Kijana jela maisha kwa kunajisi mtoto

Kijana jela maisha kwa kunajisi mtoto

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Mahakama ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imemhukumu kifungo cha maisha jela, Frank Mlyuka (24) baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti mtoto wa kike wa miaka mitatu.

Mbali na hukumu hiyo, Mlyuka ametakiwa kulipa Sh5milioni kama fidia kwa wazazi wa mtoto huyo.

Akisoma hukumu hiyo juzi Februari 14, 2018 Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Hussein Marengu amesema Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa Mlyuka alitenda makosa hayo na mwenyewe kukiri mbele ya Mahakama.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Nashoni Simon amesema mshtakiwa alitenda makosa hayo Februari 9, 2018 katika Kijiji cha Kihesa Mgagao wilayani Kilolo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashataka huyo, siku hiyo mshtakiwa alipita nyumbani kwa mama mkubwa wa mtoto huyo, Jestina Lubiba na kumkuta mtoto huyo akicheza na wenzake.

Amesema mshtakiwa alimwita mtoto huyo ndani na kumwingiza jikoni ambapo alimbaka na kumlawiti, kumsababishia maumivu makali na kwamba baada ya tukio hilo aliondoka.

Amesema mtoto huyo baada ya kufanyiwa kitendo hicho alitoa taarifa kwa mama yake mkubwa, ambapo msako ulianza na mshtakiwa huyo kukamatwa huku mtoto huyo akipelekwa zahanati ya Pomerini, baadaye kuhamishiwa

Hospitali ya Rufaa Iringa alikolazwa kwa siku moja.

Hakimu Marengu ameeleza kuwa miongoni mwa vielelezo vinavyothibitisha kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo ya kubaka na kulawiti ni hati ya maelezo ya mshtakiwa mbele ya walinzi wa amani na taarifa ya daktari.

Alipotakiwa kujitetea, Myuka anayeishi na wazazi wake amesema ametenda kosa hilo akiwa amelewa na hana cha kujitetea.

Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah amekiri kuongezeka matukio ya ubakaji wilayani humo na kubainisha kuwa wastani wa watoto wanne hubakwa kila mwezi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hiyo milioni 5 asipolipa inakuwaje? Nani atamlipia mtu ana kifungo cha maisha
 
Alitakiwa ahasiwe na kulawitiwa pia ili ajifunze
 
Huyo ana laana ya kudumu. Lakini fidia italipwaje wakati ana kifungo cha maisha? Nakumbuka kuelezwa kuwa faini hizi hulipwa baafa ya mhukumiwa kumalima kifungo chake.

Hata hivyo kwa nini katika ushaidi kusiwe pia na matokeo ya DNA ili kuwa na hakika kikamilifu ya huyo mshenzi?
 
Iwe kifungo cha maisha kweli hakuna msamaha
 
Hiyo mil.5 ni hadithi tu sasa italipwa na nani wakati anafungwa Milele?
 
Watoto wa4 kila mwezi? Mbona magereza yatajaa sasa, tatizo nn? Si muende Sinza tu? Hivi mnafikiri huku dar ingekuwa Sinza haipo hali ingekuaje, si pangekuwa na mass convictions za wabakaji kila siku? Nendeni Sinza, acheni kubaka watoto, shenzi kabisa!
 
Inasikitisha sana. Watoto wanne kila mwezi! Nini tatizo Kilolo Iringa?
 
Alitakiwa ahasiwe na kulawitiwa pia ili ajifunze
Aaah! Hii hapana. Wewe ukipewa jukumu hilo la kutekeleza utalifanya?
Tena mbele ya kadamnasi ili kuhakikisha haki imetendeka.
 
nyege mbaya sana ona anaenda kuwa "chakla" gerezani
 
Wangenipa hyo kazi ya kumuhasi nanyofoa yote. Nakoroga tindikali namwagia hapo paliponyofolewa
 
Binafsi nalihusisha hilo tukio na imani za kishirikina kwa sababu si rahisi mtu mzima kumbaka mtoto wa miaka minne
 
Back
Top Bottom