Kigwangala ungetulia ungeambulia hata Unaibu Wizara ya Afya kwa staili hii ni kuipinga Serikali ya CCM imeuiba Mgodi
Wewe unayeongelea Kigwangala kupewa Unaibu Waziri, unamfahamua au unaona tu maandishi yake humu JF? Tunaomfahamu tunasema huyu hafai kuwa kiongozi hata wa nyumba kumi. Siyo mtu unayeweza kumwamini kwa lolote, hawa ndiyo wasomi matapeli.
Aliiba jina
Aliiba baruti kwenye mgodi akafukuzwa kazi
Alitoa hongo kama wagombea wengine wa CCM kuupata ubunge
Aliwadanganya wapiga kura wake kuwa atawajengea chuo cha uuguzi
Aliwadanganya wapiga kura wake kuwa atawakopesha hela za kufanyia biashara/kuanzishia miradi
Aliwadanganya wapiga kura wake kuwa yeye ataubana mgodi ili uwajengee shule za kidato cha 5 na 6
Aliwadanganya wapiga kura wake kuwa mgodi umekwishakubali matakwa yake yote
Karibuni hapa ni kuhusu mgomo wa madaktari, nyote mnajua
Hata hayo maandamano aliyoyasema, nina hakika hayatafanyika labda kama atatembea yeye mwenyewe na wale vijana wake ambao huwa anawarushia alfu alfu.