Kuibuka kwa Vikombe vipya kila uchao wa kulaumiwa ni SERIKALI. Kwa nini nasema hivyo??? Ni kwa sababu kama Serikali wangelikuwa makini toka siku ya awali Babu alipotangaza kuwa anaweza kutibu magonjwa sugu, serikali ilitakiwa kumpa masharti yafuatayo ili iweze kumruhusu atoe tiba. Masharti yenyewe ni kwanza kutojitangaza kuwa anatibu magonjwa sugu. Pili serikali ingechukua samples ya wagonjwa wote wanaojulikana mfano HIV wagonjwa 5, TB 5, BP 5, Kisukari 5 na kuwapeleka kwa babu kupatiwa kikombe, na kuwarudisha wodini au makwao na kuwafuatilia angalau kwa mwezi mmoja ili kuona maendeleo yao. Kama itaonekana hali zao zinachange to better, basi wangemruhusu babu na vinginevyo wangemfungia. Lakini hilo halikufanyika, matokeo kila uchao wanaibuka wengine. Mfano yule kijana wa Mbeya yeye anasema kabisa kuwa anasaidiwa na wasaidizi wake kichwani (a.ka mashetani) sasa kumwamini mtu kama huyu kwa kweli inatia wasiwasi saana na upeo wa viongozi wetu. Yule mama wa Tabora naye ukimwangalia anavyoombea watu kabla ya kuwapa dawa anachezesha mimacho kama mwenye kifafa, Nashangaa kwa mkuu wa mkoa kama Abeid Mwinyimsa kweli kupewa kikombe na yule mama na akanywa!!! Inatia hofu na sijui Taifa limefikia wapi???