Nabii Joshua Mwantyala akiwanyunyuzia maji ya tiba wananchi waliokusanyika katika mkutano wake wa Neno la Mungu la uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wenye magonjwa sugu kama vile Ukimwi, Kansa na mengineyo. Nabii Joshua juzi alianzisha huduma ya tiba yake inayojulikana kama majibu ya tiba ya maajabu ya Loliondo ambapo yeye hutoa matone ya maji ya uponyaji.ambayo huwanyunyuzia wagonjwa vinywani(Picha: Regnald Miruko)
Hivi kweli kwa taifa lenye viongozi wenye mawazo kama yale yaliyojidhihirisha jana, kwa kuleta watoto wasiojua lolote ili kuziba nafasi, ili wenye uwezo wa kupambanua wasipate nafasi katika mjadala wa jambo muhimu kama katiba ya nchi, litakuwa na jamii ya aina gani?
Yule mtu tambwe hiza wala hajionei aibu kueneza propaganda za kujipendekeza katika masuala muhimu yenye kubeba mustakabali wa taifa kwa vizazi na vizazi, na anatoka hadharani na kusema mimi kwa kuzuiwa kusema usiku nimepigiwa simu zaidi ya mia saba za kunifariji.
Jamani tunaelekea wapi? Kama hiyo ndio aina ya viongozi unatarajia wale wanaoongozwa waweje?
Waache raiya wajimwage na vikombe na hata kama ikibidi mwenye uwezo anywe ndoo nzima.
.
sio wote, sema waliopiga kikombe!Aisee we Mkale! Haya ni kweli kabisa.TZ ni kweli ni majuha.
watu wamekata tamaa jamaa wanarudisha imani ya maisha kwa watu. Tunajiona wafu tu, poa sana ufunuo wa babu, mbeya, tabora. Waje wengine mia mbili. Idara ya afya imeoza. Dawa hamna mpaka utoe kitu kidogo, kikwete na mafisadi wanatafuna nchi yetu, kidogo vikombe vinatupa imani kwamba tutaishi kwa matumaini huku mungu akitulinda. Bravo. Majani+mizizi+maji+maombi= uponyajiWatakuja wengi kwa jina langu
Jf hamuachi vituko. Hii ipeleke jukwaa lake mkuu itanoga sanambona naona nabii ana koti kama la Chadema?