Kigoma: Mwalimu aondoa madawati na kuanza kuishi darasani, asema amechoka kuishi uraiani

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
'Mwalimu aliyehamia darasani amefanya hivyo bila mimi kujua, kashaweka mapazia vitanda na kufuli' - MWALIMU MKUU KANDAGA
Mwalimu Mkuu Kandaga athibitisha Mwalimu mmoja kuondoa madawati na kuanza kuishi darasani asema 'nimechoka kuishi uraiani'
=====

Mwalimu mmoja katika shule ya Kandaga iliyopo kata ya Kandaga mkoani Kigoma ameamua kusafisha darasa mojawapo shuleni kwake na kuhamia humo kwa madai kuwa amechoka kuishi uraiani.

Mwalimu huyo amesisitiza siku ambayo atatoka darasani humo ni pale nyumba za shule hio zitapokamilika ambazo zinaelezwa ziko mbili na ipo kwenye hatua ya kuridhisha.

Inadaiwa siku anahamia, mwalimu mkuu hakuwepo na aliporejea alifanya jitihada za kumsihi kuondoka darasani bila mafanikio, akaitisha kikao cha walimu nao wakajaribu bila mafanikio na watu wengine walishindwa.

Inaelezwa mwalimu huyo amehamia peke yake na familia yake bado ipo kwenye nyumba aliyokuwa akiishi awali ambapo nyumba yake mpya shuleni kaweka kufuli na hapatumiki tena kama darasa.
 
Huyo mwalimu yuko mkoa gani, wilaya gani, kijiji gani na shule gani

Watuletea hqbari nusu si dharau hizi,
 
Pengine kaona hilo darasa halina Wanafunzi na lipo lipo tu hivyo kaona bora akae yeye!

Inabidi sasa awe anaamka Saa 11 kujiandaa maana maana akicchelewa tu wanafunzi watamuona Mwalimu yule kavaa taulo na kopo lake lenye mikojo(watu wengi uswahili wanalala na makopo ya kukojolea usiku) anaenda kumwaga.

Hataishi kwa Uhuru sana!
 
KISA NINI KULALA NA KOPO LA HICHO KIMIMINIKA?
 
Back
Top Bottom