Kigwangalla amjibu Bashe Kiaina Kuhusu Pamba Nzega! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla amjibu Bashe Kiaina Kuhusu Pamba Nzega!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zulqarnayn, Nov 8, 2011.

 1. Z

  Zulqarnayn Senior Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kutoka Blogu ya Kigwangalah (MB), Nzega: Dr. Hamisi Kigwangalla's Round Table: Mapinduzi ya Kijani (Pamba) Yamefanikiwa Nzega!
  Wiki iliyopita Hussein Bashe, hasimu na mshindani mkubwa wa Mbunge Kigwangallah alifanya ziara katika kata 6 za Nzega ambapo pamoja na kupika pilau na kutoa ahadi nyingi (according to post ya FB ya Hamis Kigwangallah), Bashe alipiga marufuku kilimo cha Pamba, alizeti na Mtama, mazao ambayo yanahamasishwa na kampuni ya Mbunge huyu. Mbunge kigwangallah alikuja juu na kulalamika kwa mamlaka mbalimbali, media za mtandaoni na hatimaye alifanikiwa kukwamisha ziara ya Bashe jimboni Nzega. Pamoja na kwamba watu walimponda sana Kigwangallah kwenye FB kuhusiana na mazoea yake sasa ya kumwita Bashe msomali, haramia, alshabaab na kung'ang'ania kwamba uraia wake una utata, nadhani anafanya kazi nzuri na kama akiendelea hivi wala hana haja ya kumshambulia Bashe, wananchi watakula pilau na hela za Bashe na watamchagua kigwangallah...haya ndiyo mambo ya kufanywa na Mbunge ! Chukua 5 Bagaile!

  Mapinduzi ya Kijani (Pamba) Yamefanikiwa!


  Katika hali ya kutia moyo, wilaya ya Nzega imefanikiwa kufufua kilimo cha Pamba. Zao hili la biashara lililokuwa limepotea kabisa wilayani hapa sasa limerudi upya tena, japokuwa si kwa kufikia kiwango cha zamani lakini mwanga wa matumaini unaangaza kila kona. Wilaya ya Nzega iliacha kulima pamba takriban miaka 12 iliyopita kufuatia kuanguka kwa utaratibu mbovu wa ushirika uliokuwepo. Tatizo hili halikuikumba Nzega peke yake bali ukanda wote wa Western Cotton Growing Area (WCGA) (yaani mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kigoma, Singida, Kagera n.k). Ushirika ulikuwa ukinunua pamba kwa mkopo na kulipa wakulima pesa yao kwa awamu. Mwaka 1990 wakulima wote hawakulipwa pesa ya malipo yao ya awamu ya pili. Hii iliwakatisha sana tamaa na wengi wao waliacha kulima pamba msimu wa kilimo uliofuatia. Mwaka 1991, bei za pamba zilizidi kuanguka kwenye soko la dunia na hivyo kusababisha ushirika tena kushindwa kununua pamba ya wakulima vizuri ipasavyo, na mzunguuko huu ulipelekea wakulima wengi zaidi kususa kulima pamba misimu iliyofuatia. Mfumo wa masoko ulipoboreshwa kwa kuingia kwa soko huria hapo baadaye, sehemu nyingine zilirudia kilimo cha pamba lakini Nzega ilikoma kabisa na pamba ikabaki historia! Na huu ulikuwa mwanzo wa kushamiri wa kwa umaskini wilayani Nzega. Maana wakulima walilazimika kuuza chakula ili wapate hela badala ya kuuza mazao ya biashara.

  Kampuni ya MSK Solutions Ltd ikishirikiana na Serikali wilaya ya Nzega na Kampuni ya Rural Livelihood Development Company (RLDC) wamejifunga mikanda na kwa pamoja wamefanikiwa kuleta mapinduzi ya ukweli ya kijani. Pamba imerudi tena Nzega, imerudi kwa kasi ya ajabu ambayo haikutegemewa. Kwa pamoja wadau hawa wamekuwa wakiendesha mradi wa Nzega Cotton Development Project (NZECODEP) ambao unafadhiliwa kwa pamoja na wadau wawili, MSK Solutions Ltd na RLDC.

  Mradi huu umeweza kufanikiwa kwa sababu zifuatazo, kwanza umewahakikishia wakulima soko la uhakika na bei nzuri zaidi ya pamba yao. Pili, mradi unahakikisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo cha pamba karibu na wakulima na kwa bei nzuri zaidi. Tatu, wakulima wanahakikishiwa ushauri wa kitaalamu karibu zaidi kwa kuwa mradi unawawezesha posho kidogo mabwana shamba ili kuwatia morali zaidi wa kutoa huduma za ugani.

  Katika uhamasishaji huu, ujumbe mahsusi unaowafikia wakulima ni pamoja na uhakika wa vitu vyote hivi na pia maelezo yanayotoa cost-benefit analysis ya kilimo cha pamba ukilinganisha na mazao mengine na kwamba pamba haikuja kufuta kilimo cha mazao mengine bali kuhakikisha mkulima anakuwa na zao la mbadala endapo ikitokea amekosa mavuno ya kutosha ya mazao ya chakula ama mengine ya biashara atakayokuwa amelima. Pia wakulima wanaeleimishwa kuwa pamba inastahimili ukame ukilinganisha na mahindi na mpunga na hivyo kama mkulima akikosa hayo mazao mengine yote na akapata pamba, atauza atapata hela na kwenda kununua chakula. Na kama akipata mazao mengine, basi atafanya mambo mengine kwa kutumia hela itokanayo na pamba.

  Kutoka kilo 20,000 Mwaka wa Kwanza, hadi 350,000 na sasa Kilo 982,000! Mbali na kukuza kipato cha mkulima mmoja mmoja, pamba itakuwa ni chanzo kipya kikubwa cha mapato ya halmashauri ya wilaya ya Nzega kupitia ushuru wa mazao (district cess) na hivyo kufanikisha miradi mbali ya maendeleo kama mabarabara, shule, zahanati n.k. Pia faida nyingine ni pamoja na kuongeza mzunguko wa fedha na hivyo kutia chachu sekta nyingine za maendeleo na huduma wilayani hapa. Pia kushamiri kutaleta viwanda wilayani hapa. Maendeleo haya ni endelevu na yanagusa watu wengi ukilinganisha na uwepo wa mgodi mkubwa wa uchimbali dhahabu ambapo ikiisha ndiyo basi tena.

  Kikwazo kikubwa kinachoukumba mradi, pamoja na mambo mengine, ni propaganda za kisiasa zinazofanywa na wanasiasa kwa vile tu harakati za kufufua zao la pamba Nzega zinafanywa na kampuni ya MSK Solutions Ltd ambamo Mbunge wa Jimbo la Nzega ana hisa.


  Makala hii imeandaliwa na Ndg. Kumotola L. Kumotola, Afisa Mahusiano, Uratibu na Itifaki - Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega akishirikiana na Ndg. Hassan Jaha, Mratibu wa Mradi wa NZECODEP, MSK Solutions Ltd, Nzega.
   
 2. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa ana mambo ya kitoto, anamzalilisha sana Bashe kwa kumuita majina ya ajabu ajabu. Ktk mtandao wa Fb kuna group linaitwa TANURU LA FIKRA huko hutoa shu2ma za ajabu na kejeli zisizo na mpango kwa Bashe.
  HK piga kazi acha malumbano yasiyo na tija kwako.
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  hehhee heehaahaa!
   
 4. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kamanda, huyu msomali alinianza mwenyewe na sasa he has to face me! He thought I was the likes of Selelii...

  Bora hata mimi namshambulia yeye binafsi, yeye amekuwa akimshambulia Mama yangu mzazi na kwa hili sintomsamehe...sijaamua kuwakosea heshima wazazi wake tu basi, lakini siku ikibidi nitafanya hivyo, maana nina database ya madudu ya familia yake na niko tayari kuyaanika ili kumchafua tu kama yeye alivyofanya na anavyoendelea kunishambulia kwa kutumia makuwadi wake wasio na haya wala aibu!

  Tofauti na yeye, mimi nina kazi nyingi za kufanya na yeye he is got blah blah tu....na hana uwezo wa ku-deliver kazi yoyote ile! Wanaoijua historia yake watasema ni wapi aliwahi kufanya kazi na ikakubalika?! Hivi amewahi kuajiriwa na kufukuzwa kwenye mashirika mangapi? Mtu wa aina hii ndiyo alitaka "kuununua" Ubunge wa Nzega kweli, hivi angetufikisha wapi?
   
 5. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Namna nzuri ya kupambana na adui wako kisiasa ni kuhakikisha unamshinda kwenye uchaguzi unaofuata, na kufanikisha hilo hauna haja ya kuonyesha hasira zako kwake mbele ya umma,bali pandikiza tu shaka juu ya uwezo, umakini na uadilifu wake na wakati huohuo ukiiwaonyesha wananchi uongozi unaokidhi matarajio yao, nakutakia heri sana.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Kingwangalla, kuna kitu hakijakaa sawa kabisa hapa. Inawezekana kabisa Bashe akawa na mapungufu lakini napata shida sana kuelewa inakuwaje kiongozi wa umma anapambana na mwananchi kiasi hiki? Bashe is a private citizen sio mbunge. You on the other hand ni public figure, ni mbunge kwenye bunge la Jamhuri ya muungano. Sasa unapotumia maneno kama 'he has to face me' (see red) unaamisha nini? Narudia wewe ni kiongozi, Bashe ni private citizen, maneno 'he has to face me' - yanazua maswali mengi. Utatumia cheo chako kumshughulikia private citizen?

  Pili, kwenye red, umetumia maneno 'huyu msomali'! Kwa context ya siasa za Tanzania inaonekana kama unamnyanyapaa Bashe kwa sababu tu ni msomali! Hivi watu wenye asili ya Somalia hawawezi kuwa watanzania? Bashe sio mtanzania? Kama sio mtanzania wewe kama kiongozi kwenye chombo cha kutunga sheria umefanya nini kurebisha hili?

  Lakini lililonistua zaidi ni hili: ...nina database ya madudu ya familia yake na niko tayari kuyaanika ili kumchafua tu kama yeye alivyofanya na anavyoendelea kunishambulia..." This is downright incriminating. Unasema waziwazi kuwa utamchafua Bashe! Unbeliavable! Kama Bashe anakuchafua na unao ushahidi kuwa anakuchafua kwanini wewe mbunge usipeleke madai yako mbele ya vyombo vya sheria? Na kwanini kama kiongozi wa umma unakaa kimya pale unapoona familia inafanya madudu (familia ya Bashe)? Kwa nini usitoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika? Unasimamia nini Kingwangalla? Ninachotaka kusema hapa Kingwangalla unaelewa impact ya behaviour yako kwa jamii?

  Kwenye kura za maoni 2010 wewe, Bashe na Mzee Selelii mlichuana. Basha alipata kura nyingi akifuatiwa na Mzee Selelii. Wewe ulikuwa wa tatu. Kwa bahati mbaya governance system yetu iko upside-down hivyo No3 iligeuka na kuwa No1! Kwa maana hiyo una uhakika gani kuwa uchaguzi ujao wananchi hawatachagua kama walivyofanya last time?

  Kwa maoni yangu, unatakiwa ukubali ukweli kuwa kama kiongozi you are expected to bahave in a certain way. Huwezi ukawa unatisha watu hata kama wana makosa. Uko utaratibu wa kisheria wa kutoa haki pale mtu unapoona umekosewa. Na kama mbunge nilitegemea uwe unatambua hilo na sio hizi ngonjera za kila siku kwenye mitandao. Inachosha!


   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kuwa mwangalifu kwani unapokuwa kwenye ngazi ya ubunge wewe ni mwakilishi wa wananchi na kiongozi mkubwa kwahiyo si vema ukafikia wakati unashambulia wasiohusika, cha msingi kama kuna ushahidi wa kutosha wa yeye kutukana wazazi wako mburuze mahakamani na si kutukana wazazi wake
   
 8. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kijana unaonaje ukiacha malumbano na mtu mmoja na badala yake ukajikita zaidi katika kutekeleza ahadi zako huko nzega.Bashe sio mjinga na lazima ujue kuwa anakuchezea mind game ili ujikite kwenye bifu naye badala ya kushughulikia mambo ya msingi.Mbinu anayotumia Bashe haina tofauti na mbinu anayotumia Ferguson kuwavuruga makocha wanaoonekana kuwa tishio kwa timu yake.
  Naamini kuwa wewe ni mwerevu sana kiasi cha kutoyumbishwa na siasa za maji taka.
   
 9. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sasa Dr. Kig unataka kutueleza nini? Cjapata picha hapo...Yeye Bashe na wewe lenu moja tu, kwani wote mko CCM punguzeni jazba mjenge nchi na muwape wana Nzega maendeleo wanayoyahitaji. Asante.
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kigwangala, mi nakubaliana kabisa na wewe kuhusu suala la kupambana na mtu yeyote ili kulinda heshima yako. Tunapambana na ccm ili tulinde heshima yetu kama watu, watanzania na tulinde raslimali zetu.
  Mtu kama anaona njia pekee ya kukuondoa kwenye ubunge ni kukutukana, eti kwa sababu yeye ndo anajiona anafaa kuliko wewe, jibu mapigo kwa namna ile ile mpaka atakapoacha. Nani alliwaambia kuwa vita ina macho?
  Huwezi kumwachia ***** mmoja akutukane eti kwa sababu wewe ni kiongozi usijibu. Yeye kama anajua kuwa wewe ni kiongozi wa wananchi kwa nini asikuheshimu na mkashindana kwa hoja badala ya matusi.
  Endelea kuchapa kazi na kuhudumia wananchi wako. Akileta mchezo jibu mapigo, hata kwa ngumi mzichape. Tumia hekima na usomi wako kupambana.
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh! mkuu wewe kweli ni mbunge unatamka maneno haya?????? Kweli ndiyo maana nchi yetu haiendelei, na hao CCM wanaosema vijana wapewe nafasi kuongoza nchi kama vijana wenyewe ndiyo nyie basi tutaendelea kuishi kwa mazoea hata kwa miaka 200 kama Haiti.
   
 12. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Maoni yenu nimeyasoma na nitayafanyia kazi. Fahamuni kuwa siasa ni siasa na fitna ya kisiasa raha yake itibiwe kisiasa, na ya kisheria ishughulikiwe kisheria! Mimi kuwa Kiongozi haikupi wewe nafasi ya kunitukana, kunikashifu na kisha kunizuia kujibu mapigo! Kama ni hivyo basi wala usiniite Mheshimiwa, niite HK tu inatosha. Kabla sijawa Mbunge nilikuwa na heshima na staha yangu, leo hii badala ya kuongezeka, imeshushwa na 'mtu mmoja tu' - hili halinisumbui sana, maana mi mpiganaji tu na hizi ndiyo kona kona za maisha, lakini kumuingiza mama yangu kwenye siasa za maji taka ni jambo nitakalolipinga kwa nguvu zangu zote! Hata kama ikibidi kumshambulia mama yake huyu mtu...
   
 13. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Suala lake la Uraia si la kisiasa bali ni la kisheria na atatakiwa alirekebishe yeye mwenyewe, na analijua vizuri! Haya mengine ni ya kisiasa na tutapambana nayo kisiasa!
   
 14. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Sikuwahi kuamini kama kila mwanasiasa lazima acheze mchezo mchafu lakini sasa nimeamini kuwa ni lazima tu uingie uwanjani, na tayari sasa nimevaa jezi, akae mkao wa kula!

  Sikuleta mada hapa, watu wake ndiyo wanaonipekua pekua Kwenye mtandao na kuleta issue zangu hapa! Kazi wanayoifanya tumeishaibaini na tutawadhibiti kwa kuwaambia ukweli kama huu bila kuogopa! Selelii alinyamaza na kilichompata ni kutukanwa na kukashifiwa mpaka akapoteza 'mvuto', mimi siko tayari kupoteza 'mvuto' wangu!

  Huyo hawezi kunishinda kwa kura halali, na sasa hata kwa kuniibia. Hata hivyo anatakiwa arekebishe kwanza nyaraka zake za Uraia na akae kwenye matazamio kwa miaka 10 ndipo apewe Uraia, sasa atagombea vipi???
   
 15. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Bashe ni raia wa tz sema magamba mmemchakachua na kilichokubeba ni wama data zako mbona tunazo, malumbano kama mnaimba muziki wa mwambao, kweli magamba ziro yani wewe mbunge kabisa unakosa hekima,mbaguzi wamwita mwenzio msomali dhambi sana sijajua kama sio smart kiasi hicho bro, maisha ya bashe kutoajiliwa we inakusu nini? We mwenyewe wa kawaida tu bro! Unaunga unga! Acha kashfa na dharau kila mtu na maisha.. 2015 piga chini.
   
 16. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mwajua lakini ziumiazo ni nyasi?
   
 17. Z

  Zulqarnayn Senior Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani hizi kauli za Kigwangallah hapa si za kubeza, maana anaonekana kamsoma Bashe na data zake vizuri, itabidi Bashe afuate taratibu mapema aweke sawa nyaraka zake la sivyo ikifika 2015 atapigwa chini tena kama zamani. hapa HK anasema Bashe anatakiwa asubiri miaka 10 kabla ya utata wa Uraia wake kukaa sawa..tehteheteh, sasa HK anaogopa nini, si ammalize tu kisheria kama anavyosema, ama ndiyo fitna zenyewe hizi? Maana kabla ya hiyo miaka 10 si maana yake Bashe bado ni 'msomali' tu kihalali?

  Nilisoma kule FB kwenye kundi linaloitwa Tanuru la Fikra, ambalo inaonesha linaendeshwa na watu wa kundi la EL, HK alikuja juu na kusema Bashe amefoji umri, alikuwa mvuta Bangi primary school na kwamba anagawa pilau na nyama wakati hana hata kibanda! Pia alitumia shortcut kupata hati za Uraia na kujiita yeye mnyamwezi wa Nzega. Inasemekana Bashe alipata Uraia kwa kununua pale makao makuu, kwa kutumia hati za kufoji za kuzaliwa za Mama yake ili kukwepa mahitaji ya kisheria ya kutakiwa kusubiri miaka 10 ipite ndipo apewe hati za uraia. Baada ya kufoji cheti cha kuzaliwa cha mama yake Bashe akajitengenezea uhalali wa kuukana tu Uraia wa Baba yake ambaye aliingia Tanzania baada ya uhuru na kupata uraia halali mwaka 1987 baada ya kusaidiwa na BAKWATA kwa kuwa alikuwa ni ostadhi wa dini ya kiislamu!
   
 18. Z

  Zulqarnayn Senior Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  hivi kumwita mtu jina la Uraia wa nchi yake ni Ubaguzi siyo? Mimi nadhani kama wazazi wa Bashe walitokea huko Somalia na yeye wakati anazaliwa walikuwa bado wasomali, hata kama anajua kiswahili namna gani yeye bado ni woria tu! Kisheria alitakiwa kuukana uraia wa asili ya wazazi wake alipofikisha umri wa miaka 18, sasa kama hakufanya hivyo na bado hajafanya hivyo, maana yake Kigwangalah yuko sahihi.
  Tusilete siasa za makundi ya ndani ya hicho chama chenu hapa, tujadili hoja kama great thinkers wa ukweli.

  Hawa watu wa aina ya Bashe ni wa kuwaangalia kwa umakini sana sisi kama Taifa, maana kama anaweza kwenda kuzunguuka jimboni Nzega mwaka huu wa kwanza tu baada ya uchaguzi na kuanza kampeni huku akipiga marufuku watu wasilime pamba, alizeti wala mtama kwa sababu Mbunge anahamasisha. Ana nia nzuri kweli huyu? halafu hapo hapo kuna taarifa ambazo hajawahi kuzikanusha kuwa uraia wake una utata. hapo mimi nabaki na maswali zaidi ya majaibu?????
   
 19. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  maliyamungu, heshima ni kitu cha bure. Sioni ni kwa nini unitukane bila kukukosea kitu chochote.
  1. Umeniita mse.ng.e
  2. Umeniambia ni mcameroon
  3. Umeniita mi mwana magamba (a.k.a CCM).
  Haya matatu kwangu ni MATUSI mazito tena ya nguoni. Mimi nimetoa maoni yangu kama raia mwingine yeyote anavyoweza kutoa maoni yake. Sijakutukana wewe wala mtu mwingine yeyote. Nashangaa sana wewe kuja hapa na kuanza kunirushia matusi! I can't understand this !!
  Mkuu, umenikwaza sana.
   
 20. Ondio Osio

  Ondio Osio Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona sikuelewi mkuu unamanisha nn?kichwa yako iko sawasawa kweli?au amnazo?.
   
Loading...