PostGE2025 Kihongosi: Hotuba ya Rais akifungua Bunge ni ya msamaha na huruma

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amesema hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 ni hotuba ya kujenga umoja wa kitaifa, msamaha na mwelekeo mpya wa maendeleo kwa Watanzania.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma siku ya Jumatano, Kihongosi amesema hotuba hiyo iliainisha masuala mengi ya msingi kuhusu umoja, maadili, upendo na mustakabali wa taifa, akibainisha kuwa Rais Samia alisisitiza wajibu wa Watanzania na viongozi kushirikiana katika kuijenga na kuilinda nchi.

Kihongosi amesema hotuba hiyo inaweza kuitwa hotuba ya ujenzi wa mshikamano kwasababu Rais Samia alisisitiza kuwa jukumu lake na la wabunge ni kuendeleza umoja wa kitaifa ili taifa liweze kupiga hatua katika maendeleo na kulinda hadhi ya Tanzania kimataifa.

Amesema pia kwamba hotuba ya Rais Samia ilikuwa na ujumbe wa huruma na msamaha, kufuatia kauli yake ya kuomba vyombo vya sheria, hususan ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia uwezekano wa kuwasamehe vijana waliokamatwa kutokana na matukio ya vurugu za Oktoba 29, 2025. Kwa mujibu wa Kihongosi, Rais Samia alieleza kuwa baadhi ya vijana walijikuta wakijihusisha na vurugu hizo kwa kufuata mkumbo, hivyo kama mlezi wa taifa ameonesha moyo wa huruma kwa kuwatakia msamaha.

Amesema pia hotuba hiyo imeweka wazi kasi ya utekelezaji wa maendeleo, akibainisha kuwa ndani ya siku 11 tangu Rais Samia aapishwe, ajira mpya 12,000 tayari zimetangazwa zikiwemo ajira 7,000 za walimu na 5,000 za watumishi wa afya.

Kihongosi amesema hatua hiyo inaonysha serikali inatekeleza ahadi zake ndani ya siku 100 za kwanza, na ameeleza kuwa marufuku ya hospitali kuzuilia miili ya marehemu kwa sababu ya malipo imeanza kutekelezwa nchini kote, hatua ambayo Rais Samia aliwahi kuiahidi wakati wa kampeni na kuirudia mara kadhaa.

Mboga mboga yamechanganyikiwa hayajui wafanye nini kutuliza hali.

Vile vitisho vya mtu anakufa mara moja tu kutoka kwa makamanda sivisikii tena kuelekea 9D.
 
Siku hizi CCM haina tofauti na magenge ya wauaji kama Boko Haram tofauti yake kimesajiliwa kihalali.
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amesema hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 ni hotuba ya kujenga umoja wa kitaifa, msamaha na mwelekeo mpya wa maendeleo kwa Watanzania.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma siku ya Jumatano, Kihongosi amesema hotuba hiyo iliainisha masuala mengi ya msingi kuhusu umoja, maadili, upendo na mustakabali wa taifa, akibainisha kuwa Rais Samia alisisitiza wajibu wa Watanzania na viongozi kushirikiana katika kuijenga na kuilinda nchi.

Kihongosi amesema hotuba hiyo inaweza kuitwa hotuba ya ujenzi wa mshikamano kwasababu Rais Samia alisisitiza kuwa jukumu lake na la wabunge ni kuendeleza umoja wa kitaifa ili taifa liweze kupiga hatua katika maendeleo na kulinda hadhi ya Tanzania kimataifa.

Amesema pia kwamba hotuba ya Rais Samia ilikuwa na ujumbe wa huruma na msamaha, kufuatia kauli yake ya kuomba vyombo vya sheria, hususan ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia uwezekano wa kuwasamehe vijana waliokamatwa kutokana na matukio ya vurugu za Oktoba 29, 2025. Kwa mujibu wa Kihongosi, Rais Samia alieleza kuwa baadhi ya vijana walijikuta wakijihusisha na vurugu hizo kwa kufuata mkumbo, hivyo kama mlezi wa taifa ameonesha moyo wa huruma kwa kuwatakia msamaha.

Amesema pia hotuba hiyo imeweka wazi kasi ya utekelezaji wa maendeleo, akibainisha kuwa ndani ya siku 11 tangu Rais Samia aapishwe, ajira mpya 12,000 tayari zimetangazwa zikiwemo ajira 7,000 za walimu na 5,000 za watumishi wa afya.

Kihongosi amesema hatua hiyo inaonysha serikali inatekeleza ahadi zake ndani ya siku 100 za kwanza, na ameeleza kuwa marufuku ya hospitali kuzuilia miili ya marehemu kwa sababu ya malipo imeanza kutekelezwa nchini kote, hatua ambayo Rais Samia aliwahi kuiahidi wakati wa kampeni na kuirudia mara kadhaa.
Mtu kaua maelfu kwa maelfu halafu anatoa msamaha kwa huruma?
 
Mpuuzi huyo Kihongosi, kwamna hatujui huruma ni nini? Halafu muuaji anakuwaje ma huruma?
 
Aseme sasa walipo akina Polepole. Otherwise ni mshenzi kama washenzi wengine.
Nchi hii sio mali ya chama chochote kikiwemo CCM.
 
Screenshot_20251114-214608~2.png
 
Tangu lini Israeli mtoa roho za watu akawa na huruma! Aache kudanganya watu.
 
Back
Top Bottom