KIJANA WA UMRI WA MIAKA 20+ AFANYE NINI KUJIHIMU NA MASUALA YA KIUCHUMI NA KIUWEKEZAJI?

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
581
KIJANA WA UMRI WA MIAKA 20+ AFANYE NINI KUJIHIMU NA MASUALA YA KIUCHUMI NA KIUWEKEZAJI?



Mwaka ndiyo upo ukingoni , wengi wetu wakati huu pia tumeongeza umri kwenye namba za miaka yetu na wengi ndiyo wamekuwa vijana kwa sasa na kwa lugha nyingine maisha ndiyo wakati wa kuyakabili kwa uaminifu na kwa kujituma kuchukua usukani wa maisha yako.

Leo nakuletea maeneo muhimu sana ambayo ukiyafanyia kazi utajiletea mafanikio na utakuwa kwenye wakati mzuri wa kutimiza malengo yako. Kwa pamoja ungana name kuyaona maeneo hayo muhimu sana na uyachukue kwenda mwaka mpya wa 2019 na ukafanikiwe.



  1. weka mpango kuhusu uwekezaji maana uwekezaji si zawadi ama bidhaa.
Kwenye umri wa miaka 20+ ndiyo wakati mzuri kwako kama kijana kujituma na kufanya uwekezaji wa aina yoyote maana umri unaruhusu na unao uwezo wa kufanikisha uwekezaji wako huo utakaotaka kuwekeza.



Moja ya jambo muhimu kuhusu uwekezaji ni kuwa na mpango wa kuwekeza kwakua kama unavyofahamu kuwa hakuna mpango bila kuwa na lengo na wakati wote malengo hutimizika kutokana na mipango dhabiti , kwahivyo ili nawe ufanikiwe kwenye uwekezaji wako yakupasa uwe na malengo ya uwekezaji ambayo utayawekea malengo na kasha kuwa na mipango ya kuyatimiza na katika kuweka mipango yakupasa uweke mipango katika maeneo matatu muhimu kwenye maisha yako.



i) Mipango ya kuwa salama.

Hii inabeba uwezo wako wa kujilinda na magonjwa , ajali , majanga , na uwezo wa kumudu gharama za matibabu hapo ndiyo utakuwa salama.



ii) Mipango ya kufanikiwa.

Hii inabeba uwezo wako wa kugharamia mahitaji yako muhimu , kama chakula , malazi , na mavazi na kukuza uwezo wa juu kukabiliana na hatari za kiuchumi n.k



iii) Mipango ya kuwa tajiri.

hii inabeba uwezo wako wa kuingia kwenye Nyanja pana za kiuwekezaji na kupata vipato vya kutosha na hapa tunaamaanisha uwekezaji kwenye maeneo muhimu yanayozalisha sana kama , kilimo , ujengaji na ununuzi wa nyumba , ununuaji na uuzaji wa hisa kutoka kwenye makampuni makubwa hapa nchini kwetu.



Baada ya kuweka mipango hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kufanikisha malengo yako mama ya kuwa kijana mwenye ukwasi kwa baadaye , jambo la kukumbuka ni kuwa haya mambo hauyapati kwa siku moja yakupasa kujikaza na kujituma kwa hali na mali kufanikisha na kupata kile unachokitaka.



Maeneo makubwa yatakayokufanikisha kufika kwa haraka hapo ni pamoja na....



  • Kufanya kazi kwa bidiii
  • Kuweka akiba ambayo baadaye itumike kwenye uwekezaji wako.
  • Kutumia kidogo kuliko unachopata.
  • Kuoa /kuolewa vizuri.
  • Kuambatana na watu sahihi watakao kusogeza kwenye mafanikio yako.
Uwe na Mwaka Mpya wenye fanaka na mafanikio mengi kwako.



Ndimi MICHAEL THE GREAT ONE +255 759880010.
 
Back
Top Bottom