,amini usiamini hapa JF kuna watu hawaijui senti tano ,ile ya nduaro.
Sielewi kile mnachokipinga kwa JK ,kama ni matatizo mbona yapo mengi tu kwa wengine ,hivi huko kwenye vyama vyenu hakuna matatizo ? Yaani Nyinyi mnaona mkiipata hiiNchi maisha mtayafanya yawe laini kama siagi ,mtapandisha mishahara siku tu mkiingia Ikulu ,hivi mnaota au mshakufa ?
Maendeleo ya JK kwa sasa yapo wazi kabisa ,hivi CCM ianzie tokea Tanu na ASP huko,wameiendesha Nchi hii kutoka kwenye shida na dhiki hadi leo wanaanza kuchimba mafuta na gesi ,itakuwa kosa kubwa sana kwa CCM kuziacha juhudi zake kwa wengine , Ukiangali JK ameweza na amewezesha karibuni itakuwa kila mtu ,WaTz wa leo ni matajiri kila mmoja anamiliki kajisimu cha mobile japo kimeo ,kinaitaji hela au sio ,unakakuta kapofull credit akiitajivocha.
Wengi tu sasa wanamiliki bodaboda na vyombo vya moto vya miguu miwili au mitatu vibajaji, kesho na kesho kutwa kila nyumba itakuwa na gari ndogo nje ,haya yote yamefumka katika kipindi kifupi cha JK.
Ikiwa wewe huoni kama hayo ni maendeleo basi utakuwa maiti inayotembea.