Kiingereza cha kwenye hukumu ya mbunge Sugu na masahihisho yake

Huyo hakimu na huyu Ticha. Nani anaunafuu?
b0d1085cd6c16ebe2b94aeb4aa63ed70.jpg
 
Kiingereza cha pre form one,
*I shall went tomorrow*
*Don't smoke my river*
Hhahahahah mmenikumbusha mbali saaana
 
Hilo ndo suala la kujiuliza, kwani angetumia kiswahili hii hukumu isingekubalika?. Hakukuwa na sababu ya kutumia lugha ambayo hana uwezo wa kujieleza vizuri.
Hukumu na hata Mwenendo wa kesi Waheshimiwa huwa wanaandika kwa kutumia 'Kikristo'.

Tunacholetewa kwenye vyombo vya habari mara nyingi ni tafsrisi au nukuu za wahabarishaji.
 
Legal language. Biblical language. Ukitaka uzitafutie sarufi sahihi utapoteza maana.
Hapana,
Sio kweli, Tusilee maradhi.
Haijasemwa mahali kuwa Lugha iliyotumika ni ngumu, Ni ya Kitaalam au Haieleweki.

Tatizo la wazi hapa ni kuwa Lugha ya Malkia kwake ni shida.
Nahii si yeye tu wako wengi kwenye taasisi Hii.
 
Hii hapa ndio hukumu, ebu tujifunze kitu kwenye sentence construction kwa lugha ya kimombo kwa nia njema tu.

View attachment 702903

sentence

Has the greatest political significance in the country ?????????maana yake nini

In the national level and internationally?????? Ndo nini

The president is a nation icon??????? Alitaka kusema nini hapa, asiyejua rais ni mwakilisi wa nchi ni nani.

If be contracts sickness even not serious the country must loose it value????? Hapa anataka kusema nini kama sio mchumi au hujasomea maswala ya kiuchumi usijichomeke huko hamna maana yoyote, wapo marais wanao umwa na uchumi wa nchi unaendelea kukua, sasa sentence hii sijui alikuwa anamaanisha nini.

There is a great gap between the president and a normal citizen???? Hii tafsiri ya Kiswahili kwenda kingereza, ana maanisha nini, neno gap hutumika pale ambapo kuna mapungufu.

The president has the greatest political significance in the country???? walau angesema hivi The president of the United Republic of Tanzania play a major role in the political system, from national to international level.

I think it is a parliament only can dissolve the powers of the president??? Asahihishe hapa tafsiri ya moja kwa moja kutoka kiswahili kwenda kiingereza badala yake angesema: the parliament has the mandate or power to dissolve….

It is dangerous if a citizen will not honor or show respect to the president???? Hapa alikuwa anamaana gani na kwanini aweke neno dangerous badala ya: it's unlawful for a citizen to disrespect the president.

How is possible for a citizen to have a courage of using insulting words or defamatory words to lowering the status of the president??????hapa alikuwa ana maanisha nini hii tafsiri ya moja kwa moja kutoka Kiswahili kuelewa maana halisi hapa ni taabu sana badala yake angesema: where does the citizen gets the courage to insult the president

It is dangerous if a normal citizen will show disrespect to the president who is a main political leader of the country??????? Hapa ana maanisha nini, hivi huwa kuna normal citizen na ambaye sio normal citizen, halafu nchi ni ya vyama vingi kila kiongozi wa chama chake ni main political leader wa chama hicho sasa hapa kwanini katumia haya maneno. Badala yake angesema its unlawful for a citizen to disrespect the president…

I think and am quite correct??? Kwanini atumie haya maneno kwenye hii sentensi anamaanisha nini hayafai kuwepo hapa.

I think a good way, if the citizens do not have trust in the president they should use parliament to vote down a government rather than using social media or political platform insulting the president and other leaders???????? Makosa ni mengi sana hapa kwanza badala ya kusema hivi angetupa vipengele vya katiba na ku highlight, maana kutengeneza maneno ya kiswahili kuyaleta kwa kiingereza haitupi maana halisi haya hutufanya tuendelee kuonekana kuwa bado hatuja master lugha vizuri, matumizi ya neno TO VOTE DOWN maana yake nini haswa,

Having considered all opinions and mitigations on sentence????? Neno mitigation amelitumia vibaya hapa halifai kuwepo hapa

TUNAHITAJI KUONGEZA COURSE ZA ENGLISH ILI TUWEZE KUJINOA NA KUREKEBISHA KWA KUTOUNDA SENTENSI ZINAZOENDANA NA DIRECT TRANSLATION FROM SWAHILI TO ENLGLISH.

NINGETOA CORRECT SENTENSE CONSTRUCTION YENYE MAANA YA HUKUMU HIYO HIYO ILA SIWEZI KUFANYA HIVYO MAANA TAYARI IMESHATOLEWA

Wanakuambia hukumu iliandikiwa hotelini na maelezo yalitoka juu unajua labda hukumu iliandikwa kutoka juu maana hata juu kuna ugonjwa huo huo wa kutokujua ngeli
 
Back
Top Bottom