Kijana atangaza kumng'oa Malecela Mtera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kijana atangaza kumng'oa Malecela Mtera

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Balantanda, Mar 8, 2010.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Na Sadick Mtulya

  MWANASIASA kijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa chama hicho, wilayani Tarime mkoani Mara, Livingstone Lusinde amesema mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela (75) ni mwenye siasa za chuki na pia amemsihi asigombee tena ubunge katika jimbo hilo.

  Lusinde alisema kauli ambazo Malecela aliitoa jana, inaashiria kwamba anazeeka vibaya na atamaliza vibaya.

  Lusinde ambaye ametoka kijiji cha Mvumi ambako Malecela pia anatoka, alimtuhumu Malecela kwamba ni mbinafsi na kwamba siku zote maneno na ahadi anazotoa si za kweli.

  Lusinde alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari wakati akitangaza nia yake ya kugombea ubunge kupitia CCM katika jimbo hilo.

  Kutokana na uchovu wa kushindwa kushawishi na siasa za chuki alizokuwa nazo mzee Malecela, uchu wa madaraka usiokuwa na kikomo pamoja na kugeuzwa na watu kumi kama taasisi ya Deci, amesababisha maendeleo duni katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.

  "Pia pamoja na kuwa amewahi kuwa msaidizi wa DC, Mkuu wa Mkoa, Balozi kwenye Umoja wa Mataifa na Uingereza, Waziri wa Kilimo, Mambo ya Nchi za Nje, Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara na Mbunge wa Jimbo la Mtera tangu lilipoanzishwa, amekuwa ni mbinafsi na kwamba siku zote maneno na ahadi anazotoa si za kweli,"alisema Lusinde.

  Lusinde alifafanua kwamba ameamua kutoa kauli hiyo, kwa kuwa Malecela alikiuka makubaliano waliyoafikiana mwaka 2005 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu kwamba mwaka huu Malecela, angeachiwa kugombea jimbo hilo.

  "Pamoja na Malecela kunilea kisiasa, miaka mitano iliyopita aliniahidi kwamba hatogombea mwaka 2010 katika Jimbo la Mtera, na sio tu kugombea Mzee Malecela alifika mbali zaidi kwa kunibariki kwamba nitakuwa mbunge wa Mtera ninayemfuata yeye.

  "Lakini amebadilika na kwenda kinyume na maneno pamoja na ahadi zake. Tayari ametangaza nia yake ya kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu," alisema

  Lusinde ambaye pia amewahi kuwa katibu wa CCM Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma alisema katika mwaka 2005, ilipofika wakati wa mchakato wa kuteuliwa na CCM kwa ajili ya kugombea Ubunge, Malecela alimuomba ajiondoe katika kinyanganyiro hicho na akakubali kutokana makubaliano maalumu waliyowekeana mbele ya mashahidi.

  "Keneth Salali ni mmoja wa mashahidi walikuwepo wakati mzee Malecela aliponiomba nijiondoe katika kinyanganyiro cha kuteuliwa na chama na aliniahidi kuwa mwaka 2010 hatogombea tena.

  "Namsihi Mzee Malecela aache mara moja mpango wake wa kugombea ubunge Jimbo la Mtera,"alisema Lusinde

  Hata hivyo, Lusinde hakuwa tayari kuyataja majina ya watu ambao anadai kuwa wamemgeuza Malecela kama taasisi ya Deci kwa kupanda na kumvuna.

  Lakini alisema watu hao ni wanachama wa CCM na mmoja wao aliwahi kuwa mlinzi wa Malecela kabla hajaumia.

  "Hawa watu kumi waliomgeuza Malecela kama DECI wapo kwa maslahi yao binafsi na muda ukifika kila mmoja nitawataja," alisema.

  Gazeti hili lilipomtafuta Malecela, liliambiwa kuwa yupo nchini Uingereza kwa kushughuli za kichama.


  Source: Gazeti la Mwananchi

  My Take:

  Naona kazi imeanza sasa Mtera,huyu kijana(Lusinde) ni mwanasiasa machachari hasa,nakumbuka mwaka 2005 alimuumiza kichwa sana mzee Malecela kiasi kwamba wakafikia makubaliano kwamba asubiri mwaka huu wa 2010,kijana alikubali hasa baada ya kupewa kazi ya kuwa Katibu msaidiz wa CCM wa wilaya ya Kongwa-Dodoma(Ikumbukwe kwamba kabla ya hapo alikuwa ni mwanachama wa NLD na mwaka huo wa 2005 alitaka kugombea kwa tiketi ya NLD na alikuwa tishio kiasi kwamba mzee Malecela hakuwa na la kufanya zaidi ya kumuomba ajitoe na pia kumshawishi ajiunge na CCM kisha akapewa nafasi hiyo ya Katibu msaidizi wa CCM(W).

  Binafsi Lusinde ni mtu wangu wa karibu sana na ni mwanasiasa mzuri hasa(CCM wanamtumia sana kwenye kampeni zao),wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Tunduru Lusinde alitumika ipasavyo katika kampeni kiasi cha kupelekea mgombea wa CCM ndugu Mtutula kushinda,baada ya hapo Lusinde alipandishwa cheo na kuwa Katibu wa CCM wa wilaya ya Tunduru,kisha baadaye akahamishiwa Tarime aliko sasa...Kijana ana kipaji hasa kwenye siasa za kuongea/kujieleza...Mzee Malecela inabidi ajizatiti hasa kama kweli kaamua kugombea maana Lusinde anawezambwaga(endapo hakutatokea mizengwe ndani ya CCM

  Pia kuna jamaa mwingine anaitwa Laurent Hoya(mmiliki wa mabasi ya Mshikamano na mabucha ya kisasa ya Mshikamano),huyu naye anakubalika sana Mtera na Mvumi,naye nasikia ana mpango wa kugombea ubunge wa Mtera na juzjuzi tu hapa kapewa Ukamanda wa vijana wilaya ya Chamwino...Kazi ipo Mtera mwaka huu,tusubiri na tuone
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Habari nyingine hii hapa kutoka Gazeti la Tanzania Daima:

  Malecela apata mpinzani Mtera

  na Betty Kangonga


  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Livingstone Lusinde, ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Mtera ambalo kwa sasa linashikiliwa na mwanasiasa mkongwe, John Samuel Malecela.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Lusinde alisema amefikia hatua ya kumvaa Malecela kutokana na maombi mengi ya wananchi wa Mtera ambao wanaamini atawasaidia kupunguza baadhi ya kero zinazowakabili.

  "Napenda kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo la Mtera kwenye uchaguzi mkuu ujao baada ya kuona mzee wetu Malecela umri unamtupa mkono… hivyo damu changa inahitajika ili kuleta maendeleo kutokana na wananchi wa Mtera kuwa nyuma zaidi kimaendeleo," alisema Lusinde.

  Lusinde, alitangaza uwamuzi huo akiwa na Katibu wa CCM Mtera, Keneth Salali, na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dodoma, Charles Sungura, ambao kwa pamoja walisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona Malecela amewatumikia wananchi wa Mtera kwa kipindi kirefu.

  "Mwaka 2005 nilimshika pabaya Malecela…yeye mwenyewe na viongozi wangu wa CCM waliniomba nimwaachie hadi 2010 lakini hali ya kushangaza mwanasiasa huyu mkongwe anaonekana kubadilisha mawazo na kutaka kugombea tena… namsihi kabisa aache asije akaumbuka bure," alisema Lusinde.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Mbona majina ni yaleyale huko Dodoma? Kuna vi-dynasties vya Ubunge vimeanza kukomaa huko kama tunavyoshuhudia kwenye CCM!
   
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mambo yanakuwa mambo....

  Wapi Mgombea Ubunge .
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,411
  Likes Received: 26,251
  Trophy Points: 280
  Habari za kuwashawishi na kuwafuta jasho wanaojitokeza kugombea naye Mtera sio ngeni sana. Nakumbuka 1995 nikiwa Dodoma nilizisikia hizo kuwa kuna mgombea akiitwa Dickson Mazengo alikuwa tishio ktk kura za maoni na akakatiwa chake na kutoa jina.
   
 6. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,339
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Huu utamaduni wa kuhukumu watu kwa umri na kusaka visingizio ili uonewe huruma na kupata Ubunge mie siikubali hata kidogo. Makubaliano ya chumbani unayaleta jamvini eti alikuahidi Ubunge !!! Lusinde ameonyesha uchanga wake na ni wazi siasa ameivamia tu ndg yetu. Malecela yeye huomba ridhaa kwa wananchi iweje akuahidi ubunge na wewe unakubali tu kama zumbukuku? Sidhani na sintakaa niamini huyu Lusinde aapewe ahadi ya kijinga kama hii toka kwa Legend kama mzee Malecela.

  Vijana tusikimbilie siasa kiholela holela tu. JK asipoangalia ataiangamiza nchi kwa kauli ile kuwa anahitaji vijana wengi this time! Anapaswa aseme kila chama kiimarishe na ku screen vijana wake ili tupate cream safi ya uongozi na siyo kualika tu maana watakuja hata wasio wenu kwa vile kuna chakula cha shughuli mtaani. Kuna wajinga wengi sana wamejitokeza majimboni ailimuradi tu wana vijishekeli basi taabu tupu.
   
 7. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  "Lusinde, alitangaza uwamuzi huo akiwa na Katibu wa CCM Mtera, Keneth Salali, na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dodoma, Charles Sungura, ambao kwa pamoja walisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona Malecela amewatumikia wananchi wa Mtera kwa kipindi kirefu."


  Tatizo ni kwamba order inatoka juu na wakiona wote wanaoomba kugombea ni vimeo wanamweka mtu wao! :D
   
 8. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anataka matatizo tuu huyo,au fungu alilopewa 2005 lilikuwa dogo sasa anataka malecela aongeze dau,mwaka huu!
   
 9. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Una uhakika jamaa alipokea fungu toka kwa Malecela? Kama ni kweli alipewa atakuwa alipokea rushwa au takrima?
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Balatanda unataka kununua vita .....ngoja aamke uone moto wake, ukizingatia anakufahamu! teh teh teh
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Bant,

  Makubaliano, kuachiana mbele ya mashahidi? Ubinafsi? Mzuri wa kuongea? halafu CCM? Siahasa bwana!
   
 12. M

  Mndamba Member

  #12
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hapa mkuu mimi sikubaliani nawe. Hivi watu kuendelea kuwang'ang'ania wazee hawa kwa kuwapigia chapuo la jinsi hii ndo kusema waendelee tu kuwa viongozi mpaka kufa kwao. HAPANA waingie watu wengine preferably vijana ili tupate mawazo na fikra mpya. Nadhani ni wakati muafaka sasa kuangalia kikomo cha uongozi say up to 70yrs old baada ya hapo waenda kulea wajukuu.

  Hebu angalia mtu kama Kigunge kweli ni fair yeye kuendelea kuwa kiongozi mpaka leo hii??? aaaah mimi binafsi inanikera sana kuona nafasi zenyewe za uongozi ni chache lakini mijitu mingine inang'ang'ania tu kuendelea kushikiria nyazifa mbali mbali kwenye vyama na serikari (mawazo na fikra za mwaka 1947) wakati wa-TZ wako zaidi ya milioni 40.
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hivi miaka 38 ni kijana?duu kwa katiba ipi au definition ipi?hata hivyo namhurumia kwani anapoteza muda wake.Malecela amehodhi lile jimbo.
   
 14. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  ..Mkuu sidhani kama Lusinde anapoteza muda. Hakuna mbunge mwenye hati miliki ya jimbo lazima watu wengine wenye uwezo kama wapo wajitokeze. Huyu mzee Malecela amegeuza siasa kama ndio ajira yake...Kwa kweli huu ni wakati muafaka wa kumpiga chini Malecela. Ukienda kijijini kwao Mvumi mission huwezi kuamini ni eneo ambalo ametoka mtu aliyekuwa na wadhifa wa waziri mkuu ni kituko nadhani isingekuwa wale wamisionari walioo pale mvumi watu wa pale wangekuwa na duni mpaka leo..
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Field Marshall ES yuko wapi? Jimbo la Mrera ndio linaanza kuondoka hivyo!!
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Heheeeeeeee,hakuna cha vita wala nini,hii ni taarifa tu Nkwingwa kama zilivyo taarifa zingine,nadhani kama ni vita iwe ni dhidi ya Livingstone ama magazeti ya Mwananchi na Tanzania Daima yaliyochapa taarifa hii...Kuanzisha vita na Balantanda itakuwa ni kumuonea tu............
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mkuu jiandae kuvuliwa kofia! Kila laheri kwenye CL
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masanilo, You've made my day. Umefanya nicheke kwa sauti kubwa waliokaribu yangu wamenishangaa!
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaaaa,havuliwi mtu kofia hapa...Nashukuru aisee,ila hali ndo kama unavoiona,majeruhi kibao
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,210
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  safari hii atapelekwa kusoma nje ya nchi

  hamwezi yule mzee ndo maana anakubli kirahis kubadili msimamo wake
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...