Usitumie neno hili "MAJUHA", hayajakukuta na mshukuru Mungu kwa hilo. Kwa kweli kumekuwa na tabia ya kuwabeza watu wanaotafuta suluhu za maradhi waliyonayo. Katika nchi kama yetu ambapo Serikali imeshindwa kuwa na huduma za afya za kueleweka, unategemea nini? Tunaishi kwa kuamini zaidi juu ya uweza wa Mungu, hata serikali inapokumbana na tatizo la umeme huwa wanasubiri uwezo wa Mungu katika kuleta mvua. Takriban watanzania wengi wana matatizo ya afya ambapo wamekosa tumaini, na hii inadhihirika pale ambapo linajitokza tumaini jipya. Wako watu wana uwezo wa fedha lakini wanakosa suluhu ya afya zao kwa magonjwa yanayowasumbua, unategemea watafanya nini?
Jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwa wewe ambaye afya yako inaendelea vyema na bado hujapata maradhi ambayo wanasayansi wameshindwa kutoa suluhu yake. Lakini kumbuka yanaweza kukupata hata wewe, hujatenda mema sana kwa Mungu.
Tutumie kauli njema katika kuwaelimisha wale ambao tunafikiri wanapotea na huku tukiwapatia tiba mbadala.