Kijana mwenye jinsia mbili

Kijana mwenye jinsia mbili

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,494
Kwanza mshukuru Mungu kwa kuwa mzima bila kasoro yoyote kama ulivyo, sasa twende kwenye mada.

Kuna kijana mmoja tulikutana kwenye group moja la Dini, baada ya mimi kushusha nondo flani na makala zilizoshiba kuhusu imani na changamoto tulizonazo.

Kijana akaja inbox na ikawa mazoea kunitafuta na kuomba ushauri tu wa kiimani, ila baadae alinifungukia "Kaka maisha yangu siyaelewi nahisi nilizaliwa huku Duniani bahati mbaya. Kaka mimi sio mwanaume kama ninavyojiweka wala sio mwanamke". Nilishtuka sana kisha nikamuuliza kwanini unasema hivyo?

"Kaka mimi nina uume kama mwanaume na uke kama mwanamke na hii siri anayo baba na mama tu. Napata shida sana kujua mimi ni nani, na Dunia itanitambuaje. Natamani sana nife mapema nichoka upweke nilionao. Nimechoka sana kaka na ."

Nilimpa pole na kuanza kumuuliza maswali kadhaa kuhusu mwili wake, anapata hedhi kama mwanamke, uume haupo imara sana, anajihisi zaidi mwanamke ila tayari wazazi walimtambulishaga kama mwanaume.

Anatamani zaidi wanaume kimapenzi kuliko wanawake, hivyo anashindwa kujielewa ni upande upi sahihi?

Akaniuliza tena, "Je, nikienda kwa mwanaume sitaitwa shoga na kudharauliwa na kuwa mlaaniwa mbele za Mungu na hata wanadamu. Je sitatengwa? Na je, nikaamua kuwa na mwanamke kwanza ni mwanamke gani atanikubali? Je, sitaitwa msagaji na kuwa mlaaniwa mbele za Mungu na mbele za wanadamu?"

"Kaka nachukia sana maisha yangu, nachukia sana kuzaliwa kwangu Duniani, nimevumilia sana. Nina miaka 25 sasa siijui hatima, naona wivu sana wengine walivyo huru kuoa na kuoana angali mimi hiyo siyo haki yangu wala sifai kuwa miongoni, nishauri nifanyeje?"

Nisaidieni nimshauri nini, alinitumia picha ya jinsia zake pia, nilizifuta baada ya kushindwa kuamini na kuwa mbishi?!
 
Nimewahi ona na kuambiwa kuwa chizi anayefurahisha hatoki kwenye familia yenu.

Huyu kijana anapitia magumu sana, suala la kumsaidia hapo ni kwamba afuatane na hisia kali za mwili wake, kisha ahame mji au eneo ambalo watu wanamjua.

Huko aende akiwa muhusika wa Moja kwa moja na jinsia ambayo humletea hisia.

Akiwa na akiba ya mavazi na mahitaji yote muhimu ya jinsia yake ya pili.
Wazazi wamsaidie ktk hili
 
Nauliza hawezi kufanyiwa sajeri kuondoa moja abaki na moja yenye nguvu?
 
Kipind naanza form one shule niliyokuwa nasoma enzi izo, palikuwa na jamaa ana tatizo ilo sema alikuwa yuko form 2 alinizidi kidato kimoja...Alikuwa anapata manyanyaso alikuwa na jinsia mbili na viungo vyote vya uzazi kama watu wanavyosema.

Finally,alikuwa njema darasani sana ila alikuja kuacha shule sijajua aliendea wapi? ila form three hakwenda ..Kuna kipind mother wake alikuwa anakuja shule kushtaki jinsi mwanae anavyozodolewa na wenzie mpaka kweny school baraza tukiwa tunataka kufunga shule ishu iliongelewa.

Nimekumbuka mbali sana .
 
Yaan Tanzania mtu mwenye matatizo ya hormone, hasa me kuwa km ke, atanyanyaswa na kutengwa mwshoe anaangukia ktk Gayism.

Mtu mwenye jinsia 2 ndo kabisaaa, yaan anaonekana km kiumbe wa ajabu, inatakiwa Elimu ya ujinsia itolewe kwa jamii.
 
Aisee. Roho imeniuma gafla.
 
Yaan Tanzania mtu mwenye matatizo ya hormone, hasa me kuwa km ke, atanyanyaswa na kutengwa mwshoe anaangukia ktk Gayism.

Mtu mwenye jinsia 2 ndo kabisaaa, yaan anaonekana km kiumbe wa ajabu, inatakiwa Elimu ya ujinsia itolewe kwa jamii.
Ila kwa kweli mtu anajikuta katika hii dunia anapata mateso makali bila ya kuwa na makosa kwa vile kazaliwa automatically hamna jinsi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom