Kijana chukua hili

Kijana chukua hili

Joined
Nov 2, 2020
Posts
68
Reaction score
90
Kwa kutambua umuhimu wa kundi la Vijana, ambalo ni takriban asilimia 60 ya idadi ya Watanzania wote.

Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kulisaidia kundi hili muhimu.

Kwa sasa tunao wataalam hasa ambao wamejikita katika kulisoma kundi hili kwa undani wake,kufahamu makuzi na hatua linazozipitia katika maisha ya kila siku.

Kijana ana mengi kila uchao, Si nyumbani, mtaani, shuleni na hata maisha yake binafsi.Bahati mbaya wengi wetu tunamlaumu sana kuliko kumsaidia.

Kwa Sasa uwepo wa maafisa maendeleo ya Vijana wenye taaluma stahiki, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kulivusha kundi hili.Hii itafanikiwa Kama jamii itawafahamu na kuwapa kipaumbele. Pamoja na wao kuwa huru kushiriki na jamii juu ya wanachokijua kuhusu Vijana.

Afisa maendeo ya Vijana, Ana majukumu mengi, ikiwemo kuzungumza ana kwa ana na kijana juu ya Mambo yanayomzunguka, kuwashauri na kuwaongoza Vijana katika fursa mbalimbali na zaidi ana jukumu la kuhusika katika kuandaa sera zinazolenga kumsaidia kijana.

Watu Hawa Ni muhimu katika ngazi tofauti zikiwemo magereza, Shule, Vyuo na hata ofisi za umma na binafsi.

Naamini kwa uwepo wa JamiiForums kwa pamoja tutalisaidia kundi la Vijana wetu kufikia malengo yao ikiwemo kitaaluma na Maisha kwa ujumla wake.

Kuwa huru kushare nami yakusumbuayo kijana,Ikiwemo uchaguzi wa masomo, ugumu wa Maisha na harakati zake, au kama ungependa kujiongezea maarifa kuhusu ujuzi mbalimbali ambao unahisi utakusaidia hapo mbeleni.

Kwa kile nilichonacho kwa pamoja tutashirikiana.

Youth Worker

Hardness Teaches
 
Inapendeza...

Mkizipata hizo pesa za NGO basi mgawane nao hao vijana...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom