Kijana wa kiume mwanafunzi wa shule ya Msingi anaingiliwa kinyume na maumbile !Msaada hatua za kuchukua

Kijana wa kiume mwanafunzi wa shule ya Msingi anaingiliwa kinyume na maumbile !Msaada hatua za kuchukua

The Legacy

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
8,217
Reaction score
16,089
Wadau Habari,

Jana nikiwa nje ya nyumbani nilipigiwa simu na mke wa rafiki yangu.Akanieleza kuwa ameingia kwenye chumba cha mtoto wake wa kiume kufanya usafi amekuta kuna Boxa na kaptura zimechafuka kwa haja kubwa.

Alipo subiri kijana arudi shule akamuuliza taratibu na majibu yalikua ndio kuna mtu anamfanyia kitendo hiko tangu mwezi wa 5 lakini hakumtaja jina.

Huyu mtoti ni wa darasa la mtihani,nawaza namna sahihi ya kushughulikia hiki jambo kwa utulivu ili mambo yasiraribike.

Hatua nilizochukua:
Nilimpigia polisi wa kituo cha karibu akanishauri niongee na mtoto kama hatasema nimpeleke kituoni kwa kibano zaidi amtaje mubusika.

Dawati la jamii wakanishauri niongee na mtoto wa urafiki atataja tu ili tuweze kumsaidia.

Baba wa mtoto hayupo nchini yuko Canada kwa Masomo,

Mimi ni babà wa ubatizo wa huyu kijana na ni rafiki wa hii familia

Nifungueni kichwa kimejam,naomba ushauri.

Ukitukana, litakukuta jambo:

Aione Dkt. Gwajima D
 
Ushauri ni huo mfanye mtoto kuwa rafiki yako halafu muulize kwa upole na upendo atamtaja tu huyo muhusika.

Mara nyingi unaweza kukuta hata kitendo hicho anafanyiwa na mwalimu wake halafu anatishiwa maisha maana matukio kama haya ya walimu kulawiti watoto yamekuwa yakiripotiwa kwa wingi.

Inaumiza sana aise mtoto kufanyiwa ukatili wa namna hiyo.

Ukishindwa kupata jawabu sahihi naomba nishirikishe ili tuone namna nzuri ya kumsaidia mtoto.
 
Mke wa rafiki yako, kakupigia wewe simu, wewe ndio kichwa kinakuuma kushughulikia jambo, rafiki yako yuko wapi? Kwanin hamjamshirikisha nae ndio baba.

Anyways chukua mtoto, mpeleke sehemu anapendelea, muoneshe upendo huku ukimbana maswali ya akili,
Buni vistori vya uwongo, mfano km katishiwa, basi buni vistori kwamba ushawahi msaidia mtu katika hili na lile alitishiwa maisha, ukafanya hivi na vile, ili mtoto aone yupo sehemu salama zaidi.
Buni stori ya uongo kupitia hicho anachopitia yeye, mwambie wakat unasoma kuna mtu alifanyiwa hivi na vile, aliposema ikawa hivi na vile, utamuwin.
ila km mtoto ni mjanja kuliko ww hutaambulia kitu,
Mpeleke polisi akabanwe
 
Muda wote mzazi uso umeukunja, kufokea watoto hovyo hata mtoto anapopata changamoto anashindwa kusema.
Umesema kweli kabisa mkuu. Wazazi yatupasa tuwe na urafiki na watoto ili kusikiliza changamoto zao.

Utakuta limzazi linaunga mkono adhabu kali kwa mtoto awapo shuleni kinyume kabisa na sheria halafu kweli utegemee mzazi kama huyo awe na urafiki na mwanaye?
 
Darasa la mtihani ndio Darasa gani? hii ingetupa picha ya umri wake, Kwanini mke wa rafiko ako akupigie simu wewe? habari nyingi sana zinazokuwa na mhusika katika nafsi ya tatu huwa ni Chai, Huyo mtoto kama kaamua kusema kwanini aseme nusu nusu? Hoja yangu ni inaweza kuwa michezo ya watoto watupu, au mtoto asiwe Victim kwa maana kwamba wanafanyana kwa zamu. Unataka ushauri gani zaidi? umeeshaambiwa kaa nae chini zungumza nae kwa upole, nilifikiri baada kukaa nae chini na kugonga mwamba ndio ungekuja huku JF kuomba ushauri?
 
Wadau Habari,
Jana nikiwa nje ya nyumbani nilipigiwa simu na mke wa rafiki yangu.Akanieleza kuwa ameingia kwenye chumba cha mtoto wake wa kiume kufanya usafi amekuta kuna Boxa na kaptura zimechafuka kwa haja kubwa.

Alipo subiri kijana arudi shule akamuuliza taratibu na majibu yalikua ndio kuna mtu anamfanyia kitendo hiko tangu mwezi wa 5 lakini hakumtaja jina.

Huyu mtoti ni wa darasa la mtihani,nawaza namna sahihi ya kushughulikia hiki jambo kwa utulivu ili mambo yasiraribike.

Hatua nilizochukua:
Nilimpigia polisi wa kituo cha karibu akanishauri niongee na mtoto kama hatasema nimpeleke kituoni kwa kibano zaidi amtaje mubusika.

Dawati la jamii wakanishauri niongee na mtoto wa urafiki atataja tu ili tuweze kumsaidia.

Nifungueni kichwa kimejam,naomba ushauri.

Ukitukana, litakukuta jambo:
Pole sana, kuwa na subira na kuongea na mtoto taratibu atasema. ikibidi muweke mtego mumkamate huyo mshenzi. Nashauri sana uwashirikishe dawati la jinsia kikubwa mtoto ajione yuko safe kuongea hilo.
 
Back
Top Bottom