Kihoja cha de-dollarization, Urusi katika mkwamo na maburungutu ya Rupee za India

Kihoja cha de-dollarization, Urusi katika mkwamo na maburungutu ya Rupee za India

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,630
Reaction score
110,318
Inaripotiwa kwamba Urusi iko katika mkwamo mkubwa kwa kujikusanyia mzigo mkubwa wa Rupee za India bila kujua itazitumiaje au kuziwekeza vipi

Mapema mwaka huu katika joto la siasa za biashara za kimataifa, wanasiasa wa Urusi na India walikubaliana wafanye biashara kati yao kwa sarafu za nchi zao hali iliyopelekea India kuanza kununua mafuta na gesi vya Russia kwa pesa yake ya Rupee badala ya US dollars.

Tatizo limekuja kwamba Russia imeendelea kupokea bilioni za Rupee ambazo kwa sasa zimefikia thamani ya dollar za kimarekani billion 147 huku ikiwa haielewi itazifanyia nini.Tatizo kubwa ni urari mbovu wa biashara kati ya mataifa haya kwa sababu mahitaji ya Urusi ya bidhaa kutoka India na kuwekeza huko ni madogo sana wakati mahitaji ya India ya nishati ya Urusi ni makubwa sana.

Pia kuzibadilisha hizo Rupee imekuwa mtihani mwingine kutokana na benki na kampuni nyingi duniani kutotaka kujiingiza katika hatari za vikwazo vya biashara vya Marekani na washirika wake.

Njia pekee inayotegemwa na Urusi kwa sasa katika mkwamo huu ni kuboreka kwa urari wa biashara kati ya India na Urusi kwa Urusi kuongeza kununua zaidi mahitaji yake kutoka India dhidi ya kiasi inachouza kwa India.

Changamoto nyingine ni kwamba kuongezeka kwa mfumuko wa bei nchini India kutazidi kuporomesha na kufuta thamani ya hizo Rupee hali ambayo itawapa hasara zaidi Warusi waliolipwa kwazo.

US Dollar ni kama mbuyu fulani hivi, kuuangusha hakuhitaji mihemuko bali kufanya kazi kweli kweli na kwa muda mrefu sana.
 
Katika hiyo biashara Urusi anapoke fedha ya India ama anapokea fedha yake mwenyewe? Urusi alitangaza anauza mafuta yake kwa pesa yake ya Ruble.
Jiongeze, tumia kichwa chako vizuri.
Sasa India ingezipata wapi hizo Rubu za Urusi wakati biashara kati yao ilikuwa ni kama tone tu kabla ya uvamizi wa Urusi Ukraine??
 
Unakuwa na mabilioni ya makaratasi ambayo hayawezi kutumika popote zaidi ya baina yenu tu! Ha ha ha!

Wahindi wana akili sometimes; supa le paware kalazimishwa kupata mahitaji yake toka uhindini kimtindo ambako nako hawezi kuyapata yote. Akatunze hizo papers makumbusho.
 
Unakuwa na mabilioni ya makaratasi ambayo hayawezi kutumika popote zaidi ya baina yenu tu! Ha ha ha!

Wahindi wana akili sometimes; supa le paware kalazimishwa kupata mahitaji yake toka uhindini kimtindo ambako nako hawezi kuyapata yote. Akatunze hizo papers makumbusho.
Kwahiyo atalazimika kununua pilipili kitoka India,ila ²power bwana
 
Windhoek mito costview mbona mnaongea kishabiki sana? Hivi urari wa ufanyaji biashara si ndiyo kwa Kiingereza unaitwa " balance of Payment"?

Sasa Urusi si imekubaliana na India watumie Sarafu zao kulipana wanapouziana bidhaa zao?

Kwa ivo Urusi ikiiuzia India mafuta si italipwa Kwa Rupia? Italipwaje kwa Rubles wakati siyo Sarafu ya India?

Na Urusi nao wakitaka kununua kababi na Tambuu India si watalipa kwa Rupia walizozipata toka kwa India waliponunua Mafuta??

Sasa tatizo limekuja kuwa Urusi hainunui bidhaa nyingi India na kufanya Rupia wanazolipwa kwa kuuza bidhaa zao India (hasa mafuta) kurundikana kwenye mabenki ya Urusi.
Hili nalo ni la kubishia?
 
Sasa si anunue tuone
Sasa hivi waagizaji wa mafuta wanaagiza mafuta toka India, Urusi wanaweza kutumia mwanya huo kumwaga rupee za India badala ya kutumia Dola wakatumia rupee Ila hayo ni mawazo yangu Kama ningekuwa wazuri wa fedha.
 
Nilijua nguvu ya dollar siku moja nilisafiri kuingia kwenye nchi mojawapo wa humu Afrika, nikasahau kubadilisha hela yetu ya Kenya kwenda kwa dollar nikiwa bado kwetu.
Yalinikuta nilipoanza kuzunguka mji wa watu kwa bodaboda nikitafuta bureau ya kuchukua shilingi yetu, ilibidi niuze kwa hasara.
 
Western hawataki kukubali ila hata huu mkwamo wa Dola urusi Wana mkono maana kabla ya vita nchi nyingi zilinunua nishati kwa Dola kutoka urusi so billions of dollars zilikua zinaenda urusi
Hizo billions of dollars Urusi ilikuwa imezihifadhi kama foreign reserves kiasi cha USD billion 600 huko Marekani, nchi za Ulaya, Japan na washirika wengine wa US ambapo kwa sasa zimewekwa vikwazo.
 
Sasa hivi waagizaji wa mafuta wanaagiza mafuta toka India, Urusi wanaweza kutumia mwanya huo kumwaga rupee za India badala ya kutumia Dola wakatumia rupee Ila hayo ni mawazo yangu Kama ningekuwa wazuri wa fedha.
Rupee nyingi zaidi ziko katika benki za India na zinakuwa vigumu kutolewa kupelekwa nchi nyingine kwa sababu India ina sheria ngumu za kuhamisha mitaji kutoka nchini kwake, pia wafanyabiashara na makampuni kwingine duniani hawataki kujiingiza katika migogoro ya vikwazo vya West.
Halafu pia mataifa mengi kama sio karibia yote yanayonunua mafuta safi India wanalipa kwa dollars, Hata sisi Tanzania wafanyabiashara wetu wanalipa kwa dollars na itakuwa vigumu sana kukubali kuanza kutumia Tshs au Rupee katika hiyo biashara.
 
Back
Top Bottom