KIKWAZO CHA UFUMBUZI WA MGOGORO WA ZANZIBAR NINI HASA?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar unawaumiza vichwa watu kwa vile ufumbuzi wake umekuwa kitendawili. Tena kitendawili tega mfumbuzi afumbue, na mfumbuzi akishindwa basi hupewa mji wa mbali kwa alieweka kitendawili kutembelea na hatimae kitendawili hukiteguwa.

Kitendawili cha Zanzibar hakihitaji mtu kupewa mji kuteguliwa. Tukijuuuliza tu kwa nini wagombea wote wawili wamekuwa wagumu kuregeza misimamo yao ya kisiasa? Ni kwa sababu ya maslahi? hili linawezekana kutokana mitizamo mitatu tofauti lakini inayolingana

  1. mikataba ya kisheria (MoU) waliokubaliana kuhusu uchimbaji wa mafuta n a makampuni makubwa yenye ushawishi duniani yumkini ndio unaowavuruga wanasiasa hawa.
  2. Nchi nyengine kubwa duniani ambazo zinakodolea macho mikataba kama hiyo na kuona ufinyu wao kupata au kufikiriwa kushiriki katika mchkato huo nao wametia mikono yao. Ikumbukwe kuwa utafutaji wa mafuta na kuthibitishwa kuwepo umeshafanywa na serikali ya kikoloni ya kingereza kupitia BP Shell kwenye miaka ya 50 na viashiria hivyo kuwekewa "beacon" sehemu tofauti visiwani. Katika kitabu cha ramani"atlas" ya Zanzibar iliokuwa inasom eshwa mashule mwanzoni wa miaka ya 60, beacons hizo ziliitwa "oil reserve"
  3. mtizamo wa tatu ambao unaonekana una nguvu zaidi ni ule ulioweza kuharakisha kuliondoa kinyemela bila ya kufuata katiba suala la mafuta kuwa jambo la muungano. Hili limefanyika baada ya kuonekana kuwa kusubiri katiba mpya kutachukua muda mrefu au uwezekano wa kukwama.
Ni dhahiri kuwa mbadiliko wa uongozi utaathiri sana mitazamo hiyo na hivyo ni status quo tu. MAPINDUZI DAIMA

Nami nasema Zanzibar ni zaidi ya mafuta na gesi
 
Back
Top Bottom