Kigwangalla Kimyaaaa! Usicheze na CCM Bana!

Hivi karibuni mbunge wa Nzega (CCM), Dkt. Hamisi Kigwangalla amekuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii kuhusiana na misimamo yake madhubuti isiyoyumba iliyopelekea kutaka kufukuzwa kwenye chama chake. Tukasikia kuwa yuko mbioni kujiuzuru yeye mwenyewe kabla ya kusubiri ahukumiwe kufukuzwa. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ongezeko la posho ya wabunge kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa kila kikao akidai ni aibu kwa wabunge kukubali dhulma hiyo wakati wao wanafanya kazi masaa 8 tu ukilinganisha na madaktari wanaokesha kwenye mahospitali na kufanya kazi masaa 36. Mbunge huyu pia msimamo wake kwenye suala la madaktari umekuwa wazi sana. Yote haya yamepelekea kuwa tofauti na wenzake na hata kupelekea kuzomewa, kuzongwa na wenzake na kuambiwa akae chini kwenye vikao.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaona Kigwangalla amekuwa kimya mno bunge hili ikilinganishwa na mabunge mengine ambapo alikuwa maarufu kwa kuonyesha umahiri wake wa kutumia vizuri kanuni za bunge kwa kuomba mwongozo wa spika na kuonesha upana wa uelewa wake wa mambo mbali mbali kwa kutoa taarifa kwa wabunge wenzake wakiwa wanaongea. toka bunge hili lianze, katika hali ya kushangaza, Kigwangalla amekuwa kimya kabisa! Ndiyo kusema wamefanikiwa kumnyamazisha ama hana hoja tu? Ametuacha na maswali mengi zaidi ya majibu. hebu aibuke hapa atoe majibu.

Sio lazima kuongea tuu hata kama huna la kuongea. Unatakiwa utulie mpaka pale unapoona kuna hoja ya msingi ambayo anaweza kuchangia kwa upeo wa juu sio lazima uongee tuu ili mradi unaongea na ndio maana kuna wabunge wengine huwa wanaongea hewa na upeo,
 
Back
Top Bottom