Kiingereza cha kiTanzania
Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.
Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.
Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE
Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.
Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.
Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.
Naomba kuwasilisha.
Natumai huko mahakamani, mahakimu na waendesha mashtaka huwa wanaandika maelezo kwa kiingereza.
Sentensi kama hii wataiandikaje? ........"nilitoka kwa baba mdongo na kuelekea kwa mjomba ambako nilikuta mauaji yametokea........"
What difference does it make? Ninavoelewa hapo maneno yote yamekua ya kiingereza ila umeamua tu kurefusha sentensi. Ama umeunga maneno mawili na kuyalazimisha yalete maana ya neno moja.
Hivi lugha yetu ni SWAHILI LANGUAGE au KISWAHILI LANGUAGE......nimekutana na mgongano huu kwenye vyombo vyetu madafu vya habari vinavyoandika ki-british
Karibu sana Matofali. Jisikie huru kutoa maoni ya thread mbali mbali.Halo ndugu na jamaa wa jamii forum mimi ni member mpya naomba ukaribisho wenu.
Ukiongea kiingereza lugha hii ni "Swahili" wala si "Kiswahili"
Ki ilivyotumika hapa ni kitangulizi (prefix) katika lugha ya kiswahil kinachoonyesha hii lugha imetoka wapi, ndiyo maana kila lugha inaanzwa na Ki, Kisambaa, Kizulu, Kiingereza, Kirusi n.k.
Kwa hiyo ukiweka "Ki" unatoka katika Kiingereza na kusema kiswahili, na "Kiswahili Language" inachanganya kiswahili na kiingereza.
Ama utasema "Lugha ya Kiswahili" au "The Swahili Language"
Ama utasema "Lugha ya Kiingereza" au "The English Language"
Huwezi kusema "Kiswahili language" kama usivyoweza kusema "Kienglish language" au "Kiingereza Language"
Utakuwa unachanganya mambo.
Swahili and Kiswahili are interchangeable.
It is perfectly alright to say "Tanzanians speak Kiswahili" or "Tanzanians speak Swahili"
... xo xo xo ...