Kikosi cha pili S2 (mbinu za komando Zedi Wimba)

Zedi hakutaka kuendelea kukaa pale,alihitaji kuendelea na safari yake katikakati ya usiku mkubwa ndani ya pori la kamori, na safari hii alidhamiria kurudi tena Gatumba nchini Burundi.

Wakati ananyayua miguu yake, masikio yake yalisikia mlio wa chuma nyuma yake.

Hakuwa mgeni na aina ile ya mlio, alijua hiyo ni bunduki inakokiwa na kwa aina ya mlio, basi itakuwa ni Uzi12. Silaha ya kichina yenye uwezo sawa ile bunduki ya kirusi aina ya AK47.

Zedi Wimba alisimama na kuweka mikono juu,bila kuambiwa.

******

Dar es laam……

Ilikuwa ni ahsubuhi na mapema, simu yake ilikuwa inaita kwa fujo na hiyo ilikuwa ni mara ya pili mfululizo.

Mwanamke mzuri mwenye sura ya kinyarwanda, mrefu wa asili na weusi wa kuvutia. Mwanamke yule aligeuka upande wake wa kulia na kumtizama mwanaume wa kizanzibari, mwanaume mrefu na mwembamba, mwanaume aliejazia kimazoezi na kuufanya wembamba wake uonekane wa kuvutia zaidi.
Mwanamke aliona bado mwanaume wake amelala fofofo licha ya simu yake kuita kwa fujo kubwa.

Kivivu bila kuleta bugudha kwa mumewe,alinyanyuka akiwa u uchi kama alivyozaliwa. Alimvuka mumewe na kushuka chini, kisha alinyoosha mkono wake na kuishika simu iliokuwa pembeni kidogo ya mto wa mumewe.

Simu ile iliokuwa imekatika, ilianza kuita kwa mara ya tatu sasa.

Mwanamke aliichukua kwa lengo la kumsikiliza mpigaji, lakini alisita na kugeuka kumtazama mumewe ambae alikuwa bado amelala.
Mpigaji alimjua, na haikuwa busara yeye kupokea simu ile, wala hajawahi kuthubutu kuipokea, licha ya simu nyingi kuzipokea pale mumewe anapokuwa mbali na simu yake.

Macho ya mwanamke yule yalikimbilia ukutani, hapo alikutana na mshale wa saa uliokuwa unasoma saa kumi na mbili na dakika saba ahsubuhi.

Mmmmh!! Mwanamke aliguna.

Mkono wake laini ulikimbilia mgongo wa shingo ya mumewe, kisha aliupitisha taratibu sana kwa lengo la kumwamsha ahsubuhi ile bila papara.

Lengo lake lilifanikiwa, kwani, mwanaume alifumbua macho na kujigeuza mwili mzima na hapo alikutana na tabasamu pambe la mkewe, huku mwili ukiwa wazi bila nguo.

Mwanaume alimeza funda kubwa la mate, lakini lengo lake lilikatishwa na mkono wa kushoto wa mkewe ulipopunga hewani simu iliokuwa ikiita kwa fujo.

Macho ya mwanaume yalikimbilia kuona mpigaji..

Chief!!

Jina lilisomeka hivyo.

Kama aliefumaniwa, mwanaume alitupa shuka mbali na yeye, kisha aliinyakua simu ya mkewe kama mwewe alie na njaa ya siku kadhaa.

“Mara ya nne sasa na hupokei simu bwana mdogo!” Ilikunguruma sauti upande wa pili.

“Sio kosa langu Chief, ni ndoa!” Alijibu mwanaume.

Ulipita ukimya.!

“Kwa hiyo upo tayari kufa ukiwa ndoani?” Alihoji mtu upande wa pili.

Mwanaume alikaa kimya.
“Hayo tutazungumza siku nyingine, kwa sasa kuna tatizo kidogo.” Alisema Chief.

“Usitake kunambia ndo unakata likizo yangu!” Aliongea kwa hamaki kidogo mwanaume yule, huku akimtupia mkewe jicho la pembeni.

“Ikibidi inakuwa hivyo, japo sina hakika…ninakuhitaji sana hapa ofisini.” Alisema Chief huku akikata simu.

“Shiit!! Yani nina siku nne tu, lakini tayari likizo imeisha!” Alisema yule mwanaume huku akitupa simu yake kitandani na kuelekea bafuni.

Mkewe nae alimfuata huko huko akiwa bado u uchi.
“Makame!” Mwanamke aliita.

“Najua ugumu wa kazi yako, kazi ambayo ilifanya hadi leo tuko pamoja, naomba unipe moja tu afu uende,mana simu za huyo mtu huwa zinakuondoa hapa hata mwaka mzima” Alisema mwanamke huku akianza kumshika mumewe maungoni mwake.

“Remi mke wangu, usijali inaweza kuwa sio kama siku zote” Haji Makame, mume wa Remi, alimjibu mkewe huku akimshika chuchu zake na kuanza kuzitekenya kwa hisia.

*****

Saa mbili kasoro, ilimkuta Haji Makame akiingia kwenye viunga vya ofisi za ukusanyaji mapato posta.

Ndani ya ofisi zile, kulikuwa na ofisi nyingine nyeti ambazo hakuna aliejua, zaidi ya mkurug nzi wa mamlaka ya ukusanyaji mapato nchini. Mkurugenzi yule hakuwa na kazi hiyo pekee, bali alikuwa na kazi yake rasmi na ya siri kubwa.

Mkurugenzi aliacha kazi zote za ofisi chini ya kaimu wake, jambo ambalo lilimfaya kaimu mkuregenzi kupeleka majungu kwa Rais na mawaziri juu ya uvivu wa mkurugenzi wake. Lakini hakuwahi kuona mkurugenzi wake akiwajibishwa na badala yake kaimu aliishia kumpongeza sangoma wa mkurugenzi wake kwa kumpa dawa ya kulevya wakubwa wake kiasi wasione uvivu wa mkurugenzi wa taasisi ile kubwa.

Kaimu mkurugenzi, alifanya kazi kwa bidii kubwa kwa kuamini ipo siku atapandishwa cheo zaidi na kuwa mkurugenzi kamili, lakini hakujua ile ni mipango maalumu kwa kazi maalumu ya mkurugenzi wake.

Mkurugenzi huyu alikuwa ni bwana Zenge wa Zenge, ambae alikuwa ni mstaafu wa jeshi la polisi na alipotangaza kustaafu kabla ya umri, Rais aliamua kumteua kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya ukusanyaji mapato nchini, huku akiendelea kukiongoza kikosi cha siri cha usalama wa taifa kisichofungamana na idara husika ya usalama wa taifa. Kikosi hiki kilifanya kazi chini rais na kiliwajibika kwake tu.
---

Haji Makame, aliingia kwenye ofisi ya mkurugenzi akiwa kama mteja na hata wafanyakazi wengi walijua ni mfanyabiashara mkubwa nchini na wengine walidiriki kusema anasimamia biashara za bosi wao ambazo hataki viongozi wengine wajue.

Lakini hakuna aliewahi kujua siri ya watu wale wawili.

Haji Makame alifika ofisini na kukutana na sura yenye tafsiri nyingi kutoka kwa bosi wake.

Hakutaka kusubiri ukaribisho, alisogeza kiti kilichokuwa pembeni yake na kukaa, kisha alitulia kimya akingoja alichoitiwa ahsubuhi ile ambacho aliamini si kitu kizuri.

“Pole kwa kukuharibia zoezi la ahsubuhi” Zenge wa Zenge alimwambia Haji Makame.

“Usijali, hiki ni kiapo changu natumikia!”

