Kigoma: Wananchi wa kata ya Mwandiga walalamika kukosa maji

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
Ikumbukwe wiki moja iliyopita dunia yako tulikuletea makala ilizungumzia kigoma kaskazini kutopata mbunge mwenye kutatua Kero zao. ITV imetoa tarifa kata ya mwandiga aliyo ongozwa miaka kumi na zitto kabwe mpaka Leo wanasumbuliwa na kero ya maji. Napata tabu Sana kuona jimbo lililongozwa na zitto kuwa na kero ya maji wananchi tuwe makini. Nitawaletea makala kuhusu jimbo hilo na kero zote na kueleza kwanini zitto alikimbia jimbo hill. Ukweli usemwe

maji%201_0.jpg

Wananchi wa kata ya Mwandiga katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamelalamikia kata hiyo yenye zaidi ya watu elfu kumi kukosa huduma ya maji licha ya kuwepo mradi wa maji ambao ulishindwa kutoa maji kwa miaka mingi.

Wamemweleza waziri wa maji Mh. Profesa Makame Mbarawa kuwa kata hiyo ilikuwa na mradi wa maji wa Mkongoro lakini haukuweza kusaidia kutatua tatizo la maji na kutaka mradi mpya unaendelea kukamilika kwa wakati ili kuondoa adha wanayopata wananchi

Kwa upande wake mhandisi wa maji wa mamlaka ya maji safi na taka mjini Kigoma Jones Mbike amesema mradi huo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika kata ya Mwandiga huku waziri wa maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa akieleza kuwa mradi huo unaotokana na mradi mkubwa wa maji Kigoma Ujiji utakamilika katika kipindi cha miezi miwili ijayo na ukitumia zaidi ya shilingi milioni mia tisa.

Chanzo:ITV
 
Walikosea kumchagua mbunge asiyewajali Zitto

Mwakani wasifanye makosa wamfirushe
 
Umarufu wa zitto na kujitapa kote ni mbunge wa Taifa jimbo alokaa miaka yote hiyo....hata Maji hakuna. Hahahaha
 
Back
Top Bottom