Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,695
- 149,921
Hili ndio swali kila mmoja wetu analopaswa kujiuliza kwanza ndipo atapata mwanga wa nini kinaweza kufuatia hapo baadae kuhusiana na yote haya yanayoendelea na hasa katika kupata ukweli wa nini kilitokea.
Na hapa naomba niongeze jambo moja ili tuweze kutoka kwenye huu mkwamo.
Nashauri wakati umefika sheria /utaratibu unaozuia kujadili kila kitu kinachohusu jeshi na usalama wa Taifa ifanyiwe marekebisho.
Siku za nyuma niliwahi leta mada hapa JF nikipendekeza baadhi ya taarifa zinazohusu idara ya usalama wa Taifa iwe zinajadiliwa Bungen kwani sitaki kuamini kuwaa kila kitu kinachofanyika katika hii Idara ni siri na umma haupaswi kujua.
Mada hiyo unaweza kuisoma kupiti hii link hapa chini:
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa awajibike kwa Bunge pia
Pengine hii "taboo" ya kutojadili kila kitu kinachohusu hii Idara na hata Jeshi ndio chanzo cha yote haya kwasababu hii taboo sasa inakuwa ni kama kinga.
Labda niulize.Hivi nchi zote duniani kila kitu kinachohusu usalama wa Taifa au Jeshi hakijadiliwa Bungeni?
Mnakumbuka habari ya kivuko kibovu kuhamishiwa iliko hamishiwa?
Hata Hoja ya zitto ya kutaka maswala haya yachunguzwe kwa kuundiwa chombo maalumu na Bunge nawambieni mapema kabisa kuna weza kukawekwa mashariti na kwa mtazamo wangu shariti mojawapo ni linaweza kuwa Chombo au Tume hiyo itakayoundwa kutoruhusiwa kuchunguza wala kujadili chochote kinachohusu hiyo Idara kwasababu teyari ni taboo.
Nashauri baadhi ya mambo ambayo hata yakiwekwa wazi kwa umma kuhuusu TISS au Jeshi hayawezi kuleta madhara yoyote kama tulivyoona Bungeni leo,yawe yanajadiliwa na tuwe na sheria inayoruhusu jambo hili na inayoweza kutamka /kutaja ni mambo gani yanayohusu idara hizi yanaweza kujadiliwa Bungeni kwa uwazi bila kuleta athari yoyote kwa nchi.
Mfano.kwasababu hakuna alie juu ya sheria,ikitokea watendaji wa idara hizi wamevunja sheria za nchi basi tuhuma au taarifa za aina hiyo ziweze kujadiliwa hata ndani ya Bunge.k
Hebu tujiulize.Kama tuhuma za Zitto kuwa Idara hii ndio ilihusika kuvamia kituo cha Clouds ni za kweli, kuna ubaya gani Bunge kutaka kujua ni nani alihusika kuagiza askari wale wavamie hicho kituo?
Unajua kwasababu hakuna uwazi katika kujadili mambo yanayohusu hii Idara matokeo yake yanaweza kuwa ni makosa ya mtu mmoja tu kuchafua taasisi nzima kwasababu wananchi wanakuwa hawajui ukweli na nani anahusika hivyo idara yote inaonekana haifai.
Tu-deal na vyanzo vya matatizo na si kila siki ku-deal na matokeo vinginevyo tunajidanganya na tuhuma hizi hazitakaa ziishe kamwe.