Kigoma: Mwisho wa Reli, Mwanzo wa Huzuni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigoma: Mwisho wa Reli, Mwanzo wa Huzuni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, May 20, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Leo jioni nilifika pale stesheni Kigoma. Ukweli nilijisikia huzuni sana. Ilikuwa ni baada ya kumpiga picha dada yule mrembo anayeuza dagaa kwenye sinia. Niliuona umasikini wa dada yule aliyezungukwa na utajiri wa nchi yake.

  Anauza dagaa kwa mafungu makubwa. Moja shilingi mia tano. Hakuna wateja. Lakini, Iringa tunanunua dagaa kilo shilingi elfu tano. Nikaona akina mama wale wakiuza migebuka iliyotoka ziwani leo leo. Fungu kubwa la samaki wanauza kwa shilingi elfu tatu.

  Naambiwa, dagaa na migebuka haina soko. Wengi hawana uwezo wa kifedha. Hawana kazi. Hawana masoko ya bidhaa zao za kilimo na uvuvi. Reli ni njia ya pekee ambayo ingekuwa ya uhakika na gharama nafuu kusafirisha bidhaa zao. Reli kwa sasa ni usafiri usio na uhakika kabisa. Inasikitisha.

  Na viongozi wetu wanazungumza tu juu ya umuhimu wa reli, lakini hakuna juhudi za kweli za kufufua usafiri huo. Inasikitisha, kuwa hatuhitaji kujenga upya reli, tunayo. Tunachohitaji ni kukarabati na kuboresha huduma. Tunashindwa. Na watu wetu wanazidi kubaki kwenye umasikini.

  Naam, hata baada ya miaka 50 ya Uhuru tumeshindwa kutambua umuhimu wa reli. Inasikitisha.
  Maggid,
  Kigoma
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,419
  Likes Received: 81,469
  Trophy Points: 280
  .....Subiri Msanii Kikwete atakavyoibadilisha Kigoma mwaka 2250 ili iwe Dubai ya Tanzania.
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Majid! Nchi yetu hii, hakuna mwenye kumjali maskini ama mlalahoi, kila anaepata nafasi anajifikiria yeye kwanza, jiulize tija ya safari za kikwete kila uchwao, linganisha na maisha wanayoishi wananchi wake, Staajabia anapohubiri kila leo nje ya nchi juu ya swala la kutokomeza njaa na umaskini huku akiwa ama hajadhubutu au hajadhamiria kufanya hivyo kwa wananchi yake
  yafaa nini kuhutubia G8 maswala ya kutokomeza njaa na umaskini huku huyawahi kujadili mambo hayo na wananchi wako
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu maggid kwanini umeleta uzi huu saaizi jamani....unataka nilale nalia?.....ujue maneno haya ni mazito sana tena sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Triple A

  Triple A JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 750
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tanzania ni nchi yenye mali nyigi watu wengi wa ulaya wanaililia sana.... hiki kipande tu cha wimbo niliwahi kuimba nikiwa primary....!
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,957
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Wewe si muungaji mkono wa ccm, malalamiko ya nini tena?
   
 7. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bora wewe umeenda Kigoma na umejionea, lakini hapo unaposema ni Kigoma mjini, ukitaka masigitiko zaidi panda meli ya Liemba hapo bandarini Kigoma kulekea kusini, hali vijijini huko ni mbaya mno na kuna mali haina mfano. Tatizo usafiri unaofika huko ni meli ya Liemba na Muongozo tu, watu wanaishi kama vile hawako Tanzania. Huko kuna watu wajawahi ona gazeti la Tanzania, wala hata kusikiliza redio yoyote ya nchi hii. Kuna kijiji kinaitwa Kalya kinawakulima wazuri wa mpunga na mavuno yao yote yanauzwa kwa DRC kwa bei ya kutupa.
   
 8. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  he!..unasemakweli?sasa analalamika nini...anapima upepo
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  pia upite uswahilini dar, wale kule uswahili si wote waswahili(wale wavivu) .Life ndio inawafanya muwe mnawacheka kwa vituko.Na pengine kuwaandika ktk blog zenu wahame warudi mikoani waachie jiji lenu.Huyo dada uliyemwona akija dar(akikosa wa kumgombania na kumtakatisha km akina maimatha) km atapata pa kupanga ni huko mabondeni,na pengine nyumba ya kwanza atanunua huko ili aweze punguza gharama za kwenda uza dagaa maneo ya jiji.(Imgawa umenfagilia pengine akija dar watu wanaweza mgombania na kumpa jiji-ILA ANAWEZA KUWA KESHAPATA FADHILA YAKO INGAWA SI KIHALALI)

  Ukimaliza pita tanzania nzima kuna watu wengi wanaishi hivyo au mbaya zaidi.Ndio utajua kwanini smile zenu ktk magazeti na kauli zenu ni matusi kwa wanaopigika.Wanaoenda omba kazi wanakemewa na kufika maeneo hayo au kupata simu zenu watuw a dili.I hope its not too late kuanza peleka kale kaproject kako ktk real life na si ktk nursery (demo) ,ili kupata hela za wazungu n aumaarufu binafsi na baadaye kuutaka ubunge+
   
 10. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  we muungaji mkono mkubwa wa Ccm hutakiwi kusema haya, au hukujua nini?
   
 11. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Alichokifanya mjerumani kwa muda wa miaka 25 tanzania bara, hakilingani hata kwa chembe tulichokifanya kwa miaka 50 ya uhuru, ni aibu!.
  Embu angalia reli, meli, mashamba, yote yalianzishwa na mjerumani, mpaka taifa lenyewe, sisi tumefanya nini?

  Mwezi wa kwanza nilirudi Tanzania kwa likizo fupi, kwa kweli hali inatisha, hasa vijijini, umesikini umeongezeka kwa kasi ya ajabu.
  Watu niliowaacha wenye uwezo wa kula mara 3 hawawezi tena, kujitibu hawawezi, pamoja na kuwa miaka 3/4 nyuma walikuwa na uwezo huo.

  Pia ongezeko la watu limeongeza shinikizo katika mazingira.
  Kuna uharibifu mkubwa sana wa mazingira kutokana na kutokuwa na nishati mbadala. Gesi tunayo, lakini gharama ni kubwa watu hawamudu.

  Cha kushangaza sasa, wafanyakazi wa serekali walioajiriwa muda mufupi tu uliopita, wanautajiri wa kutisha, sio kwa juhudi zao binafsi bali kwa njia za ujanja ujanja.

  Kwakweli tusitegemee lolote jipya, tulishakosea toka mwanzo wakati tunaanza kujitawala wenyewe, ni vizuri tutazame tulikosea wapi, tujipange upya na wala si kusahau.
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,945
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  ndo kwetu huko. Mkapa enzi zake aliwahi kutangaza dhahiri katika mkutano hapa Mwanga centre ya kuwa 'mnichague au muache, nitakuwa rais wenu'
   
 13. i

  interlacs Senior Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Huko ndo nyumbani kaka; ulipofika ni mjini nenda kigoma kusini, kijiji cha kirando kitongoji cha nyankima kipo karibu na kijijii cha sunuka kwa aliyekua mbunge wa dhamani jimbo la kigoma kusini Mhe Msambya. Huko wanafunzi hawaingii darasani kabla ya kuomba dagaa kutoka kwa wavuvi ( inaitwa kusoroza dagaa), wanafunzi na waalimu wanasubiri vipe viegeshe ndo waingie darasani. ikifika saa sita mchana ni lazima warudi nyumbani kugeuza dagaa walizo anika juani. vijana wengi hawasomi kwa sababu hakuna waalimu darasani. Kule watu hawana habari na serekali, kule wana jesi ni kama wa falme, polisi wananyanyasa ile mbaya, wananchi hawajuwi haki zao kwa sababu wasomi ni wachache.
   
 14. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This is Tanzania....!!!! hadi huzuni. Unaweza kutoa machozi...lakini inasaidia nini? Kama bado wasomi na elimu, tena wamesomeshwa kwa kodi za hawa wanaokula mlo mmoja, wanashabikia ccm na kufuja mali za umma unategemea nini? Na wanachi wenyewe kama vichaa, wanasherehekea kwa kuvaa kofia, vitambaa, tisheti na kanga za kujani na njano kwa muda wa kampeni na kutoa kura kwa ccm huku wenyewe wakikosa kula....! Unamlaumu nani? Japo tunajitahidi kutoa elimu ya uraia, lakin bado hakuna mabadiliko yanayoonekana vijijini na ndiyo maada ccm bado wanajidai kwa sabababu wanajua mtaji wao mkubwa ni UMASKINI WA WATANZANIA HASA WA VIJIJINI!!!
   
 15. n

  ngaranumbe Senior Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fika Kijiji cha Mwamgongo Kaskazini mwa Mji wa Kigoma. Ukifika waweza kuanguka na kufa bila kukata roho, mlo mmoja kwa siku ni jadi, hujisaidia kwenye mawe-hakuna vyoo. Uvuvi umeshuka sana, utoro umekithiri mashuleni, wazazi hawachangii miradi ya maendeleo hata cent 5.Ndio ujue umasikini ni fimbo
   
 16. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mura mimi sio mzalendo tena mura wali sili wala sicheki niko normal tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. n

  ngaranumbe Senior Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pia, Mkoa wa Kigoma umetawaliwa na imani za kishirikina kama Kibondo, Ujiji, Mwambao wa Ziwa, Kasulu, Kazura Mimba na Maeneo mengi ya vijijini, Uvivu na unywaji wa Kahawa huachangia umasikini. Vilevile wivu wa kutokupenda maendeleochangia kwa zaidi ya 70%[​IMG]
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  asante kwa taarifa! unapowaeleza wengine hawajui hali halisi!
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Kitaifa Zitto naona hayo hajayaona ,Na Mwenyekiti mtarajiwa wa NCCR kafulila inaelekea anaona waombarushwa wabunge wenzake tuu ,Na Katibu Mwenezi mpya wa NCCR Machali yeye anayaona ya Mtwara na soko la korosho tuu na Mwanasheria mjanja mjumbe wa halmashauri kuu ya NCCR yeye anachojua ni Kutetea wale wanaoona ubaya wa uongozi wa NCCR na Serukamba kazi yake kubeba mikoba ya wenye fedha kutoa ripoti za utata za wizara kama mwenyekiti wa kamati jamani wabunge uoneeni huruma mkoa wenu embu pigeni kelele kwa nguvu zenu zote acheni kuona aibu kule ni kwenu hata mfanyeje
   
 20. DEMBA

  DEMBA JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 7,295
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kweli tulikuwa tukiaminiii wenyeweee
   
Loading...