Kijana muwindaji aliyempenda zimwi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Hi hadithi nilihadithiwa na marehemu bibi yangu RIP bibi.
Katika kijiji kimoja alitokea kijana hodari sana kwa mawindo. Kijana huyu aliweza kuitunza familia yake vizuri hata baada ya baba yake kufariki. Kila akienda porini alirudi na nyama ya kutosha. Dada zake walichimba mizizi na kutafuta mboga na matunda hivyo katika familia yao kila siku walikula chakula chenye tunu . Bibi yake aliyekua kikongwe alionekana kunawiri kutokana na matunzo mazuri ya familia.

Muda ulifika familia ilimshauri muindaji atafute mke. Kijana hakuridhika na msichana hata mmoja pale kijijini. Kila siku ndugu na jamaa walimkumbusha lakini aliwaambia wampe muda. Siku moja akiwa mawindoni katikati ya msitu alikutana na msichana mzuri sana akiwa amekaa chini ya mti. Alimsalimia msichana aliyekataa kujibu. Muindaji aliona kabisa huyu ndiye mke anapaswa kumuoa. Muindaji aliamua kumbeba Yule binti mabegani. Walitembea umbali mrefu, muindaji alichoka. Alitaka kumuweka msichana chini ili anywe maji na kupumzika. Msichana aligoma kushuka.

Wailifika kijijini muindaji akiwa hoi. Ndugu walimshangaa mgeni aliyekuja na kijana wao. Waliksribishwa chakula lakini msichana alikataa kushuka chini. Mwisho watu wote walikwenda kulala. Muindaji alpitiwa na usingizi akiwana mgeni wake shingoni. Kumbe mgeni ni zimwi lilimuua mwindaji na kutokomea. Asubuhi familia ilibaki ba msiba mzito.
 
Stori dhaifu sana unge kaanayo mwenyewe ingependeza .haina funzo lolote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom