Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema ushindi wa chama hicho katika uchaguzi unatokana na nguvu na mizizi iliyoanzia ngazi za chini, hivyo haupaswi kuwa ajenda ya kuhojiwa na vyama vya upinzani.
Akizungumza kwenye Kikao cha Shina Namba Moja, Singida Mjini leo Januari 19, 2026, Kihongosi amekitaka chama chochote kilichosusia kushiriki uchaguzi kuacha kuuliza kuhusu matokeo, akisisitiza kuwa hakina uhalali wa kufanya hivyo.
“Kuna chama kiligoma kushiriki uchaguzi, vyama vingine vikashiriki, CCM kikashinda kwa kishindo wanahoji ‘mmeshindaje shindaje?’ Wewe hujashiriki uchaguzi unauliza kama nani? Umesusa, umekataa, watu wameshinda unaanza kunung’unika. Raha ya ngoma ni kuingia kucheza,” amesema.