“Sawa!! Ila mkeo sijamuona siku nyingi, nadhani ameanza na kunisahau sasa!”

“Hawezi kukusahau baba yake wa hiyari Baba uliemkutanisha na mumewe!”

Ulipita ukimya wa sekunde kadhaa.

“Haji!” Mkurugenzi Zenge wa Zenge aliita.

Haji aliinua uso na kumtazama.

“Wakati wewe unaenda likizo, wenzio tuliendelea na majukumu. Honda alienda Sudan, Obimbo Mtei alienda Somalia na hapa nilibaki na Mina pamoja na Zedi Wimba.” Chief alisema na kunyamaza, kisha aliendelea.

“Kifo cha kanali Mrisho Twetwe wiki tatu nyuma kilikuwa na sura ya kawaida kwa walio wengi, ukizingatia alipata ajali tu.” Chief alinyamaza kidogo kisha aliendelea..

“Lakini vijana wa rais waliosambaa nchi nzima, walileta ripoti ambayo ilimstua kila mmoja alieipata. Ripoti ile inasema; Kanali Mrisho Twetwe, alikutwa na matundu mawili ya risasi kifuani mwake. Lilikuwa ni jambo la kushitusha sana, kiasi mwili wake ilibidi ufanyiwe vipimo upya na hapo ilibainika alikufa saa nne nyuma kabla ya muda wa ajali kutokea.” Chief alinyamaza.

“Kwa hiyo ilikuwa ni hujuma?” Haji aliuliza.

“Sikutegemea swali kama hilo kutoka kwako, lakini jibu lake ni ndio,alihujumiwa” Chief alijibu.

Kisha aliendelea…!!

“Badae ilikuja kugundulika silaha iliotumika kuchukua uhai wake, ilikuwa inamilikiwa na Meja Masubo, mkuu wa shule ya sekondari Ugiri inayomilikiwa na jeshi la wananchi mjini Kigoma.”

“Mbona ni ajabu hii sasa, mtu yupo Kigoma atawezeje kuua mtu Dar es laam?” Haji aliuliza huku akikaa vyema kwenye kiti.

“Jambo lile halikuachwa, Meja Masubo alipofuatiliwa, alionekana kuwa Dar siku ya tukio, na walipoenda nyumbani kwake, walikutana na maiti ikiwa imeanza kuharibika na bila shaka alitamatisha uhai wake mwenyewe. Kisa cha kuyafanya yote hayo, hakuna aliejua, lakini wakati vijana wanapekua huku na huko, walibahatika kukutana na mawasiliano, baina ya Meja Masubo na mtu fulani alieitwa Mswahili. Mswahili inaonekana alikuwa Tanzania siku ya kifo cha Kanali Mrisho Twetwe, na katika maongezi yao, walimtaja mtu mmoja ambae tulishamsahau kitambo sana.” Chief alinyamaza. Haji Makame alikaa vyema kwenye kiti.

“Walimzungumzia sana Luteni Kanali Saliza Biseko. Mswahili alimwambia Meja Masubo namna anavyopata tabu kumtapisha Luteni kanali Saliza Biseko. Lakini kikubwa alitaja sehemu aliofidhiwa, ambayo ni huko Gatumba nchini Burundi.” Chief alikamilisha maelezo yake.

“Kwa hiyo hapa ni mchezo mpya umeanza?” Haji alihoji.

“Kwa maelezo, inaonekana sio mchezo mpyau, bali ni mwendelezo wa jambo fulani la hatari, na safari hii,naona mchezo umeshakolea.” Chief aliongea.

“Sasa chief, unahisi kwa nini Kanali Mrisho aliuwawa na Luteni kanali Masubo na kisha nae aliuwawa”

“Nadhani ni mchezo wa kupunguzana kwenye mnyororo”

“Inafikirisha sana kamanda”

“Inafikirusha sana, kiasi mbio za vijana wa rais ziliishia kwa watu hao wawili tu, huku wakibaki na jina mswahili, ambalo halijasajiliwa popote katika Dunia hii”

“ Kwa hiyo hakuna tena taarifa zaidi kuhusu watu hao na mipango yao?”

