GE2025 Kigogo wa ACT Wazalendo atua CHAUMMA

GE2025 Kigogo wa ACT Wazalendo atua CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,450
Reaction score
5,279
Aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Kagera wa Chama cha ACT-Wazalendo, Linus Maeje (Meja) amejiondoa kwenye chama hicho na kujiunga rasmi na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) leo Jumamosi Julai 19 2025 Mjini Karagwe mkoani Kagera.

Meja mepokelewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari kwa Umma wa (Chaumma), John Mrema aliyeambatana na Naibu Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu, Ester Fulano.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mrema tangu Julai 10 mwaka huu yupo Kanda ya Victoria kusimamia shughuli ya wanachama wa chama hicho wanaotia nia ya kuomba kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kuwapokea wanachama wapya wanahitaji kujiunga na chama hicho.

Screenshot 2025-07-19 194352.png
 
Back
Top Bottom