Kigogo wa Polisi akwapua bil.2/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo wa Polisi akwapua bil.2/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Oct 17, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kigogo wa Polisi akwapua bil.2/-

  Na Mwandishi Wetu

  WIKI mbili baada ya gazeti hili kuandika habari za wizi wa mabati katika eneo la Chang’ombe uliohusisha polisi, kuna habari kuwa Jeshi hilo sasa linamshikilia kigogo wake ambaye anatuhumiwa kwa mauaji na wizi wa takriban Sh bilioni mbili.

  Ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amekanusha kuwapo kwa taarifa hizo katika vituo vyake, chanzo chetu kimethibitisha kukamatwa kwa Inspekta Msaidizi wa Polisi (jina linahifadhiwa) kwa tuhuma hizo.

  Tuhuma hizo zilizofunguliwa jalada namba BUG/IR/4723/2010, katika kituo cha Polisi Buguruni, ni za tukio la wizi na mauaji yaliyotokea Mei 26 mwaka huu katika kampuni ya usafirishaji ya Tawaqal iliyoko Buguruni karibu na kituo cha Polisi, ambapo iliibiwa Sh bilioni 1.9.

  Inadaiwa kuwa watu wasiojulikana, wakiwa na askari huyo, walivamia ofisi hizo usiku wa kuamkia Mei 26 na kupambana na mlinzi wa kimasai na kumuua eneo la tukio na kufaulu kuondoka na kiasi hicho cha fedha.

  Habari zingine kutoka kituo cha Polisi Buguruni, zilidai kuwa raia mwingine maarufu kwa jina la Masai anashikiliwa pia kuhusiana na tukio hilo, baada ya kubainika kuwa ndiye aliyeamriwa na Inspekta huyo kulinda wakati wizi ukifanyika.

  “Huyu ndiye aliyeanika habari hizi baada ya kusikia kwamba fedha zilizoibwa ni nyingi na yeye alipewa mgawo wa Sh milioni 15 tu ndipo akahisi kupunjwa akaanika mpango wote,” chanzo chetu kilisema.

  Kiliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo, Inspekta huyo alinunua gari dogo ambalo aina yake haikuweza kufahamika mara moja, na hivi sasa amehamishiwa kituo cha Polisi cha Selander Bridge.

  Akizungumza na gazeti hili, Dar es Salaam jana, mmoja wa maofisa wa Tawaqal ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu za kiusalama, alidai kuwa pamoja na kutokea kwa tukio hilo, polisi wamekuwa wakisuasua kulifuatilia kwa kina.

  “Tukio lilitokea Mei 26, kati ya saa tisa na kumi usiku. Mlinzi wetu Nelson Lameck, aliuawa katika tukio hilo na wizi wa fedha na mali nyingine nyingi ulifanyika.

  “Polisi walikuja kama mara mbili au tatu mwanzoni na kuuliza hili na lile, lakini baadaye waliacha kuja hadi sasa hatujui kinachoendelea,” alisema ofisa huyo.

  Akizungumzia kiasi cha fedha kilichoibwa, ofisa huyo alisema wavamizi waliiba fedha nyingi zilizokuwa zimehifadhiwa katika ofisi ndani ya karakana hiyo ya Tawaqal, lakini alishindwa kutaja kiasi kwa madai kuwa Mtunza Fedha anayejua kiasi hicho jana hakuwa ofisini.

  Alisema pamoja na fedha, pia wavamizi waliiba kompyuta ndogo moja, skrini ya kamera maalumu za usalama na nyaraka mbalimbali.
  Chanzo: Habari Leo

  My take: Inashangaza kwa gazeti hilo la serikali kuja na habari kama hii kuhusu ujambazi/ufisadi wa polisi wao. Hii ni kwa sababu tukio hilo halihusishi vigogo wa ufisadi wanaoifadhili CCM.

  Nimeelezwa na mtu wa kuaminika ndani ya idara hiyo ya polisi kwamba Habari Leo walikuwa wamelipata lile tukio la Mengi kuhusu polisi kutaka kumbambikia mtoto wake madawa ya kulevya lakini gazeti hilo halikutaka kufuatilia habari hiyo kwa vile mtuhumiwa ni kigogo mmoja wa ufisadi anayechangia kampeni za CCM!

  Shame upon you Habari Leo!

   
 2. T

  Tajiri Mtoto Senior Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 131
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  • Kwa nini kiasi chote hicho cha pesa kilikuwa ofisini?:nono:
  • Huyo "Polisi" na wote aliokuwa nao walijuaje kuwepo kwa fedha hizo ofisini?:nono:
  • I take it mpaka kuwa na amount hiyo ofisini, hii ni big entity. Inatosha kweli kuajiri mmasai kwa ajili ya ulinzi? Nilitaraji kuna kampuni ya ulinzi!
  I think it is high time kwa watu/wafanyabiashara kufanya transactions zao kupitia mabenki. Ninachokiona hapa ni ukwepaji wa kodi ndio unaopelekea watu kufanyia transactions mitaani.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi na wale waliotuhumiwa na Mengi bdo wapo kazini?
   
 4. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe Tajiri Mtoto Billion 2 ni kiasi kikubwa sana kuwekwa ofisini. Nadhani habari hii ina walakini.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa habari leo ni serikali na wamekuja hii ishu. basi amini kwamba credibility ya hii ishu ni likely bila hofu.
  Ila mie take yangu ni kwamba hizo pesa ni nyingi mno kuwepo kwenye kasiki. huyo mwenye mali akamatwe kwa kutengeneza mazingira ya kifo cha staff wake. na pia achunguzwe kama analipa kodi. na hiyo ya polisi tunamtaka kova aje public kukanusha.
   
 6. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wizi mtupu....kila kona.....kisha mnatarajia eti nchi iwe na maendeleo!
   
 7. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Nafikiri kiasi cha pesa kimeongezwa na mwenye mali makusudi maana itawezekanaje ofisi iwe na bilioni 2, maswali ya kujiuliza zilikuwa za mauzo? kama hapana zilikuwa za kufanya malipo hani ya cash?? nisaidieni mawazo kupata rationale
   
Loading...