“Hakuna. Ndio mana taarifa zilifika kwenye dawati letu na tulipozichambua, tuliona tuna kazi moja ili kuupata mwanga wa jambo hili” Chief alinyamaza kidogo kisha aliendelea..

“ ….Luteni kanali Saliza Biseko na Meja jenerali Butiku, walikuwa ni miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu waliokuwa wanahudumu kwenye vikosi vya kulinda amani nchini Congo. Ambapo badae Meja jenerali Butiku, alistafu akiwa huko huko na rais alimteua kuwa balozi wa Tanzania nchini Congo. Kabla ya kuapishwa kwake na kuanza kazi, ndipo kambi ya walinda amani kutoka Tanzania ilivamiwa na kuuwawa watu kumi, kisha Luteni kanali saliza, ambae alikuwa mkuu wa kambi ile, pamoja na mstaafu meja jenerali Butiku, walipotea. Hakuna aliejua walipo, jitihada zilifanyika kujua walipo, lakini hakuna taarifa zilizowahusu na huu mwaka wa sita sasa.. Kwa hiyo kusikia jina la Luteni kanali Saliza Biseko linatajwa,ina maana alikuwa yu mzima. Hivyo haraka ilibidi watumwe mashushu wetu walioko Burundi,kufuatilia pahali alipo na jana jioni, taarifa ilinifikia na sikuona sababu ya kukawia, niliwatuma Zedi na kundi lake la makomando kwenda kumuokoa kisha tutajua kuanzia hapo ni nini kilikusudiwa na watu hawa” Kamishina mstaafu na mkurugenzi wa mamlaka ya ukusanyaji mapato, ambae pia, alikuwa ni mkuu wa kitengo cha siri cha usalama wa taifa na mipango endelevu ya ukombozi, alimazia ufafanuzi wake na kukaa kimya huku akimtizama Haji Makame ambae alikuwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa sana.
Haji aliegemea kiti chake, kisha alishusha pumzi nyingi kwa mkupuo.

“Kwa hiyo Zedi karejea?” Hatimae Haji aliuliza.

“Hajarejea na kundi lake pia halijarejea, lakini taarifa zimeshafika hapa na inasemekana walifanikiwa kumuokoa, lakini walikamatwa tena. Lakini Zedi hakuwa miongoni mwao na hajulikani alipo hadi sasa.” Chief alijibu..

“kwa hiyo tunafanyaje.” Haji alihoji.

“Kukosekana kwa Zedi kwenye idadi ya makomando waliotekwa, inanipa tumaini kuwa yupo salama na huko namwachia, hadi nitakapopata taarifa tofauti kuhusu yeye. Lakini wewe hapa nimekuita kwa sababu moja kubwa” Chief alinyamaza na kuifumbata mikono yake pamoja, kisha alisema..

“Mchezo huu unahusu watu kadhaa hapa nchini, na leo ahsubuhi nimepokea taarifa za kifo cha mkuu wa chuo cha mafunzo na utendaji kivita, Meja Jenerali Maka Magwata. Nilipopokea taarifa hizo, niliomba mwili wake uondolewe na nyumba isifanyiwe ukaguzi wa aina yoyote ile, hivyo nahitaji uende kwake Tegeta, uone yalioko huko, kisha utarejea na jibu litakaloamua wapi ufanyie kazi; kama ni hapa nchini, au usafiri Burundi kumtafiuta Zedi” Chief alitoa maagizo hayo kwa Komando na jasusi, Haji Makame.

“Sawa kamanda, naomba niondoke sasa!” Haji aliaga na kuondoka ndani ya ofisi zile za makao makuu ya mamlaka ya ukusanyaji mapato nchini.
 
Kudo shushaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom