Kijana chini ya miaka 30, nicheo gani kikubwa umewahi kushika kwa kupigiwa kura

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Vijana tunapitia vipindi tofauti tofauti katika Maisha yetu, vingine vinatuchapa Ila vingine vizuri vinavyotupa tumaini ya safari zetu huko mbeleni.

Leo hii kijana ukienda kuchukua form ya kugombea ubunge kwa mfano wajumbe kabla hawajakupitisha watataka kusikia uzoefu wako Kama ulishahudumu cheo chochote hapo chuma kabla hujaenda kuomba nafasi hiyo.

Sasa Mimi kabla sijateuliwa kwenye nafasi moja kubwa katika kanisa nilikata Tamaa ya kuja kuchaguliwa kuongoza jambo lolote like kwa maana kula nilipojaribu kupiga kampeni bora Ili nichaguliwe niliishia kuwa wa pili nyuma ya Kinara.

Kasumba hiyo mwaka Jana nashukuru Mungu niliishinda pale ambapo Kama kijana niliingia kwenye ulingo kugombea Ukatibu Mkuu wa Parokia nakufanikiwa kushinda kwa kura nyingi mbele ya watu mashuhuli kwenye kanisa ngazi ya Parokia.

Uchaguzi huo ulitoka na viongozi wa jumuiya ambapo nilikuwa M/kitu wa jumuiya, nikachaguliwa kuwa katibu wa Kigango kutokana na viongozi wa jumuiya wote. Baada ya hapo viongozi wa vigongo tuliwekwa kwenye uchaguzi kupata viongozi wa Parokia.

Kitu hicho kilinivutia nakuona Sasa kumbe naweza ingia kwenye uchaguzi wowote na Mimi nikawa natumaini la kushinda tofauti na hapo mwanzo.

Kijana under 30 na wewe unaweza kuweka cheo kikubwa ulichopata kwa kupigiwa kura Bila kuteuliwa. Tujifunze kitu
 
Back
Top Bottom