Kiki bila kazi nzuri ni anguko la Msanii

Kiki bila kazi nzuri ni anguko la Msanii

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
20,849
Reaction score
43,025
KIKI BILA KAZI NZURI NI ANGUKO LA MSANII

Tarehe 27 December 1999, rapa Sean "Puffy" Combs maarufu pia kama P. Diddy alikamatwa kwa tuhuma za kupiga risasi ndani ya NightClub. Pamoja nae walikamatwa aliyekuwa mpenzi wake komredi Jeniffer Lopez na rapa aliyejulikana kwa jina moja kama Shyne. Polisi walimwachia dada Jeniffer kisha kuwafikisha Diddy na Shyne mahakamani. Shyne alihukumiwa miaka 8 jela huku Diddy akiachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia. Wengi husema Diddy alimhonga mwenzie ili abebe mzigo wake naye kuwa huru. Lakini baadae sana ilikuja kujulikana kwamba Diddy alipiga risasi hewani ikiwa kupata KIKI kwa ajili ya album yake iitwayo Forever aliyokuwa ameiachia August mwaka huohuo 1999. Hiyo album ilikuwa na mafanikio makubwa.

Nimeanza na story fupi ya Diddy ili kupata msingi wa kuelezea ninachotaka kueleza hapa yaani KIKI. Hili suala limekuwa likifanyika sana ili kupata attention ya watu na kuongeza mauzo ya kazi za msanii. Diddy sio wa kwanza kufanya hivyo. Karibu kila msanii hufanya jambo la kuvuta hisia za watu anapotaka jambo lake lifanikiwe. Kwa mfano mwaka 2009 zilienea sana tetesi kwamba Fally Ipupa anatoka kimapenzi na Komredi Olivia wa USA... tetesi zilikolezwa na picha mbalimbali zikiwaonyesha kama wapenzi. Kumbe na yenyewe ilikuwa ni KIKI kwa wimbo wao wa Chaise Electrique uliopo kwenye album ya Fally. Hata Koffi Olomide miaka ile Jeniffer Lopez anavuma aliwahi kutamka kwamba atafanya nae Collabo. Lakini ilikuwa ni KIKI.

Tofauti ya KIKI za kina fally Ipupa, Koffi Olomide na Diddy na hizi za hapa kwetu ni moja tu. Wao wanafanya KIKI huku wakiwa wametoa kazi nzuri zinazovutia wateja kununua. Kwa mfano pamoja na KIKI ya Fally na Olivia bado wimbo ulikuwa mzuri kuanzia audio hadi video. Hapa kwetu KIKI inakuwa nzuri kuliko wimbo unaoachiwa. Yaani msanii anawekeza akili yake kwenye KIKI kuliko kazi nzuri. KIKI bila kazi nzuri ni kuchafua brand. Hii itasababisha wananchi wakupuuze na kupoteza imani.

Pia KIKI zinazotengenezwa ni ushuzi mtupu. Utakuta msanii anatangaza hadi kafa kumbe ni uongo. Yaani wanafanya matukio mengi ya kudhalilisha utu wakidhani ni KIKI. Kazi ikiwa nzuri hakuna haja ya KIKI. Itajiuza kwa kupitia njia za kawaida za marketing.

Nawasihi wasanii wajikite kutoa kazi nzuri huku akiwa na timu nzuri kuanzia management, marketing & sales na wengine wote muhimu.
 
Miaka ya nyuma kuna msanii mmoja "handsome" wa kariakoo gerezani alijizushia KIKI ya kuliwa TIGO na akatrend kweli
 
Hakika ni kweli kabisa, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom