Kijiji cha mfano

Kijiji cha mfano

Mimi nimeshawahi kufikiria the same but kwa level ya Kata kama ifuatavyo ili kweli tuweze kuwaendeleza wananchi wetu : Kuwe na kata ya mfano na hii kata iwe na vijiji 4 tuu. Makao makuu ya hii kata pajengwe ofisi kubwa ya kata yenye vitu vifuatavyo : ofisi ya WEO, huyu WEO lazima awe na digrii au masters... Ofisi ya afisa kilimo wa kata, awe graduate pia, ofisi ya afisa mifugo - graduate, ofisi ya afisa maendeleo jamii wa kata, afisa ushirika, afisa Misitu, afisa biashara, afisa mazingira, afisa Wanyamapori, afisa elimu wa kata, mshauri wa mgambo wa kata n.k kila mmoja awe na ofisi yake. WEO awe na gari yake Toyota land cruiser hardtop, na maafisa wengine wote wawe na gari aina ya Toyota hilux double cabin. Jirani na ofisi ya kata kuwe na kituo cha polisi cha kata chenye kila kitu, magari, pikipiki, computer, umeme /solar, kuwe na hospital ya kata yenye hadhi zaidi ya kituo cha afya na iwe inatoa huduma zote za muhimu. Pia hapo jirani pawe na Sekondari kubwa ya Bweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka kwenye shule za msingi za kila kijiji. Kuwe na mahakama ya kata iliyokamilika na kuwe na gereza dogo. Sasa ukitoka kwenye kata kwenye kila kijiji kuwe na mtaalamu wa kila fani muhimu anayekaa huko huko kijijini. Kila kijiji kuwe na majengo ya ofisi za kijiji zenye chumba cha mwekiti, VEO, ukumbi wa mikutano, mahabusu ndogo, na kila mtaalamu awe na ofisi yake pale kwenye majengo ya ofisi za kijiji. Kila kijiji VEO na kila mtaalamu wawe na nyumba yake nzuri, yenye umeme /solar, maji nk. Kila mtaalamu, VEO na mwenyekiti wa kijiji wapewe usafiri rahisi wa gari mfano vile vigari vi Suzuki na kila mwezi wapate mafuta kupitia akaunti zao za mishahara. Kila kijiji kuwe na polisi post yenye gari 2 na pikipiki. Vijiji vyote 4 vipimwe na kufanyiwa land use plan, udongo wote upimwe na aina ya mazao ya kupandwa kila msimu yajulikane. Mifugo yote ijulikane na idadi ya juu ya mifugo inayotakiwa kufugwa ijulikane na sheria ndogo zitungwe. Idadi ya wanakijiji ijulikane na sheria kali iwekwe kwa wahamiaji kutoka nje ya kijiji. Kila kijiji kiwe na shule 2 za msingi na moja ya sekondari ya day. Kila mwanakijiji awe na shamba lililopimwa kusilopungua ekari 5 na awe anazilima. Kila kijiji kuwe na gulio/soko, zahanati, godawn la kuhifadhia mazao kila kitongoji, sehemu maalumu za kuchungia mifugo, kuoshea mifugo, viwanja vya michezo, barabara za mitaa au vitongoji, maji ya bomba au visima. Kabla ya msimu wa kilimo kuanza wataalamu wapite vijiji vyote na kupanga mikakati ya kilimo, mbegu na pembejeo zinazohitajika na jinsi ya kuzipata (kwa mkopo kutoka makampuni mbalimbali yaliyosajiliwa kuleta pembejeo na kununua mazao etc). Kila mtaalamu kwenye kijiji chake ahakikishe mashamba yote maandalizi yameanza kwa wakati... Nitaendelea next time, yaani hii kata ya mfano inatakiwa iwe ndiyo engine ya maendeleo
..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni nzuri ila yakwako ni pana mno. Tunaanzia kwenye nuclear level. Kijiji ambacho wote mnafahamiana na ni bei rahisi. Tukitoka hapo tukaweza tutaenda kwenye kata.
Unajua mkuu huku kwetu hatuna tena ile wanaita suburban. Yaani kila mahali ni uswazi tu sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu kuwaza tu. Mfano akatokea kiongozi mmoja mwenye akili kama mimi akaanzisha Kijiji cha mfano labda Kisarawe huko.
Kiwe na shule ya msingi na sekondari. Kiwe na soko na maduka ya bidhaa muhimu,kiwe na msikiti na kanisa . Mwisho kiwe na ukumbi wa mikutano.
Kila mkazi awe na 50 square meter, kiwe na drainage system inayounganisha nyumba zote na pia huduma ya umeme.
Kiwe na mitaa iliyopangilwa na miti kando ya barabara,wakazi wake wawe ni familia 100 tu. Na usafiri wake ndani ya Kijiji iwe baosikeli tu. Kutokea stand kuu.
Mambo mengine yote yafanyike nje ya Kijiji hicho,mazingira yake yatavutia au hapana.




Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa bahati mbaya viongozi wetu waliozaliwa chini ya miti na kwenye nyumba za nyasi huko porini hawafikiri hivyo.

Hatujaweza kupanga miji yetu tangu Mjerumani na Mwingereza ndio utajua ilivyo vigumu kupanga vijijini.
 
Yale yale ya Marehemu J.K. Nyerere, si milijifanya kumpinga kiko wapi sasa?? vijiji vingi aliviacha vikiwa vya mfano km kijiji cha ujamaa Moghabiri,

Kongore,

Mwenge ujamaa village kilimiki na Bendi kabisaa ajili ya burudani!

Geza ulole.

Kibugumo ujamaa village,

Ng'aramu,

Kenyamanyori,

Kiribho lift valley

Mugango kwibara,

Mpaka leo vyang'ara si kawaida, kuna Matrekta, Mashamba, maduka, Combined harvest ya kijiji, kwa wananchi wakodi kwa bei nafuu, likiondoka tu kijijini kwenda kufanya kazi mbali bei inapanda.

unasema maisha ambayo wenzako tunayaishi. hata hapo Moshi, Machame, Arusha nk nenda uone mipangilio ya maisha yao! utachoka, hujiulizi kwa nini Wachaga wanapenda kwao kuliko wamakonde na wamatumbi? hata Wafanya kazi wa idara zote za umma uchagani siyo tatizo wakienda tu hawatoki tena. wako tayari kuacha kazi wabaki hukohuko. hujatembea ukajionea!

Mleta mada Kama umezaliwa miaka ya 2000 kuendelea ntakusamehe bure, chini ya hapo wewe ni ulikwaa Division zero! km ulienda shule! hata kibanga ampiga Mkoloni hujui?
 
Back
Top Bottom