Kigoma: Imamu afungwa mika 30 kwa kosa la kubaka Mtoto

Status
Not open for further replies.

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Korti ya Wilaya Kigoma imemuhukumu aliyekuwa imamu wa msikiti wa Wagoma, Hassan Bamba kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa miaka 14.
 
Korti ya Wilaya Kigoma imemuhukumu aliyekuwa imamu wa msikiti wa Wagoma, Hassan Bamba kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa miaka 14.




Amehukumiwa kwa uchafu wake alioufanya na si kwa nafasi yake ya uimamu wa msikiti wa wagoma wala dini yake,mada zenye mlengo wa kuleta faraka hazina nafasi katika jamii ya wastaarabu.

Tusihusishe Uislam na uzinifu wa mtu binafsi.
 
Amehukumiwa kwa uchafu wake alioufanya na si kwa nafasi yake ya uimamu wa msikiti wa wagoma wala dini yake,mada zenye mlengo wa kuleta faraka hazina nafasi katika jamii ya wastaarabu.

Tusihusishe Uislam na uzinifu wa mtu binafsi.
Umeongea kwa uchungu. Ndo tujifunze kuwa na hekima tunapoongea yahusuyo wenzetu. Kuwa kiongozi wa dini au baadhi ya waumini wakipotoka hayo si mafundisho ya hiyo imani au hata kama dhehebu likimeguka basi upotovu sio wa dhehebu lote pia hata imani nyingine wanachoamini hakitakaa kifanane na chako unacho amini!!!. Ndo mana huwa naamini kuwa Mungu si mmoja kwa jinsi tunavotofautiana jinsi ya kumuabudu na mafundisho yake. KILA MTU ATULIE NA IMANI YAKE.
 
Huo ni uchochezi, una maana Bwana Mtume angekuwepo sasa alitakiwa awe Segerea?
haiwezekeni, yaani kwamba angekuwepo leo ilitakiwa TAMWA waandamane kwamba jamaa anyofolewe nanihii yake? Napinga kabisa, kwanza wakati anakashugulikia kabinti ka miaka tisa yeye alikuwa babu wa miaka mingapi?
 
1.png


Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Sheikh wa Msikiti wa Goma, Hassan Bamba (48), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kubaka.

Sheikh huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kitongoni, mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Frola Mtariania, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hakimu Frola, akitoa hukumu hiyo, alisema mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa viongozi wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.
Alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano, pamoja na kielelezo cha PF3, ambacho kilithibitisha kwamba Sheikh Bamba mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Alipotakiwa kujitetea ili kupunguziwa adhabu, akiongozwa na wakili wa kujitegemea Method Kabuguzi, mshtakiwa aliangua kilio na kuiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana familia inamtegemea.
Pia alidai ni kosa lake la kwanza tena shetani alimwingilia. Hakimu Frola alitupilia mbali utetezi huo na kusema:

"Mshtakiwa ukiwa kiongozi wa dini, kitendo ulichokifanya si cha kijamii maana wewe ndiwe unayefundisha watu kuachana na maovu cha kushangaza unakuwa ndiye wa kwanza kuyatenda maovu.

"Sasa utakwenda gerezani miaka 30 ili ukajifunze tabia ya kuwa kiongozi bora wa dini, kwa sababu huku uraiani umeshindwa kuishi na jamii."

Awali, akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Anita Julius, alidai kuwa Januari Mosi, mwaka huu, saa 4 asubuhi eneo la Ujiji Kigoma, mshtakiwa huyo alibaka msichana huyo.

Ilidaikwa kuwa siku ya tukio mtoto aliyebakwa akiwa na pacha wake, ambao baba yao ni rafiki wa sheikh huyo, walikwenda kwa sheikh huyo kwa ajili ya kuombewa duwa na kufanyiwa dawa kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kuingia darasa la saba.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, baada ya kufika, Bamba alimtuma mwenzake aende shuleni kuchukua mchanga na ndipo alipomfanyika kitendo hicho yule aliyebaki.

Mwenzake aliporejea, ilidaiwa kuwa alimkuta pacha wake analia na alipomuuliza alimjibu kuwa amebakwa na Bamba.

Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, wakiwamo waumini wa msikiti aliokuwa akiswalisha, ulikusanyika mahakamani na kushuhudia Sheikh huyo anapelekwa jela.


Chanzo: Mpekuzi
 
Huyo sio Shekhe ni mhuni tu......hata kanzu hana na kavaa fulana ya 50 Cent? Hawa waandishi maamuma wanauchafua sana Uislamu

Mkuu sio kila kiongozi wa dini ana wito na hiyo dini, wengine hutumia dini kama kichaka cha riziki, hivyo usitetee kua huyo sio sheikh. Hata ma Padre sio wote wenye wito. Nakutahadharisha hawa viongozi wetu wa dini sio wa kuwatetea, unavyomwona nje sivyo alivyo rohoni
 
Shetani analo kila baya afanyalo binadamu ni yeye anawapitia sijui huwa wanaenda wapi na huyo shetani?
 
Ni huko msikiti wa Goma, Kigoma, anaitwa sheikh Hasan Bamba.
Mahakama imetoa adhabu hiyo I we fundisho kwa wengine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom