Kigoma yatengwa rasmi, Treni baada ya miezi 6! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigoma yatengwa rasmi, Treni baada ya miezi 6!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Jan 8, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, Serikali imetangaza rasmi kusimamisha usafiri wa reli ya kati kwa muda wa miezi sita. Kama hiyo haitoshi, nimepata taarifa kuwa hata usafiri wa mabasi kutoka Kigoma kwenda Dar na mikoa mingineyo kwa sasa haupo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea nchini hali ambayo imepelekea watu wengi walioenda likizo mwisho wa mwaka kukwama kutokana na mkoa huo kubakiwa na usafiri wa ndege moja tu ya ATCL ambayo hufanya safari zake mara sita kwa wiki.

  Mwishoni mwa mwaka ulokwisha- Desemba 2009, nililazimika kuondoka kwa basi kwenda Dar baada ya kuambiwa kuwa usafiri wa ndege hiyo moja ya ATCL imejaa hadi tarehe 11 Januari! Kampuni ya Precision Air ambayo pia ilikuwa na ndege inayofanya safari za Dar-Kigoma-Dar Kila kusimamisha safari zake kwa muda usiojulikana kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

  Ni mabasi mawili tu yaliyokuwa yanasafiri kutoka Kigoma Tanganyika, kwenda Dar es Salaam, Tanzania kila baada ya siku mbili- Adventure Bus na Saratoga Bus kupitia Nyakanazi-Kahama-Singida-Dar ambayo nayo yamesimama.

  Njia ya barabara ambayo ilitumika kutoka Kigoma kwenda Tabora nayo kwa sasa haitumiki kutokana na kujaa kwa maji kwenye bonde la Mto Malagarasi.

  Peace!
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..sasa hivi Raisi yuko busy na ugeni wa Drogba.

  ..wananchi wa Kigoma,Kilosa,Kilombero, etc, wenye matatizo wasubiri kwanza Raisi na serikali wana ugeni muhimu.
   
 3. b

  bigilankana Senior Member

  #3
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mungu wangu....... sasa tunazalisha Raila Tanzania......Zitto atabeba wabunge wote wa Kigoma katika uchaguzi.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Jan 8, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,876
  Trophy Points: 280
  Wana kigoma jitengeni au mkitaka jiungeni na Burundi-nchi yenu iitwe KigoBuru. Mbona mnachelewa, mkifanya hivyo mtasaidia mambo mengi sana nchini mwetu, kura hazisaidii tena, we need another strategy, na ninaona kasababu ka kufanya hivyo. Anyway hata mkijitoa leo tutasema Kigoma imejiondoa katika nchi ya Tanganyika!na imebaki Tanzania!

  I believe ukombozi wa Tanzania utatokea Kigoma! only Kigoma! wakilianzisha hawa moto utasambaa nchi yote! believe me

  [​IMG]
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu hebu tuwekane sawa hapa,hivi serikali imesitisha safari za reli ya kati ama imetangaza kwamba safari za reli ya kati zitaanzia Dodoma mpaka lile daraja la mto Mkondoa litakapokuwa limekamilika ama??,nieleweshe tafadhali,labda sikuielewa vizuri ile taarifa ya serikali
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nilielewa hivi. Hii kwamba safari zimesitishwa, ndo naliona hapa
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Homeboy, amini niliyokwambia. Hakuna cha treni kuanzia Kigoma na kuishia Dodoma wala nini, tumekuwa tukisikia hivyo lakini ukweli ni kuwa hakuna treni kabisa tangu daraja likatike.

  Nilikuwa huko wiki ilopita na nilitegemea treni ingefika kutoka Dodoma na hakuna hata ngo-ngo-ngo la mizigo! Na ninvyokwambia sasa hivi kuna ndugu zangu wako huko na walitarajia kwenda Dar tangu mwanzoni mwa wiki hii lakini treni haijatokea. Bahati mbaya wamehsachelewa kazini sasa siju kama Serikali itawafukuza kazi au itawasamehe!

  Kwa taarifa yako; wakati treni ilipokuwa ikifanyakazi kulikuwa na treni mbili tu kwa wiki = treni nne kwa mwezi, sasa kama treni moja ilikuwa imeshavuka Kilosa wakati ikienda Dar na ikabaki moja njiani tangu mafuriko yaharibu reli na kuvunja daraja si ingekuwa imeshafika Kigoma?
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Haka kainchi kameoza from left, right , top and bottom. Hizi biashara za kupeana na wahindi bado mna hamu nao tu. Nasikia zile pesa za walipa kodi tayari wamepewa lakini hakuna kitu.
   
 9. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini wakati wa uchaguzi wanathithiemu watafika na kura watapata jamani wananchi wa wa ukanda wa ziwa danganyika angalieni umuhimu wa kura/kula zenu
   
 10. O

  Omumura JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kigoma amkeni jamani, Mungu atawapigania! Hiyo ndo heshima ya serikali yenu ya thithiemu!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  flight za kigoma booking ni weeks b4
   
Loading...