Kijue kijiji cha ajabu nchini India

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
2,351
2,000
Kinaitwa Kuldhara, kwasasa ni kijiji kilichotelekezwa, hakikaliwi na watu, kipo umabali wa kilomita 21 kutoka mjini Jaisalmer magharibi mwa India, kijiji hiki kilianzishwa tangu miaka ya 1200 lakini baadae miaka ya 1800 kiliachwa na kikimbiwa na watu wote kwasababu za kushangaza.

Kuna sabaabu nyingi sana zinatajwa kujibu swali la kwanini wanakijiji wote walikimbia, moja ya sababu hizo ni kwamba katiki kijiji hiki kilikumbwa na mafuriko, sababu nyingine wanasema kulitokea tetemeko la ardhi lakini ipo sababu inayoaminika kuwa ndio halisi, lakini hufichwa isizungumzwe.

Ukweli ni kwamba sababu ya watu kukikimbia kijiji hiki ni kwamba katika miaka ya 1800 kijiji kikiwa na wakazi kati ya 3000-4000 ghafla usiku mmoja kikatoweka, yaani kijiji kilipotea ndani ya usiku, baadae ilipofika asubuhi kikarudi. Hii sio tuu wanakijiji kupotea, bali kijiji chote na watu wake hakikuwepo kwa usiku huo.

Baada ya kurudi kila mmoja akawa anasema lake ni wapi alikokuwa na aliona nini, baada ya tukio hilo vilianza kutokea vizuka usiku, mara sauti za ajabu, hapo ndipo wanakijiji wote wakaamua kuhama na mpaka leo yamebaki magofu tuu ya nyumba zao walizokuwa wakiishi miaka hiyo.

Historia nyingine imeandika kuwa katika miaka huyo kulikuwa na kiongozi katili aliyeitwa Salim Singht aliyekuwa analazimisha kumuoa binti mdogo wa mmoja wa wazee wa kijiji hicho, alikuwa anatoza ushuru mkubwa kila wanapokataa amuoe binti huyo, ndipo wazee wa kijiji walipokaa kikao, usiku mmoja kiongozi huyo anakuja anaona kijiji hakipo !.

Hii ni story ya kuaminika juu ya ni kwanini kijiji hiki kilipotea kwa usiku mmoja na kurudi, baadae watu wote wakahama.

FB_IMG_1627418266366.jpg
 

souljar

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
763
1,000
Acha na India, hapo Kenya kuna kijiji maji yanapanda mlima.. WONDERS SHALL NEVER END UNDER THE SUN.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom