Kiini Macho Kingine cha TUME ya Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiini Macho Kingine cha TUME ya Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mizambwa, Oct 30, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Tanzania tumekuwa na utitiri wa TUME zinazoundwa kuchunguza mambo mbalimbali lakini majibu ya TUME hizo hayawekwi hadharani.

  Tume inpoundwa inatangzwa na pia muda wa uchunguzi unawekwa wazi lakini matokeo yake hayawekwi hadharani.

  Kuna umuhimu gai wa kuunda Tume zinazotumia pesa nyingi ya walalahoi ambayo ingelisaidia huduma za jamii???

  ANGALIA KITUKO KINGINE HIKI CHA BUNGENI!!!!

  ========================================================================================================

  Wingu laigubika Ripoti ya Ngwilizi - Habari - mwananchi.co.tz

  WINGU LAIGUBIKA RIPOTI ya NGWILIZI


  Waandishi Wetu, Dodoma
  WAKATI Bunge likianza mkutano wake wa Tisa leo, zipo taarifa Ripoti ya Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa haitasomwa na kisha kujadiliwa.
  Badala yake, kwa mujibu wa watoa habari wetu, Kamati ya Uongozi, iliyokutana jana iliamua kwamba litatolewa tamko kuhusu ripoti ya kamati hiyo, hivyo haitasomwa wala kujadiliwa kama ambavyo wabunge wamekuwa wakitaka.

  Kwa maana hiyo Spika wa Bunge, Anne Makinda huenda akatumia kanuni nyingine kutoa tamko kuhusu uchunguzi huo, hali ambayo haitatoa fursa kwa wabunge kuijadili kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakishinikiza.
  Miongoni mwa kanuni ambazo Spika anaweza kuzitumia ni pamoja na ile ya 33 (2) ambayo inasema: "Wakati wa kikao, Spika anaweza kutoa taarifa nyinginezo kadri atakavyoona inafaa."

  Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel jana alikataa kuzungumzia suala hilo akiahidi kulitoa ufafanuzi leo... "Ratiba ya shughuli za Bunge bado iko kwenye ngazi ya Kamati ya Uongozi. Sasa pengine tusubiri kesho (leo) ikiwa tayari kila kitu kitakuwa wazi, hakuna haja ya kuwa na haraka."
  Jana, Kamati ya Uongozi wa Bunge ilikutana mjini Dodoma kujadili mambo mbalimbali na habari zinasema kwamba suala la Ripoti hiyo ya Ngwilizi, pia lilijadiliwa.

  Agosti 2 mwaka huu, Spika Makinda aliunda kamati hiyo ndogo kuchunguza tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wabunge ambao walidaiwa kwamba walihongwa ili kuikwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

  Kuundwa kwa kamati hiyo, kulitanguliwa na tukio la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Julai 28, mwaka huu pia kutokana na tuhuma hizohizo.
  Tayari kumekuwa na taarifa kwamba ripoti hiyo imevuja na maudhui yake kuchapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari, hali ambayo ilisababisha Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuonya kwamba waliohusika na kuvuja huko huenda wakajikuta matatani kwani ni kosa la kisheria.

  "Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo katika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 31 (1) (g) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura 296," alisema Ndugai katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni.

  Mmoja wa wabunge ndani ya kamati iliyochunguza suala hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa), ndiye anayedaiwa kwamba aliivujisha ripoti hiyo ya uchunguzi kwa makusudi, lengo likiwa ni kumshinikiza Spika Makinda aitoe hadharani ili kuwasafisha watuhumiwa.

  Mbunge huyo alifanya hivyo kwa msukumo wa baadhi ya wabunge waliotuhumiwa kujihusisha na rushwa, pamoja na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kabla ya kuvunjwa.
  Kadhalika, Ndugai katika mkutano wake na vyombo vya habari alisema suala la ripoti hiyo kusomwa bungeni au vinginevyo linategemea uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge.

  Ndugai alisema baada ya kamati kuwasilisha ripoti kwa Spika, Kamati ya Uongozi ya Bunge itakaa kujadili na kama itaona kuna umuhimu wa kuingizwa katika ratiba ya vikao vya Bunge ijadiliwe.
  Alisema Vifungu 114 (17) na 119 (1) hadi (6) vya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007 kwa pamoja vinampa madaraka Spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni.
  Kamati hiyo iliyoundwa na Spika ilikuwa chini ya Ngwilizi ambaye ni Mbunge wa Mlalo, ina wajumbe; Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma. Kamati hiyo ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa spika tangu Septemba 20 mwaka huu.

  Kamati za vyama

  Kamati za vyama bungeni zinatarajiwa kufanya vikao vyake leo asubuhi.
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alisema
  Kamati nyingine za Bunge hazijakutana kutokana na wabunge wengi kuwa safarini kwenda mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge.

  "Kwa taarifa tulizopokea sasa ni kwamba kamati zimeshindwa kukutana kutokana na wabunge wengi kuwa njiani kuja mjini hapa, hivyo kwa vyovyote kesho (leo) Bunge litakuwa ni fupi ili wabunge wapate nafasi ya kuandaa utaratibu mzima wa ratiba za vikao," alisema Minja.
  Alisema leo mara baada ya kuanza kwa kikao hicho, Bunge litatoa nafasi ya maswali na majibu ambayo Serikali itayajibu kabla ya kuahirishwa.

  Mara baada ya kuahirishwa saa nne asubuhi, kamati za vyama zitakutana kupitia mambo mbalimbali kabla ya kuingizwa kwenye kamati mbalimbali za bunge.
  Moja ya mambo yanayotarajiwa kutawala katika kamati za vyama ni pamoja na wabunge wa CCM kujiweka sawa kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa ripoti ya Kamati ya Ngwilizi.
  Kingine kitakachojadiliwa katika Mkutano huu wa Bunge ni muswada binafsi kuhusu fao la kujitoa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tayari Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika wamewasilisha miswada yao kwa Katibu wa Bunge, Tomas Kashillilah.
  ===================================================================================================
   
 2. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nmshangaa Spika na Kamati yaker ya uongozi. Inaelekea lengo lao ni kulindana kwani walioonekana kujihusisha na rushwa ni wabunge wa CCM. Katiba mpya iruhusu mwananchi ye yote kumfikisha mahakama kuu Spika kama atapindisha haki kwa kanununi yo yote ile. Kwani hayuko juu ya Katiba huyo.
   
 3. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi naungana na baadhi ya Wabunge wa Upinzania ambao walipendekeza kuna Kanuni za Bunge zimepitwa na wakati, ziliandaliwa wakati wa Chama Kimoja.

  Ni wakati sasa kuzipitia tena na baadhi zifutwe kabisa.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,553
  Likes Received: 16,519
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama sheria kweli zimepitwa na wakati,ni tatizo la viongozi wetu waliomadarakani kuzitumia vibaya.Nina uhakika kanuni hizo hizo zingeweza kulipeleka taifa letu hatua kumi mbele kama zingetumiwa kiadilifu na kwa muogopa mungu aliyetupa uhai.
  Spika anauwezo wa kutumia sheria hizo vizuri kwa manufaa ya taifa letu badala ya kuogopa watu na kuficha uovu.Ifike mahali Spika wetu Anna Makinda aangalie miguu yake na roho yake je ana uhalali wa kwenda kanisani kila siku asubuhi wakati anachokifanya kinahalalisha uovu?Ajipime halafu achukue hatua!:confused:
   
 5. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ripoti ya kamati ya Ngwilizi imewasafisha wabunge na tuhuma za ukaji Rushwa,na wanataka kuibana Serikali kua ina makosa hasa Waziri Prof .Muhongo,kwa upande wake yenyewe Serikali (Muhongo) imedai inao ushaidi usio na shaka kua wabunge walikula Rushwa.
  Hivyo Spika anataka kuikalia hiyo Ripoti akitaka kuwaokoa wabunge wenzake,kwasababu anajua Prof Muhongo huwa hakurupuki mara nyingi anaongea kile anachomaanisha.
  Wabunge wanajaribu kulindana kabla ripoti hiyo ilivyoandaliwa.
   
 6. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni vema ukapeleka maoni kwenye tume ili yaingizwe,badala ya kulalamika!
   
 7. O

  OPTIMUS TZ JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngwilizi na Rushwa ni kama yai na gamba lake ilitarajia nini wakuu!
   
 8. washa

  washa JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 476
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wanajamvi kuna yeyote ambae ana nakala ya ripoti hiyo?..ninaamini ni haki yetu sisi walipakodi kuelewa hawa wanatume walikuwa wanafanya nini na pia tujue walichobaini lakini muhimu sana ni kutumia taarifa za tume hyo kuona weledi, umakini na uzalendo wa hawa wenzetu walioshiriki katika tume. La mwisho ambalo ninahisi ni kubwa ni hili lakuona bunge kama chombo chetu cha uwakilishi kinatuwakilisha kweli katika kuisimamia serikali iliyoko madarakani.
   
 9. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama sio mara zote basi mara nyingi tume huundwa kupotezea!Uamini Chunguza!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Ndiyo ukweli huo mkuu,wameitafutia sababu ili isisomwe.Kama ni madhara ya kuilikisha waliyajuwa,na wamefanya makusudi,halafu kweli sisi ni wadanganyika,certainly ni upepo tu utapita!
   
 11. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Zimepitwa na wakati kwasababu zinatoa mwanya wa viongozi wetu kuzitumia vibaya. zirekebishwe ili zisitoe nafasi kama hii
   
 12. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mi sina hamu na kinachojadiliwa huko kama hawajarudisha fao la kujuitoa wafie wote humo humo ndani ya mjengo.Tume za nini kwani Tanzania imeanza kuibiwa leo, waachane na mambo ya tume wajadili mambo yanayowagusa direct wananchi kama fao la kujitoa
   
 13. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ndugu ili kuficha ukweli Bwana Ndugu ai akatoa kitisho kuwa HAIRUHUSIWI KUWEKA REPORT HADHARANI kabla ya kupitishwa Bungeni.

  Hivyo kila mmoja ataogopa kwa muda huu, na ndio Serikali yetu kila kitu wanafanya SIRI ili wananchi wasijue uozo wao.

  Lakini yote yana mwisho tu haya.  MIZAMBWA
  IANNIUMA SANA!!!
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  mpaka ufike mwisho wake umeshaumia sana
   
 15. c

  cencer09 JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 2,320
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 180
  wale wabunge nagamba waliokuwa wanapiga kelele kwamba zito ndiyo amekula rushwa sasa hivi kimya wanaangalia ni jinsi gani ya kuficha uozo wa magamba wenzao,spika anataka kuwasevu,naibu spika kaweka mkwara,hao ndiyo ccm,tunasubiri watetezi wao watuambie humu jamvini nini kinaendelea
   
 16. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Yaite viini macho vya bunge. Ndo zao
   
 17. S

  Swat JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 4,182
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Repoti ya tume si sawa na research report ambayo inaweza wekwa hadharani for public use. Report ya tume hupelekwa kwa alieiunda. Labda huyo kama atataka kuiweka hadharani ndio public mtaiona lakini pia anaweza kutoiweka hadharani na akaamua kuchukua hatua kimyakimya. Ndio sheria na utaratibu wa tume. Tumlaumu aliyeunda tume na si tume kama tutafichwa matokeo.
   
 18. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kwa utaratibu huu ilipaswa hata wakati wanauda Tume wasitutangazie kuwa kuna tume imeundwa kuchunguza jambo fulani. Wafanye siri pia kwa sababu haituhusu kuijua, kwa mtindo huo.

  Na kama ikitangazwa basi i9na maana ni kwa manufaa ya umma wa Watanzania.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...